TANESCO ibinafsishwe ili kuongeza tija

Dig the EA

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
279
270
Tatizo la Umeme nchini ni kubwa sana. Tatizo hilo ni la muda mrefu, miaka mingi sana. Mikakati na mikakati imekuwa ikipangwa lakini hakuna kinachoendelea.

Kuna miaka ya nyuma ilisemwa kuwa ile gas ya Mtwara ingemaliza kabisa tatizo la Umeme nchini, lkn hakuna kilichotokea.

Taifa au serikali inasita nini kubinafsisha TANESCO? Kama Bandari kubwa ya DSM imebainishwa, kwa nini TANESCO isibinafsishwe.

Bandari ya DSM kwa umhimu wake, uzito wake na mashiko yake kwa taifa imewezekane kubinafsishwa, kwa nini TANESCO isibinafsishwe.

Kuna shida gani TANESCO ikibinafsishwa? Watu kwenye majukumu yao ya kutafuta chochote, maofisini, kwenye mashirika wanashindwa kufanya kazi zao vzr sababu ya umeme kukatika mara kwa mara. Umeme haupatikani zaidi ya masaa kumi kwa siku, tena mchana.....watu wataishije.

Shida iko wapi, je ni uzalishaji wa umeme, je ni usambazaji au ni nini ? Atafutwe mwekezaji aendeshe TANESCO ili nchi isiwe gizani. Ni wakati muafaka sasa TANESCO ibinafsiswe.
 
Back
Top Bottom