TAMWA ZNZ yatoa wito kufanyike utafiti kuhusu ongezeko la vitendo vyaudhalilishaji Zanzibar

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kinashauri Serikali kufanya utafiti ili kubaini sababu zinazopelekea kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji Zanzibar na kwa nini bado kesi nyengine hazipati hatia, ili Serikali na wadau kwa pamoja waweze kuchukua hatua stahiki kuzuia vitendo hivyo.

TAMWA ZNZ inaamini kwamba udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ni ukiukwaji wa haki za binadamu na wahanga huathirika kimwili, kisaikolojia na kiuchumi hali inayochangia kurudisha nyuma maendeleo yao na jamii.

Ripoti ya mwaka ya udhalilishaji na ukatili iliyotolewa na Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali hivi karibuni imeonesha kuwa idadi ya matukio yameongezeka kwa asilimia 43.7 kufikia matukio 1,954 mwaka, 2023 kutoka matukio 1,360 mwaka, 2022.

Ripoti hiyo inaonesha pia kuwa watu ambao wamepatikana na hatia ni asilimia 19 kwa mwaka 2023 ambalo ni ongezeko la asilimia sita kutoka asilimia 13 mwaka jana.

Hili ni ongezeko chanya kwa upande mmoja kuwa vyombo vya sheria vimeongeza juhudi ya uchunguzi na utowaji wa haki.

Hata hivyo, juhudi zinahitajika katika sehemu zote mbili za kukinga vitendo hivyo visitokee na pia kuwaadhibu watendaji na hivyo utafiti utabainisha vyanzo hasa vya hali hizo na suluhisho la kila moja.

Tafiti za kihabari za hivi karibuni kuhusiana na kuongezeka kwa vitendo vya

ukatili/udhalilishaji zimebainisha kuongezeka kwa matumizi ya mitandao kwa vijana hasa wa vijana wa kiume, kutokuwa na uangalizi mzuri wa watoto majumbani na ukosefu wa elimu ya kujitambua na kuzuia mihemuko kwa watendaji.

Kwa upande wa adhabu kuwa bado ni asilimia ndogo inaweza kutoa mitazamo hasi kama; rushwa muhali, rushwa ya fedha na kukosa uwajibikaji kwa Maafisa kutoka vyombo vinavyoshughulika na utoaji wa haki.

TAMWA, ZNZ inawasihi wananchi wote wa Zanzibar, wakiwemo viongozi wa Serikali, asasi za kiraia, na wadau wengine kushirikiana ili kudhibiti na kumaliza matukio haya yenye madhara makubwa kwa jamii, hasa wanawake na watoto.

TAMWA ZNZ inaamini kwamba Zanzibar bila ya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto inawezekana iwapo kila muhusika atachukuwa wajibu wake ipasavyo.

View attachment 2886208
IMG_20240128_121251_304.jpg
 
Shida ya huko kubwa ni kufukua mifereji halafu wababa wanafukua Hadi watoto wa kuwazaa kibaya zaidi "THEY ARE FIVE ANTELOPES"
 
Back
Top Bottom