Tamko la Wazee wa CHADEMA , trilioni 8 za wastaafu, Sheria ya Makosa ya Mitandao, Sheria ya Magaze..

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Ndugu waandishi wa habari, tunapenda kuwashukuru kwa kuitikia wito huu wa kukutana nanyi leo kama ambavyo imekuwa kawaida tunapokuwa na jambo la muhimu kuwasemea wazee wote nchi nzima, kuishauri serikali na jamii yetu juu ya masuala anuai yanayohusu maslahi ya nchi yetu, kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tumekuwa tukitimiza wajibu huu wa kupaza sauti kwa niaba ya wazee wote nchi nzima kwa kuzingatia kauli mbiu ya Baraza la Wazee wa CHADEMA isemayo “Wazee Ni Hazina ya Hekima na Busara”.

Tunapenda pia kutumia nafasi hii ya utangulizi katika mkutano huu, kuunaungana nanyi wanahabari wa Tanzania na wadau wengine wote wa masuala ya habari nchini na dunia nzima kwa ujumla katika kuazimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambayo huazimishwa Mei 3, kila mwaka kwa madhumuni ya kujikumbusha misingi muhimu katika uhuru wa habari, kutathmini mwenendo wa uhuru wa habari kuutetea na kuulinda uhuru huo dunia nzima dhidi ya mashambulio au vitisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao wakitimiza majukumu yao ya kutafuta, kuzalisha na kusambaza habari.

Tunajua hapa nyumbani, Watanzania wanaadhimisha siku hii ya leo wakiwa katika sintofahamu kubwa kwa sababu uhuru wa habari na upatikanaji wa taarifa kwa jumla unapitia katika wakati mgumu kabisa kuliko hata ilivyokuwa wakati wa ukoloni au kuliko enzi za tawala za kidikteta kama akina Benito Mussolini, Adolf Hitler na wengine.

Hujuma, vitisho au mashambulizi dhidi ya haki ya kupata taarifa, uhuru wa habari na wanahabari wenyewe ni mojawapo ya viashiria vikubwa vya jamii inayoongozwa na watawala waliojaa hofu ya kuhojiwa na wasiokuwa tayari kukubali fikra mbadala. Jambo ambalo ni hatari kwa afya ya taifa. Tunaamini kuwa Watanzania wataitafakari kwa kina na kuifanyai kazi kauli mbiu ya wadau wa habari nchini Tanzania kwa mwaka huu, inayosema “KUPATA TAARIFA NI HAKI YA MSINGI, IDAI’.

Tuitumie kauli mbiu hii kuwaambia watawala kuhusu;

Sheria mbovu zinazominya uhuru wa habari na kukandamiza upatikanaji wa taarifa. Mf;

Sheria ya Magazeti

Sheria ya Takwimu

Sheria ya Makosa ya Mitandao

Kuzuia upatikanaji wa habari za bunge na taarifa kuhusu wawakilishi wetu wanavyofanya kazi.

Kuzuia vikao vya bunge kuwa ‘live’

Kuwa hivyo ni viashiria vya kuturudisha nyuma na si kwenda mbele na kamwe hatuwezi kuwa mfano wa kuigwa na watu makini wanaofikiria ustawi wa jamii zao vizazi vingi vijavyo na kwamba tunalaani vikali kurudisha nyuma demokrasia.
2.0 Ukimya wa Rais kuhusu ufisadi wa Trilioni 8 za Wafanyakazi, Wastaafu.

Ndugu wanahabari, baada ya kuzungumzia kwa kirefu kuhusu hali ya uhuru wa habari nchini kutokana na umuhimu wake, tunaomba kuzungumzia hotuba ya Rais J.P. Magufuli aliyoitoa kwa taifa, Siku ya Mei Mosi ambayo hutumika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.

1. Tunawashukuru wadau wa maslahi ya wafanyakazi wa nchi hii, hususan wachumi ambao wameonesha kwa hesabu zilizo wazi kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushusha kiwango cha kodi ya PAYE kwa asilimia 2 (ambazo ni pesa kidogo) bila kuboresha mishahara ni utani kwa wafanyakazi wanaoendelea kuhangaika na kima cha chini ambacho bado hakitoshelezi mahitaji.

2. Kwa niaba ya Wazee, tunamsihi Rais Magufuli kutoa kauli juu ya hatma ya trilioni 8.43 ambazo ni jumla ya deni kwa mujibu taarifa ya CAG, ambalo Serikali inadaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Wafanyakazi na wastaafu walitegemea kumsikia Rais akizungumzia suala hilo siku ya Mei Mosi.
3. Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa ikiitaka Serikali kufanya jitihada za haraka za kunusuru uhai wa mifuko hiyo kwa kulipa fedha walizochota kwa ajili ya uwekezaji katika miradi mikubwa mingine ikiwa haina tija na iliyojaa harufu ya ufisadi mkubwa.

4. Deni hili sugu la serikali yanatishia uhai wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini. Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko hiyo (SSRA) iliwahi kutoa angalizo kwa serikali kuwa iwapo serikali haitalipa madeni hayo itakwamisha mifuko hiyo kuwalipa mafao wanachama wake, kujiendesha yenyewe na hata kuwekeza zaidi. Taarifa zinasema kuwa fedha zingine zimekopwa na serikali bila hata ya kuwepo kwa mikataba. Huu ni ufisadi. Hizi sio fedha za serikali.

5. Madhara ya hali hiyo yako wazi. Yamesababisha kumekuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wastaafu kuhusu ucheleweshwaji wa mafao yao na hata wengine kufariki dunia kabla ya kupata malipo yao.

6. Kuchelewesha malipo ya mafao ya wastaafu husababisha usumbufu mkubwa na hata kuwaathiri kisaikolojia na kiafya na kuwafanya waishi maisha ya mateso katika umri wao wa kustaafu ambao walipaswa kuangaliwa vizuri na kufurahia mafao yao.

7. Ni madeni haya sugu ya serikali kwa mifuko, yamesababisha kuwepo na mlolongo wa muda na urasimu mkubwa kwa wazee kupata malipo ya mafao, wakati katika nchi zingine inachukua mwezi mmoja tu mtu kupata mafao yake.

8. Mbali ya kutoa kauli, pia kwa sababu ya kuwepo kwa maneno mengi yanayoashiria kuwepo kwa harufu ya ufisadi katika baadhi ya miradi hiyo, Wazee tunamsihi Rais Magufuli kumwagiza CAG afanye ukaguzi maalum katika madeni hayo ya serikali kwa mifuko ya jamii.

3.0 Michango ilizokusanywa na Mifuko ya Hifadhi Jamii kutoka kwa wafanyakazi hewa zitumike kutoa pensheni kwa wazee wote nchini.
Katika hotuba yake hiyo kwa taifa Siku ya Wafanyakazi, Rais Magufuli alisema wafanyakazi hewa wamekuwa wakilipwa shs bilioni 11.6 kwa mwezi, sawa na sh Billioni 139.2 kwa mwaka na sh billioni 696.1 miaka mitano.

Kwa mantiki hii inamaana kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikipokea michango ya wafanyakazi hewa, ukichukulia mchango wa asilimia 10% kila mwezi kwa kila mfanyakazi kwa mijibu wa sheria, utakuta mifuko ya hifadhi ya jamii imekua ikipokea Sh. Billioni 1.16 kwa mwezi, na Sh. Billion 13.92 kwa mwaka sawa na Sh Billioni 69.61 kwa miaka mitano kwa kutumia takwimu za Mh. Raisi hapo juu.

Baraza la wazee CHADEMA linapendekeza michango hii ya wafanyakazi hewa iliyokusanywa na mifuko ya jamii kwa muda mrefu ifuatiliwe na itumike kuanzisha mfuko wa Pensheni ya Wazee wote nchini (wale waliofanya kazi kwenye sekta rasmi na sekta zisizo rasmi) ambacho kimekuwa ni kilio cha wazee cha muda muda mrefu.

Msingi wa kutoa pensheni jamii kwa wazee wote unatokana na hali halisi na changamoto zinazowakabili wazee katika maisha yao pia ni haki yao kwa mujibu wa Azimio la Kimataifa la Haki za Bina Binadamu la mwaka 1948 ibara ya 25 inatamka haki ya hifadhi ya jamii wakati wa uzee.

Mwisho

Imetolewa leo Jumanne, Mei 3 na;
Rodrick Lutembeka
Katibu Baraza la Wazee CHADEMA
 
Do mmeishiwa kweli jamani ,swala la wafanyakazi hewa ni ubunifu wa rais wetu ,sasa mnamfundisha jinsi ya kulishughulikia wakati ,wakati mei mosi alilizungumzia kwa kina tafuteni hoja zenu za kupandia sio kudandia dandia vitukio
 
Back
Top Bottom