Tamko la Vijana 'WASOMI' wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma Dhidi ya wabunge wa CHADEMA

Nyie mnaojifanya wasomi wakati ni wavivu wa kufikiri acheni hizo,ni wapuuzi na ccm itawafanya kama kondomu.Baada ya kuwatumia na mikopo mtaendelee kupata kwa shida.Mlitaka wananchi waandamane ndipo mjue kuwa uchakachuaji ulifanyika.Ninawapongeza wabunge wa Chadema kwa kufanya hivyo na tunasubiri mchanganuo jinsi hawa walivyoiba mpaka dunia nzima ielewe huyu jamaa si rais halali ila katiba mbovu ndio inamuweka madarakani.Hongera sana Chadema na tunasubiri taarifa rasmi kuhusu jinsi mafisadi hawa walivyoiba kura.

Wananchi wataandamana??Mdau mmoja kaniambia jana wabunge wa chadema walikuwa wanakunywa wine baada ya kutoka nje ya bunge pale dom hotel,tena kwa hela yetu wavuja jasho.Wote wezi tu
 
Hamna elimu hapo ngoja cream ya taifa ijipange pale jijini ndo tutajua, hao ni makapi ndo maana wanatoa tamko kama hilo hawajui hata kwa nini wako shule
 
tupe picha uliyonayo kama ushahidi ya kuwa walikuwa wanakunywa wine, la sivyo hapa si mahali pa umbeya tafadhali.
 
Ni wasomi kwa sababu ya kuingia kwenye madarasa / majengo ya vyuo vukuu lakini ni wasomi ambao hawajaelimika. Could be DNA zao zina elements za ufisadi zitakuja kujidhihirisha watakapopata uongozi kama mbunge mmoja wa kule ungonini.
 
Hongereni sana kwa Tamko, mmedhihirisha kuwa TANZANIA BILA CCM HAIWEZEKANI, KEEP IT UP KUAMSHA BONGO ZAO ZILIZO LALA !!!!
 
TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.

NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
NDUGU WANANCHI,.

Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.

Wassomi mtakuwa nyie.....?!
 
Hivi walikaa lini mpaka kufikia maamuzi hayo?

Ujumbe umejaa makosa mengi hata unashangaa ni wasomi walioandika au ni vijana wa mitaani?

Mungu ibariki Tanzania.
 
Dah maajabu ya musa haya.... Hawa si Vijana wasomi ila ni Vijana wasomewa....

Hiki kitu ni ujinga mtupu hawajui lile wala hili.. hope wanasoma kindergarten si chuo.

Msomi wa chuo hawezi hata kuchanganua nini maana ya wabunge kutoka ndani ya bunge au mfano hata wabunge wanapo simama kuna maanisha nini?

Kiukweli hao vijana bado wana kazi kubwa ya kuchanganua mambo achilia mbali kuwa wanasoma lakini bado upeo ni mdogo sana.

wajifunze vitu na wawe wanauwezo wa kureason kwanini napewa hii karatasi kuisoma kwa media vinginevyo ni yale yale ambayo hawajua wanacho kisoma katika fani au hata kufikiria kinachofundishwa kina maana gani kwao.

yale yale ya kumeza kitu na kukitoa kama kilivyo bila kutafakari .

poleni wasomi wa taifa lijalo sijui la sisiem au la wasomi kutoka UDOM?

Its real nonsense kuita waandishi wa habari kuongea ujinga huo.
 
Wananchi wataandamana??Mdau mmoja kaniambia jana wabunge wa chadema walikuwa wanakunywa wine baada ya kutoka nje ya bunge pale dom hotel,tena kwa hela yetu wavuja jasho.Wote wezi tu

Wewe ni mwongo na mwizi mkubwa kwa 2010 yote, toka lini wabunge wa chadema wakala vijisenti vyako? waache kina Sugu wajichane kufuta vumbi walilopata kwenye uchaguzi...weee ulie tu na safari hii mnalo
 
pure nonsense; they didnt walk out of their resposibility, but out of their responsibility to the people they represent. Hivi hawa vijana wanawakilisha wenzao wote, au ni kundi tu lililonunuliwa na CCM mafia; for heavens' sake; vijana ndio wanaokuwa more affected by this unfair system, no employment, when they are employed they ar egiven meagre salaries, and when they complain, "I do not need your votes" etc. Mama zenu na baba zenu wanahangaika na ukata vijijini, halafu you bring this nonsense!!!! Someni mpate busara, na si kusoma kuendeleza ujinga, otherwise they is no need mtumie country's resources to harbor foilly; that you can get it even without going to school
Wasitupe shida haya ni mapandikizi ya mafisadi, hawajui kiwalacho ki nguoni mwao. Hizi elimu zifike mahali ziwe na manufaa kwetu. tena hiyo risala ukifuatilia haiwakilishi mawazo ya hata nusu ya wanafunzi wa Dodoma University. Wanadhani kwa maelezo hayo RA na nchi yake wataongeza funds
 
KWANZA SIAMINI KAMA HAO WATOTO NI WASOMI KWELI, NA KAMA NI KWELI BALI MBONGO ZAO ZIMEATHIRIWA AU NI MATOKEO MABAYA KABISA YA SHULE ZA KATA, TUNAWAHESHIMU SANA, HEBU NIWAULIZE KATI YENU NI WANGAPI WAMEPIGA KURA, SASA MNAWEZA MKAACHA KUIPIGIA CHADEMA HALAFU MUONE KAMA HII NCHI HAIJAKOMBOLEWA BILA NYINYI. MMENIKERA SANA SI NINYI MLIOKUWA MNAANDAMA JUZI KUDAI MIKOPO IMECHELEWA MARA HII MMESHAHAU? LABDA NIAMBIWE KWAMBA HUU WARAKA SIO WENU, PUUU, FULL UPUPU!:A S angry:
 
Kama kweli hawa ndiyo wasomi wetu then tuna matatizo makubwa sana nchini kwetu. Ingekuwa Kenya au Uganda wasomi wangekuwa wanawaunga mkono Chadema. Ila hawa wasomi wa UDOM sijui wanamatatizo gani?? Ngojeni waingie mtaani ndipo watajuwa??

Huwa nafikiria njisi tulivyopigana na cost sharing naona kizazi chetu kilikuwa kinaelewa kinafanya nini. Hivi kweli that time tungekuwa na akili kama hii si leo hata hiyo mikopo isingekuwepo!!

Shame on You Wasomi wa Dodoma!!
 
Poleni sana wadogo zangu.

Kama mmetumwa basi nawaomba muepuke kabisa kudanganywa na watu wachache kwa maslahi ya hao wachache. Na kama ni msukumo wenu wenyewe, basi pole tena, maana mko gizani.

Kwanza niwatahadharishe kuwa mjue kuwa elimu mnayoipata sasa hivi imebaki jina degree. Quality ya elimu mnayoipata ni dhaifu sana, na sababu kubwa ni utawala mbovu. Hivyo wakati mnaendelea na masomo wekeni bidii sana ktk kusoma vitabu na pia jaribuni kuwaangalia wenzenu vyuo vingine vya nje wanafanya nini.

Pili, naomba mjue kilifanywa na CHADEMA, ni kwa faida yenu nyinyi kama watanzania. Kwa maana hiyo basi tumieni njia hiyo hiyo kuwaomba CHADEMA na watanzania radhi kwa kuwa hamkupata muda kulitafakali jambo hilo. Na katika hilo hamtajututia mliyoyasema.

Mwisho, niwatie moyo THINK BIG and GLOBALLY.
 
Kwanza nimeshangaa sana walivyojiita "WASOMI" kwa maoni yangu mtu hawi msomi hadi awe amemaliza/amehitimu kile anachokisomea!!

Ukichambua sana Dodoma kuna Chuo Kikuu Kimoja tu, UDOM, ambacho hata hivyo ni kama zilivyo sekondari za kata nacho naweza kukiita ni "CHUO CHA KATA"..vitoto vidogo visivyoelewa muelekeo wa nchi hii kisiasa wala kiuchumi! Watoto hao wanaojiita wasomi wanatafuta umaarufu kwa kuitisha vikao na baadhi ya waandishi wa habari ili wajifanye wanawakilisha wasomi wengine...100% nonesense!! Hivi hao watoto ni nani kati yao ana usomi kuliko say; Mabere Marando au Tundu Lissu? Wanadhani kina Mnyika hawakufika chuoni? Wanafikiri Chadema hawafahamu wanachokifanya? They are completely of everything......

Uamuzi wa Chadema ni wa kisiasa na at the political strategy ni wa manufaa kwa Chadema na kwa watanzania wote. Ni ujumbe tosha sasa kwa ulimwengu mzima kufahamu kwamba baadhi ya vyama vya upinzani havimtambui Rais...kila mtu atajiuliza WHY? and it is from this interest that the evils of CCM will be revealed!

Hao wasomi uchwara wanaodanganyika na vibia na mishikaki ya bure watuondolee upuuzi wao...

Chadema wamefanya lililo sahihi as a strategy kwa chama chao!
 
Leo ndiyo nimeamini kuwa humu JF kuna vilaza na mbumbumbu wakubwa. Hiyo taarifa ya vijana inajieleza na iko wazi kabisa. Oneni aibu na muwashauri wabunge wa Chadema. Soon or later they will go out of sight mirror completely!
 
Waraka huu umesomwa muda si mrefu mbele ya vyombo vya habari zaidi ya 15 huko Dodoma.

TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.

NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
NDUGU WANANCHI,.

Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.

Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.

Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.

Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja’ je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?

Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.

Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.

Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .

Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.

Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.

Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.

Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.

Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.

Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.

Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.

Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.

Aksanteni sana.

IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD

KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA

hako ni katiwi ka-CCM pale UDOM, si ndio walichanga hata hela za kuchukulia form na za JK!
 
Waraka huu umesomwa muda si mrefu mbele ya vyombo vya habari zaidi ya 15 huko Dodoma.

TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.

NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
NDUGU WANANCHI,.
wali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.

Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.

Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.

Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja' je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?

Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.

Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.

Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .

Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.

Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.

Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.

Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.

Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.

Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.

Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.

Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.

Aksanteni sana.

IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD
KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA

Ndugu zngu, hawa sidhani kama ni wasomi ukiangalia sehemu zenye red utangudua hapa hakuna vijana wasomi bali ni genge la wahuni wa kisiasa, msomi gani anakosea maneno kiasi hicho, au hawajafanya proof reading ya hicho walicho kiandika?

Vyo vikuu mbalimbali Dodoma ni vipi? Hawa wanawafamu wananch walio wachagua wabunge wa Chadema hadi weseme kwamba wanach waliowapigia kura hawakubaliani? hawa wamefanya mahojiano na hao wananchi?

Ndugu zangu, hawa wasomi kama wale wa REDET walianza hivihivi. Taifa hili tutalikomboa pale tu wasomi watakapo tumia usomi wao ili kuleta mabadiliko, acheni njaa vijana fuateni masomo hizo siasa waachieni wanasiasa wenyewe na wala msikubali kutumia na watu, Taifa letu linahitaji mabadiliko ya kweli kimfumo wa ungozi ili kuleta madiliko kuanzia ngazi ya chini kabisa ya mtanzania anaeishi maisha ya shida na vijana ndio wenye jukumu la mabadiliko.

Watanzania tuache ushabiki, unafiki, usaliti na pia tujitambue, hizi njaa hizi zitatuua
 
Back
Top Bottom