Tamko la Umoja wa Kizazi cha Kuhoji(UTG) kuhusu hali ya usalama nchini na kupotea kwa Ben Saanane

Ukweli ni kwamba wenye mitandao wameshapewa onyo dhidi ya mawasiliano ya Ben Saanane. Namba zake zitakuwa in black list. Maafisa usalama wanakumbuka gazeti la mwanahalisi lilivyowaanika kwenye sakata la Ulimboka. Na kwa bahati mbaya hao wa mitandao hawako huru. Kumbuka sababu za kubadilishwa badilishwa majina kabla ya kustukiwa.

Na boss alishatoa tahadhari tena kwa ukali kuwa hawako huru that much. Hivyo kunawakati inabidi waugulie rohoni, wakifungua midomo watajikuta wanahamisha virago.
Issue ya Ben Kubenea anaijua vizuri acheni kuhangaika. Gazeti hilohulo la Mwanahalisi kimewahi kuandika Ben ameonekana kwenye vijiwe vya kahawa
 
UTG ndio nini, inajihusisha na nini....Mmesajiliwa wapi.?

Isije kuwa ni kikundi kipya cha utekaji.!
 
1. UTG inatilia shaka ukweli wa taarifa ya mawasiliano ya mwisho ya Ben. Mawasiliano yaliyowasilishwa jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao (Cyber crime) ambayo tumeweza kuyaona, yanaonesha kuwa Ben aliwasiliana mara ya mwisho kupitia simu yake mnamo 16/11/2016 saa 2:01 asubuhi.

Lkn Ben aliondoka nyumbani kwake tar 18/11/2016. Hii inamaanisha Ben hakuwasiliana kbs tar 17 na 18 jambo ambalo UTG tunaamini si kweli. Kama Ben aliondoka nyumbani kwake 18/11/2016 iweje mawasiliano yake ya mwisho yawe 16/11/2016? UTG tunaamini mawasiliano ya Ben ya siku mbili za mwisho (tar 17 na 18) yamefichwa kwa sababu maalumu.

2. Katika mawasiliano yanayoishia tar 16/11/2016, zipo namba ambazo tunazitilia mashaka, ambazo si za ndugu, marafiki wake wala jamaa wa Ben. Namba hizo zinaonesha kuwasiliana na Ben siku za mwishomwisho kabla ya kupotea na hazijawahi kuwasiliana nae kbs ktk kipindi cha awali.

UTG kwa kushirikiana na familia ya Ben, tumelitaka Jeshi la Polisi kufuatilia namba hizo ili kuwabaini wahusika na wahojiwe juu ya mawasiliano yao na Ben. Lkn hadi sasa hatujapata taarifa rasmi kutoka polisi kuhusu kukamatwa kwa watu hao.

3. Tangu Ben amepotea hadi sasa tumefanya mawasiliano na jeshi la polisi mara 21. Mara zote hizo Polisi wamekua wakituambia kuwa wanaendelea na uchunguzi. Lkn hawajapata kusema wamefikia wapi katika uchunguzi wao huo.
Tunaheshimu utaratibu wa jeshi la polisi kufanya uchunguzi lakini tunaomba watujulishe hatua waliyofikia. Majibu ya mkato kwamba wanaendelea na uchunguzi hayaridhishi hasa kutokana na suala hili kugubikwa na sintofahamu kubwa.

4. Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Ernest Mangu akihojiwa na gazeti la RaiaMwema la wiki hii alisema Ben anatafutwa kama "missing person" yani kama ambavyo watu wengine walioripotiwa kupotea wanavyotafutwa.

Tunamshukuru IGP kwa kukiri kufahamu suala la Ben. Lkn kutokana na suala hili lilivyo tunaamini si sahihi kumtafuta kama missing person.Ben hakuwa mtoto, wala mgonjwa wa akili, iweje atafutwe kama missing person? Ben amewahi kutoa taarifa Polisi juu ya kupigiwa simu na sms za vitisho. Mtu wa aina hii hawezi kutafutwa kama missing person.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
Tunaomba Kilefu cha UTG tafadhali
 
Prove him wrong!!! Acha unaongea kwa hisia!/ UTG wako very technical!
Yupo wrong kutaka kumlazimisha mtu atumie namba anayoijua yeye.hata wewe ukiamua unaweza kutmuia simu na namba amabayo anaijua mkeo tu,ukazima inayojulikana watu wakaanza kudai umetekwa
 
1. UTG inatilia shaka ukweli wa taarifa ya mawasiliano ya mwisho ya Ben. Mawasiliano yaliyowasilishwa jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao (Cyber crime) ambayo tumeweza kuyaona, yanaonesha kuwa Ben aliwasiliana mara ya mwisho kupitia simu yake mnamo 16/11/2016 saa 2:01 asubuhi.

Lkn Ben aliondoka nyumbani kwake tar 18/11/2016. Hii inamaanisha Ben hakuwasiliana kbs tar 17 na 18 jambo ambalo UTG tunaamini si kweli. Kama Ben aliondoka nyumbani kwake 18/11/2016 iweje mawasiliano yake ya mwisho yawe 16/11/2016? UTG tunaamini mawasiliano ya Ben ya siku mbili za mwisho (tar 17 na 18) yamefichwa kwa sababu maalumu.

2. Katika mawasiliano yanayoishia tar 16/11/2016, zipo namba ambazo tunazitilia mashaka, ambazo si za ndugu, marafiki wake wala jamaa wa Ben. Namba hizo zinaonesha kuwasiliana na Ben siku za mwishomwisho kabla ya kupotea na hazijawahi kuwasiliana nae kbs ktk kipindi cha awali.

UTG kwa kushirikiana na familia ya Ben, tumelitaka Jeshi la Polisi kufuatilia namba hizo ili kuwabaini wahusika na wahojiwe juu ya mawasiliano yao na Ben. Lkn hadi sasa hatujapata taarifa rasmi kutoka polisi kuhusu kukamatwa kwa watu hao.

3. Tangu Ben amepotea hadi sasa tumefanya mawasiliano na jeshi la polisi mara 21. Mara zote hizo Polisi wamekua wakituambia kuwa wanaendelea na uchunguzi. Lkn hawajapata kusema wamefikia wapi katika uchunguzi wao huo.
Tunaheshimu utaratibu wa jeshi la polisi kufanya uchunguzi lakini tunaomba watujulishe hatua waliyofikia. Majibu ya mkato kwamba wanaendelea na uchunguzi hayaridhishi hasa kutokana na suala hili kugubikwa na sintofahamu kubwa.

4. Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Ernest Mangu akihojiwa na gazeti la RaiaMwema la wiki hii alisema Ben anatafutwa kama "missing person" yani kama ambavyo watu wengine walioripotiwa kupotea wanavyotafutwa.

Tunamshukuru IGP kwa kukiri kufahamu suala la Ben. Lkn kutokana na suala hili lilivyo tunaamini si sahihi kumtafuta kama missing person.Ben hakuwa mtoto, wala mgonjwa wa akili, iweje atafutwe kama missing person? Ben amewahi kutoa taarifa Polisi juu ya kupigiwa simu na sms za vitisho. Mtu wa aina hii hawezi kutafutwa kama missing person.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
Polisi wa upelelezi (CID) wanategemea sana taarifa na ushirikiano toka kwa wananchi. Si jambo rahisi namna hiyo kwamba ku trace mawasiliano ya simu ukategemea kumnasa mhalifu. Nchi zilizoendelea wameweka hadi CCTVs kila maeneo na wana setilites lakini bado ni ngumu kunasa wahalifu hawa. Teknolojia inasaidia kiasi kidogo tu katika forensic investigations hasa kwenye nchi zetu hizi za kimaskini ambazo hata teknolojia bado duni sana. Isitoshe hata wataalamu waliobobea kwenye taaluma hii ya forensic ni haba hapa kwetu.

Kwa hiyo the main tool ya forensic investigation duniani kote bado na itaendelea kuwa ni taarifa toka kwa wananchi.

Inasikitisha sana na kushangaza kwamba kijana Ben alipotea mchana kweupe bila kuacha trace yo yote hasa kwa watu wake wa karibu. Tena alipotea siku za kazi maana tarehe 18/11/2016 ilikuwa siku ya ijumaa. Na alipotea peke yake, na mahali pa mwisho alipoonekana kabla ya kupotea hiyo ijumaa haijulikani. Katika mazingira ya namna hii usitegemee CIDs wetu ambao wengi wao hawana hata digrii moja ya forensic ikawa rahisi kujua kilichompata Ben. Kwanza hata kujua tu kama ni suicide or homicide or accident inakuwa ngumu achilia hilo la abduction.

Hivyo ni vyema tukawasaidia polisi kupata taarifa sahihi na za ukweli katika uchunguzi huu. Sina uhakika kama sheria inaruhusu kufanya independent investigation. Kama inaruhusu basi mleta thread hii ajitolee kufanya upelelezi huo. Kulalamika tu haitusaidii sana bali kutukurudisha tu kwenye machungu ya kupotelewa na kipenzi chetu.
 
Hivi unaamini mharifu anaweza akatumia namba yake ili kufanya uharifu? Mtu anaweza kusajili namba ya simu kwa jina ambalo si halisi na akaitumia namba hiyo kufanya uharifu, sioni kama mna impact yoyote kwa suala hilo kama mna imani kuwa mharifu anaweza kupatikana kwa njia hiyo zaidi ya kupata umaarufu wa mitandaoni.

Suala bado linashughulikiwa lakini umeshaanza kuandika mitandaoni kinachoendelea, huoni kama unaharibu upelelezi?

Nilishawahi kushauri kuwa suala la kupotea kwa Ben waulizwe watu wa karibu, isingekuwa rahisi kwa Ben kutekwa kwa njia ya kupigiwa simu tena kwa namba ngeni! Naamini hivi kwa sababu Ben alikuwa anaishi kwa tahadhari kubwa sana kwa kuwa alishatishiwa awali, hata angekuwa boya kiasi gani huwezi kumpata kwa njia hiyo.

Mlitakiwa kujua kama siku hiyo alikuwa ofisini? Alitoka saa ngapi akiwa na nani? Alikuwa anapendelea kuwa na nani?
 
Siku nyingine kama hujui kitu uliza. Ni aibu kuonesha hadharani namna ulivyo mjinga. Ngoja nikusaidie. Kwenye kufuatilia mawasiliano ya mtu tunaangalia simu (IMEI), namba ya simu (MSISDN), OTHERPARTY, aina ya mawasiliano (CALLTYPE), muda (DURATION), Mnara simu ilipopigwa au sms ilipotumwa (CL_SITE_NAME), mida simu ilipopigwa/piga au sms ilipotumwa/tuma (TIME), Tarehe (DATE), wilaya na mkoa ambako mnara huo upo (C_LDISTRICT/REGION). Hii ina maanisha kwamba hata ukibadili line bado IMEI number itabaki ileile. That means simu itasoma ileile, isipokua itaonesha mabadiliko ya line.!
Bado si rahisi kumpata mharifu aliyejipanga kwa njia hiyo, kwani anaweza akasajili line kwa jina ambalo si halisi, pia akatumia simu mpya, kwani hata wao wanafahamu kuwa wanaweza kutafutwa kwa njia hiyo, kuna kipindi mimi nilishawahi kusajili namba ya simu bila kitambulisho.

Pia ni vema mkawahoji watu wa karibu na Ben kwani isingekuwa rahisi kwa Ben kuingia kwenye mtego rahisi kiasi hicho, yaani apigiwe simu na namba ngeni halafu aingie mkenge ilihali alishatumiwa vitisho na namba ngeni awali, lazima kuna namna nyingine iliyotumika kumteka, inawezekana hata kuna mtu wa karibu alitumika kumrubuni huyo Ben, sidhani hata wewe kwa kipindi hiki unaweza kukamatwa kwa kupigiwa simu na mtu usiyemjua na ukaingia mkenge!
 
Shida kubwa ya nchi hii ni kuwa na wajinga wengi wanaojifanya wajuaji. Mtu anahoji UTG ilikua wapi, wakati andiko linaelezea hatua ambazo UTG imechukua tangu siku ya kwanza iliporipotiwa Ben kapotea. Tangu mwezi November UTG imechukua hatua mbalimbali na wameeleza yote kwenye hiyo taarifa yao. Taarifa pia inaeleza Press conference walizofanya na hatua zilizochukuliwa. UTG pia ndio waliofungua jalada polisi kwa kushirikiana na familia ya Ben kama hatua za awali baada ya Ben kutokuonekana. Lakini mtu mmoja kwa uvivu wa kusoma anaibuka na kuuliza maswali ambayo yote yamejibiwa ndani ya andiko. Ujinga ni kipaji.!
...Mbona UTG ni ya watu wa Kilimanjaro Tu?...
 
Hivi unaamini mharifu anaweza akatumia namba yake ili kufanya uharifu? Mtu anaweza kusajili namba ya simu kwa jina ambalo si halisi na akaitumia namba hiyo kufanya uharifu, sioni kama mna impact yoyote kwa suala hilo kama mna imani kuwa mharifu anaweza kupatikana kwa njia hiyo zaidi ya kupata umaarufu wa mitandaoni.

Suala bado linashughulikiwa lakini umeshaanza kuandika mitandaoni kinachoendelea, huoni kama unaharibu upelelezi?

Nilishawahi kushauri kuwa suala la kupotea kwa Ben waulizwe watu wa karibu, isingekuwa rahisi kwa Ben kutekwa kwa njia ya kupigiwa simu tena kwa namba ngeni! Naamini hivi kwa sababu Ben alikuwa anaishi kwa tahadhari kubwa sana kwa kuwa alishatishiwa awali, hata angekuwa boya kiasi gani huwezi kumpata kwa njia hiyo.

Mlitakiwa kujua kama siku hiyo alikuwa ofisini? Alitoka saa ngapi akiwa na nani? Alikuwa anapendelea kuwa na nani?
Safi sana. Na kuna maswali mengi tu yanayotakiwa kujibiwa, kwa mfano:
1. Kijana Ben alikuwa akiishi peke yake? Kama jibu ni hapana, hao alikuwa anaishi nao wanasema nini? Ni lini hakurudi nyumbani na walichukua hatua gani na lini? Jee aliaga kuwa hatarudi nyumbani au ni kawaida yake kutorudi nyumbani bila taarifa na kadhlika.

2. Hao aliokuwa anafanya nao kazi wanasemaje? Muonekano wake siku za karibu na mwisho wake ulikuwaje? Jee alionekana kuwa na sonona (depressive mood) au msongo wa mawazo (anxiety neurosis) siku chake kabla ya kupotea ( to rule out of possible suicide)? Jee ni nani walikuwa wabaya wake (to establish possible homicide)? Na kadhalika. Mleta mada alete majibu ya masuala haya na mengineyo badala ya kuamini TCRA inauwezo wa kumkamata mharifu kwa kutumia GPS tracking ya simu ya aliyepotea. Mleta mada atumie akili yake badala ya mihemuko ya kisiasa kwenye serious issues kama hizi. Haiingii akilini kuwa TISS ihangaike na mtu mdogo kama kijana huyu ambaye hana impact yo yote kwa usalama wa taifa. Si wangehangaika na bosi wake?
 
je mwisho wa ku post social media ni tarehe 16? au hata baada?

je baada ya tarehe 18 ni kweli kuna posts FB zilijifuta/futwa?na yeye au mwingine?
 
Niliacha kubishana na wewe kwa sababu ya kuogopa kutetea unayotaka siwe. Ila utaelewa nilimaanisha nini!!

Angalia jamaa yako huku anavyodhalilika sasa na maandishi yake.
Simama uhesabiwe (New episode).
Ndio nimesema sio kubenea tu pia bashe na nape wameshawahi ongea haya nje ya bunhe hao wote muwakamate muwahoji kwani nani kakataaa????

Nyie mnajua sana kuwa kuna haja ya kuwahoji sema mnaogopa siri itavuja maana sioni wapi nape alieshiriki operation zote za chama adanganye khusu taasisi yenu hio nyeti!! No way na kwakuwa hamjakanusha wala kumkamata kwa uchochezi wanachi wataendelea kuamini its TISS iliyomteka saanane unless nyie muamue kuact now mlete ushahidu mwzani wa mbowe kumteka otherwise its cheap meaningless propaganda
 
Polisi wa upelelezi (CID) wanategemea sana taarifa na ushirikiano toka kwa wananchi. Si jambo rahisi namna hiyo kwamba ku trace mawasiliano ya simu ukategemea kumnasa mhalifu. Nchi zilizoendelea wameweka hadi CCTVs kila maeneo na wana setilites lakini bado ni ngumu kunasa wahalifu hawa. Teknolojia inasaidia kiasi kidogo tu katika forensic investigations hasa kwenye nchi zetu hizi za kimaskini ambazo hata teknolojia bado duni sana. Isitoshe hata wataalamu waliobobea kwenye taaluma hii ya forensic ni haba hapa kwetu.

Kwa hiyo the main tool ya forensic investigation duniani kote bado na itaendelea kuwa ni taarifa toka kwa wananchi.

Inasikitisha sana na kushangaza kwamba kijana Ben alipotea mchana kweupe bila kuacha trace yo yote hasa kwa watu wake wa karibu. Tena alipotea siku za kazi maana tarehe 18/11/2016 ilikuwa siku ya ijumaa. Na alipotea peke yake, na mahali pa mwisho alipoonekana kabla ya kupotea hiyo ijumaa haijulikani. Katika mazingira ya namna hii usitegemee CIDs wetu ambao wengi wao hawana hata digrii moja ya forensic ikawa rahisi kujua kilichompata Ben. Kwanza hata kujua tu kama ni suicide or homicide or accident inakuwa ngumu achilia hilo la abduction.

Hivyo ni vyema tukawasaidia polisi kupata taarifa sahihi na za ukweli katika uchunguzi huu. Sina uhakika kama sheria inaruhusu kufanya independent investigation. Kama inaruhusu basi mleta thread hii ajitolee kufanya upelelezi huo. Kulalamika tu haitusaidii sana bali kutukurudisha tu kwenye machungu ya kupotelewa na kipenzi chetu.
Sina uhakika kama mihemuko ya kisiasa au ya kitaalam ndiyo inayofanya kazi katika utoaji maoni juu ya hoja hii iliyoko mezani.
Maelezo hayo hapo juu yana mantiki kubwa sana na yanahitaji kupewa umuhimu unaostahili ili angalau kupata mwelekeo.
Aidha, kama tayari Observers kutoka Umoja wa Mataifa wameitwa kuja kufanya upelelezi / uchunguzi, hamna haja ya ku pressurize upelelezi wa ndani ambao tayari umeishatiliwa mashaka.
Pamoja na hayo, Mbowe na Kubenea, wanaweza kuitisha press conference ili angalau na wao wakatoa ufafanuzi kidogo?
 
je mwisho wa ku post social media ni tarehe 16? au hata baada?

je baada ya tarehe 18 ni kweli kuna posts FB zilijifuta/futwa?na yeye au mwingine?
Ujuzi wako wa tekinolojia hii ya ki electronic una mashaka. Unaamini hizo FB na social media zingine zina security ya maana. Watu wanaingia ki electronic hadi kwenye saver za uchaguzi wa Amerika na kubadilisha matokeo ya uchaguzi. Watu wanaingia hadi saver za Yahoo na kudukua emails za Hilary Clinton. Watu wanadukua na kuiba pesa kwenye mabenki, ATM na mitandao mingine ya pesa. Sasa sembuse huto tumitandao twa FB, Instagram, jamii forum nk? Tena hiyo ya kufuta posts kwenye FB na mitandao miingine ya social media ndiyo rahisi kuliko vyote hata wewe na mimi unaweza kufanya, hasa kama simu yake unayo. Kama hujui sitaki kukufundisha maana unaweza kuwafanyia wenzako udukuzi.

Hakuna security ya maana kwenye hiyo mitandao ya social media including humu Jf. Usidhani umejificha nyuma ya keyboard. Wakitaka wanaingia tu kwenye saver ya jf kirahisi (wana i hack) bila hata hao wenye jf kujua, halafu wanakukamata kirahisi. Haizalishi mtandao uwe au usiwe na registration ya dot tz. Na hili ni kwa usalama wa nchi na hivyo kila nchi ina uwezo wa kufanya hivyo, zinapishana tu kiwango cha uwezo huo. Russia na USA ndiyo wanaoongoza, na mpambano (vita) ni mkali. Vita siku hizi ni za kidijitali. Mabomu, ndege, meli na dhana zingine za kivita zinaongozwa ki elekroniki.

Ndiyo maana kila kukicha wataalamu wanatengeneza viruses na vitu vingine vya aina kwa madhumuni haya ku hack mawasiliano ya dijitali. Antivirus na wall defenders mbali mbali zinabidi kutengenezwa kila kukicha kupambana na vita hii ya ki electronic duniani pamoja na backups mbali mbali in the clouds na kwingineko ndani na nje ya dunia yetu. Sasa wewe unayetumia antivirus na wall defenders za bure bure (free of charge) unajiona you are not vulnerable? Ikalagabaho!!!
 
1. Kuwasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi) Tume ya haki za binadamu na utawala bora, ambayo kikatiba ina mamlaka ya kusikiliza mashauri/malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.

Kwa mujibu aa ibara ya 130 na 131 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tume hii ina mamlaka ya kumuita na kumhoji mtu yeyote katika Jamhuri ya Muungano isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar.

Tunaamini kwa mamlaka ambayo tume hii imepewa kikatiba inaweza kuwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini na kuwahoji juu ya matukio ya kuogofya yanayoendelea nchini ya watu kupotea na wengine kuripotiwa kuteswa au miili yao kuokotwa wakiwa wamekufa.

2. UTG imewasilisha maombi rasmi kwa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora imuagize Mkemia mkuu wa serikali (kwa kushirikisna na mamlaka zingine) wafukue miili ya watu 7 waliyoizika kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo ili ifanyiwe vipimo vya vinasaba (DNA test). Hii itasaidia watanzania waliopoteza ndugu zao kupata fursa ya kwenda kuoanishwa vinasaba hivyo kubaini kama ndugu zao waliopotea ni miongoni mwa watu hao 7 waliozikwa kienyeji wilayani Bagamoyo.

Tunaamini hata kama miili ya watu hao imeharibika ardhini, bado vipimo vya DNA vinaweza kufanyika kwa kupitia mifupa yao, kwa sababu hata Faru John alipimwa DNA kupitia mifupa yake. Kitendo cha serikali kutumia mamilioni ya fedha kupima DNA yafaru John huku ikipuuza kupima DNA kwa miili ya binadamu wenzetu iliyookotwa, hakileti tafsiri nzuri kwa wananchi. Wengi wanaona kuwa serikali inathamini zaidi uhai wa wanyama kuliko watu.

3. Taasisi ya UTG imekiomba kituo cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC) kupeleka malalamiko rasmi Umoja wa mataifa (UN) juu ya matikio ya watanzania kupotea. Mapema mwezi uliopita Mkurugenzi wa kituo hicho Dr.Hellen Kijo Bisimba alishiriki mkutano wa umoja wa mataifa wa taasisi za kiraia zinazoshughulika na masuala haki za binadamu ambapo aliweza kupenyeza hoja kuhusu watanzania kupotea katika mazingira ya kutatanisha akihusisha suala la Ben Saanane.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo Umoja wa mataifa ulimtaka Dr.Kijo kuwasilisha kwa maandishi malalamimo hayo ili Umoja wa mataifa uweze kutuma wataalamu wake kuja kuchunguza. Ieleweke kwamba Umoja wa mataifa una chombo huru cha uchunguzi kiitwacho "The Observer" na kina uwezo wa kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi yoyote mwanachama (Tanzania ikiwemo).

Hivyo basi UTG tulishirikiana na LHRC kuhakikisha kuwa barua hiyo inaandikwa na kufika Umoja wa mataifa katika utaratibu rasmi ili waweze kutuma wataalamu wake kuja kuchunguza. Tayari barua hiyo imeshaandikwa na tunasubiri majibu.!
 
Back
Top Bottom