Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
Kikojozi
Naona ni WaTanzania tu kama wewe ulivyokuwa umetokea misitu ya Congo kusaka ngedere katika misitu ya SukumaLand na kuachwa huku na leo umekuwa Mtanzania ,dogo kasome historia yako ili ujijue asili yako nawe ni ya wapi wale ndio ushawabagua kuwa ni wahindi sasa wewe ?
 
Nakubali kuwa RA na kundi lake limetajwa sana kuhusika na vitendo vya kifisadi lakini jukumu la kuthibitisha hayo lipo mikono mwa polisi na si vinginevyo....
Na kama polisi hawachui hatua wanazopaswa kuchukua tufanye nini?
 
kwa nini huyu bwana ni muoga sana kuongea hadharani? si bungeni au mbele ya waandishi wa habari....aliongea mara moja tu ile ya mtikila kwa vile alikuwa na ushahidi!!!!!

DHAMBI INAMUHUKUMU .........
 
How can Rostam run away from this? I need to know, how in the world huyu jamaa anakuwa na mikwara mingi?

from that letter i can say this, Rostam hajaandika bali ni mwanasheria wake sababu ya uchaguzi wa meneno unaonyesha. On top of that Rostam is empty head.

Jamani naomba niwe racist for a second, How is possible MUIRAN akacontrol maisha ya watu million 40? I just think Rostam doesn't care about Tanzania sababu He don't know nothing about Tanzania. Does Rostam know the struggle of majority of Tanzanian? Does he know the pain that watanzania wanapitia sababu ya mtandao wake. God help us, i lay my case mbele ya Mungu.... It seems no one can either defeat this guy.... Tanzania we have problem.

yOU CUD HAVE ASKED YOURSELF THE opposite; how so stupid are the "black presidents (meaning the the Tanzanian President" to be controlled by one man like Rostam; instead of taking care of his own people, the 40 plus million Tanzania (and instead collaborating to steal from the treasury with Tanzanians of Asian decent). It doesn't click in my brain how our leadrers can be used by these creatures like prostitutes! The prostitutes of very low value; who can take way their underwears by a glass of wine; (like one of our ministers who is speaking now). I am ashamed of my own country; these are worse than pigs and dogs!!
 
Excellent mr. Rostam, mengi hawezi kuifanya tanzania kama haina sheria bwana hata kama tuhuma zake zina uzito kiasi gani kwani hajui pa kuzifikisha mpaka abwatuke, kama kamwaga mboga na ww (ra) mwaga ugali.
Tutaona mengi mwaka huu.

Mengi anabwatuka kwenye vyombo vyake vya habari. Sisi tunabwatuka hapa JF. Anayemaindi aende mahakamani.
 
Ushauri wa kijinga.

Mengi usipeleke ushahidi wowote wala usiombe mtu radhi.
Napenda kuona Rostam Azizi akiita waandishi wa habari ili kufichua maovu yako.

Naona kama RA anajitahidi kumblackmail Mengi ili amwangukie vile?

Hiiiii Hiiiii Hiiii!

Wapiganapo Fahari wawili....
 
Let me make one thing clear here, am not in support of RA, Manji or Mengi. To me they all bunch of nuisance old businessmen who are driving this nation to its grave.

The biggest fool is The Executive Chairman of IPP Media, and Chairman of Media Owner Association of Tanzania plus holder of many other top position in bussness related associations, Mr powermonger, Reginald Mengi.

Inawezakana vipi akurupuke kuita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja na kuwatuhumu wenzake kwa kile anachodai ufisadi papa? Anataka kutuambia nini watanzania, mahakama zetu na vyombo vya dola vimeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo, je yeye nani katika nchi hii hadi ifike wakati aende kifua mbele kuwatuhumu watu atakavyo.

Nakubali kuwa RA na kundi lake limetajwa sana kuhusika na vitendo vya kifisadi lakini jukumu la kuthibitisha hayo lipo mikono mwa polisi na si vinginevyo....mbona hatujamuona huyu mzee mnafiki kwenda kupiga kura kwenye ile kampeni yetu ya kuwataja watu wanaohusika na vifo vya maalbino na wahalifu wakubwa wakiwemo mafisadi. Ni kweli Bwana Mengi anauchungu na nchi hii? Kwanini hakupeleka ushahidi wake polisi na kisha kuja kututangazia umma kuwa yeye ameshalabidhi ushahidi na yuko tayari kuwa shahidi namba moja katika kesi dhidi ya watu hao?

Kusema kweli tabia ya mengi inakera sana hasa kwa nchi ambayo inafuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria kama Tanzania. Kwahiyo baada ya kuwataja alikuwa anatarajia nini kiendelee, au angejisikiaje kama sisi wananchi tungejichukulia sheria mkono kama ilivyokuwa kwa bwana Balali ambapo wananchi waliamua kujigawia mashamba yake kwa hasira. Mi simuelewi huyu mzee hata kidogo....kama ni ushindani kibiashara angetafuta njia nyingine si staili hii ya kuchonganisha wenzake. Hali hii inafanya niamini kuwa Mengi ameanzisha kikundi chake cha Kimafya ili kuspy wanayofanya wenzake...where else he would have gotten all these information and this guts to stand up in public and declare oother guilt without being prosecuted in court of law.

Najua wapo watu humu ndai wanajenga mapenzi kwa mtu yeyote anaelekea kuwasakama watuhumiwa hawa wa ufisadi, na hali hii inawezakana kuwapofusha hata warevu wachache kuona ukweli wa mambo. Kama mnapenda kusikia RA na wenzake wanakwenda mahakamani iweje msitoe hamasa hiyo hiyo kwa Bwana Mengi kwenda mahakamani au ndo ule usemi wa kiswahili usemao "Nani atamfunga paka kengele?". Let's not rejoice for anyone who break the law under the name of saving the nation unless we are all agree that our Jurisdictions can not be trusted and only then let take matter on our own hand as per Mr. Mengi point of view. Period
Kama huna la kusema si lazima uandike. Mengi ame-practice uhuru wake; he selected to speak on this issue; and this was his prioritity(maybe); how can you select his priorities? wewe kula dona ulale!
 
Kikojozi
Naona ni WaTanzania tu kama wewe ulivyokuwa umetokea misitu ya Congo kusaka ngedere katika misitu ya SukumaLand na kuachwa huku na leo umekuwa Mtanzania ,dogo kasome historia yako ili ujijue asili yako nawe ni ya wapi wale ndio ushawabagua kuwa ni wahindi sasa wewe ?

Ok, let me rephrase the question.

Unataka tuwatetemekee mabwana wako 'Watanzania wenye asili ya kiasia' ndani ya nchi yetu?
 
nafikiri RA anapaswa kuzungumzia mambo yote yanayozungumzwa juu yake na sio moja tu la Ndg Mengi. Kwa mfano ni kwanini anuani zake zintumika na makampuni yaliyoliibia taifa. Pili, azungumzie pia kiapo cha wakili aliyemtaja kuwa ndiye aliyesuka dili la EPA n.k

Hapo tutamuelewa. Ahsante san Ndg Mengi kwa kuwatoa nyoka pangoni. Sasa ni kutafuta vichwa vyao kuvigonga tu.

hata akisema nini ukweli utabaki pale pale kuwa alikuja kutoka kwao maskini wa kuitupa na fedha zote amezifisadi hapa hapa bongo!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kumbukeni tu anaewahi mahakamani na kushitaki ndie anaepata baraka za mahakama ,chochote kile atakachowasilisha Mengi kama utetezi hakitafaa kitu kwa maana shitaka lenyewe halitahusiana na ufisadi kabisa ,litajitenge na Mengi atafunguliwa shitaka lingine kabisa ambalo litamtaka aonyeshe ni wapi alipata madaraka ya kuwataja mafisadi,uchunguzi gani aliufanya,ni kwa nini aliwataja wahindi watupu hapo ataingia katika ubaguzi na kama haitoshi ameingilia mahakama ambalo hilo peke yake ni kosa huku ndio mwisho wa kuchamba kwingi. WaVhadema mteja huyo mwambieni ajiunge na chama cheni haraka ili mpate kumkwamua la si hivyo wahindi watamlaza jela kama mnavyojua jamaa ndio wanaoendesha serikali. au sivyo ?

Fair point.
Inamaana leo hii nikija kumwuiba yule ng'ombe wako uliye mfunga kule malishoni na ukanione na pepea na ng'ombe wako ,kwa mtanzamo wako wewe itakubidi utafute organ husika ikupe mamlaka ya kuniita mwizi wa ng'ombe wako ?????????????

Na ukmenikamata na ng'ombe wako hivyo huruhusiwi kuniita mwizi kwa sababu huna mamlaka hayo maana vinginevyo nitakushitaki????????????

hakuna chombo kinachotoa ruhusa hiyo ila ni ushaidi ulionao ndio utabainisha.
Mengi kama mtanzania kaibiwa pesa zake na wezi wake anawafahamu kwa sababu anaushaidi wa kutosha hivyo mwacheni atatoa ushaidi gani jinsi fisadi papa lilivyopapua fedha.

Kama hana huo ushaidi ama hakumuona mwizi akikwapuwa ng'ombe hiyo basi itakuwa stori nyingine.
 
Last edited:
Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009. Wakati tunamsubiri nakala yake tupate dondoo hii kutoka kwenye hitimisho la tamko hilo:

"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"

Wakati huo huo gazeti hilo linaripoti kuwa mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji, yeye ameshachukua hatua ya kufungua kesi dhidi ya Reginald Mengi ambapo anadai fidia. Maswali ya msingi ya kujiuliza ni : Je, katika mpambano huu ile methali ya "wapiganapo tembo nyasi huumia" itatimia au nyasi ndio zitapata fursa ya kustawi zaidi? Je, mpambano huu utaishia kuwa mchezo wa kuigiza au utazitimizia hizo nyasi methali ya "avumaye baharini papa kumbe wengi wapo"?

TAMKO LAKE HILI HAPA:

i372_Rostam.jpg


When you cast a stone at a pack of DOGS, the one that howls is the one that got hit. Rostam Aziz your day of reckoning is approaching...
 
Pinda aliposema wauwaji wa albino na wao wauliwe, tulisema hakuwa sahihi kwa kauli yake, haikuwa na maana kuwa tulikuwa tukiunga mkono mauwaji ya albino, kilichokuwapo ni kuwa zipo hatua ambazo tumejiwekea na kkubaliana kuzifuata katika kushungulikia matatizo hayo, na kwa hili la Mengi kama kweli alifahamu kuwa hawa ndo mafisadi na ushahidi anao kwanini asifuate taratibu zinazoeleweka na yeye Mengi anazifahamu, hawa watu wakashughulikiwa kwa njia hizo badala ya kubwatuka na kuw "sensitize" Watz (ambao tokea hapo weshadata kwa ugumu wa maisha), wakajenga chuki za bure?
Hoja ni kwanini asifate sheria, wakati hakuzuiliwa kufanya hivyo na mtu yeyote, hata hao aliowaita mafisad papa.
sasa hatari yake ndo hii, heshima yake Mengi, imepotea, anaonekana ovyo tu kama aliyechanganyikiwa na nini sijuwi.
Kama alitafuta ziada ya umashuhuri, angetumia staili ile ile ya Mtikila, Mtikila anajuwa pahala pa kutafuta ugomvi na watu.
 
Jana asubui nilifanikiwa kuona interview TBC1 ya Waziri Sophia Simba kuhusu sakata la Mengi na wale aliowaita mafisadi papa. Mambo aliongelea kama waziri ndio msimamo wa serikali. Binafsi naona msimamo huo wa serikali una kasoro.

1) Kama serikali ilitaka kutoa tamko ingemtafuta waziri ambaye ni "eloquent" wa kuweza kuzungumzia swala nyeti kama hili la ufisadi. With due respect kwa Mheshimiwa Simba alijigonga gonga kuhusu maswali aliyokuwa anaulizwa. Majibu yake hayakuwa "factual" enough na hivyo kuoneka anapwaya! Kwa mfano mdogo, Marin Hassan alimuuliza dhana ya kutengenisha baishara na siasa na yeye akajibu kwamba katika wale watuhumiwa watano hakuna mwana siasa hata mmoja! Duinia nzima inajua kwamba Mhe. Rostam Aziz ni mbunge wa Igunga na mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na alikuwa Mweka Hazina wa CCM. Juzi Mama Simba amenukuliwa kwenye gazeti akisema kwamba Kamati ya Maadili ya Viongozi haipaswi kujishugulisha pesa za viongozi zilizoko nje ya nchi! My foot!! Maoni yangu ni kwamba serikali ikiachia watu kama waziri Simba kuelezea msimamo wake katika mambo nyeti kama hili tunaweza tukaishia kama swala la Zitto Kabwe na Buzwagi. That issue was mishandled by the government at a high political cost.

2) Historia inatukumbusha kwamba mwaka juzi wakati swala la EPA lilipoibuka kwenye mtandao na Dr. Slaa kulileta Bungeni, Waziri Meghji (akiwa waziri-Fedha) na Spika walimbeza (skepticism) wakisema hakuna ushaidi na hayo ni mambo ya mitandao. Waingereza wanasema " It came to pass". Leo hii kesi za EPA zinanguruma mahakamani na waziri Meghji sio waziri tena!

3) Katika nchi yetu sio mara ya kwanza kutaja wazi wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi. Septemba 2007 Dr. Slaa na wenzake walitaja majina kumi ya watuhumiwa wa ufisadi pale MwembeYanga, Temeke. Baadhi yao walicharuka na kutishia kwenda mahakamani kwa kuchafuliwa na wengine wakasema hakuna ushaidi. Mpaka leo hakuna hata kesi moja ilifunguliwa mahakamani kwa "uzushi" huu! Leo hii Mhe. Lowassa, Karamagi na Chenge wako nje ya Baraza la Mawaziri kwa tuhuma kama walizosema kina Dr, Slaa. Mhe, Mramba, Yona na Mgonja wako mahakamani kwa tuhuma kama hizo. Rais mstaaafu Ben Mkapa halali usingiz mzurii kwa kutuhumiwa na umma kwa kutumia madaraka vibaya. Kinachoshangaza wakati wote huu sijaona serikali ikitoa msimamo wake mkali (kama Mama Simba) kuhusu watuhumiwa wa Dr. Slaa. Kulikoni sasa waziri anakuja mbogo kwa kutajwa mafisadi watano tu? Labda kwa kuwa limeongezeka neno " papa"? Mbona serikali haijatoa tamko kuhusu kutuhumiwa Rais mstaafu?

4) Mhe. Rostam Aziz amekuwa akitajwa tajwa katika haya mambo ya ovyo. It is not by coincedence, I believe. Alitajwa Mwenbeyanga, anatajwa katika wizi wa EPA, alitajwa na Tume ya Mwakyembe kuhusu Richmond na Dowans na sasa anatuhumiwa na Mengi kuwa ni fisadi "papa" . Huyu ni sawa na "Yuda Iscariot" kwa kuisaliti CCM hapaswi kula meza moja na viongozi wetu labda kama nao ni "birds of the same feathers"? Kwa nini asitolewe kamati kuu CCM hadi hatakapojitakasa? Bila hivyo maswali yataulizwa tu. Wakubwa wapende wasipende.

5) Tanil Somaiya amefadhili uchaguzi wa juzi wa UV-CCM kwa "mchango" wa shs. 400 milioni. Je waziri Simba hakuona kwamba kwa utetezi wake kwa hawa watuhumiwa kunaweza kukatafusiriwa kwamba serikali ya CCM inalipa fadhila? Je wananchi wakisema CCM imetekwa na matajiri kuna wakubisha?

6) Mama Simba anasema Mengi kama ana ushahidi aupeleke kwenye vyombo husika hususan TAKUKURU. Tunauliza TAKUKURU ipi? Hii inayoongozwa na Hosea? Kuna azimio la Bunge kuhusu kiongozi huyu kwa kuboronga uchunguzi wa ufisadi Richmond. Mengi kama mtu mwelevu hawezi kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere. Na hata wananchi hawana imani na Polisi katika mambo haya. Kama imani ingekuwepo serikali hii isengeitisha kura za maoni kutafuta wauaji wa Maalbino. Watu wangewataja watuhumiwa kwa jeshi la polisi na Polisi wangeisha maliza tatizo hili. Iko wapi ile orodha ya wauza unga aliyotuaaidi Mhe. Mwapachu akiwa waziri wa Usalama wa Taifa?

7) Sio mara ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho kwa Mengi kuzozana hadharani na wafanya biashara wenzake. Walikwaruzana na Yusuf Manji mpaka wakafikishana mahakamani. Mengi alizozana na Rostam kuhusu Rostam kuzindua album katika kanisa moja la Kiluteri mpaka (tunaambiwa) mchungaji akachukuliwa hatua. Hakuna jipya na sisi hatuoni kwa nini serikali inaigilia mzozo huu. Kuna sheria zinazohusu kafsha na kama waliotajwa na Mengi wanafikiri wameonewa Mengi kwa kauli yake atafurahi kukutana nao. Manji ameshatinga mahakani ni Rostam aende huko. Why is the minister poking her nose in the affairs that do not concern her? Ana kihele hele. Kwa hili yeye ndie KACHEMSHA na aambiwe hivyo.

8) Swala la Ubaguzi wa rangi halina mashiko. Hatuwezi kuogopa kutajana na kusutana eti tutaambiwa ni wabaguzi. Kama Wahaya kumi ni wezi wa mali ya Umma nawatajwe. Mbona wachaga wanasemwa kwa kujazana TRA kwa misingi ya Ukabila na hawajalalama? Lipumba na wenzake walikuwa wapi wakati Salum Mohamed Salum akibaguliwa wazi wazi wakati wa mchakato wa Urais ndani ya CCM 2005 na hakuna aliyenyosha kidole? Rostam should not hide behind racism veil to justify his misdeeds.

Nimalizie kwa kutoa mfano wa Biblia. Yesu alipowasema sana mafarisayo, mazudakayo na wakuu wa dini ya kiyahudi walipanga njama ya kumuua. Na katika kuhalilisha kifo chake Kuhani Mkuu wa wakati ule jina lake Keyafa aliwashauri kwamba " inabidi mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi". Baadhi ya magazeti yamesema Mengi kwa kufanya alichofanya anajitoa mhanga. Inawezekana lile neno likatimia. Hatuwezi kuendelea na uoza huu katika nchi yetu. Tanzania bila Ufisadi inawezekana.

Kula 5,ukweli mtupu no bias no spin,ni kweli Mengi kajitoa muhanga.
 
Pinda aliposema wauwaji wa albino na wao wauliwe, tulisema hakuwa sahihi kwa kauli yake, haikuwa na maana kuwa tulikuwa tukiunga mkono mauwaji ya albino, kilichokuwapo ni kuwa zipo hatua ambazo tumejiwekea na kkubaliana kuzifuata katika kushungulikia matatizo hayo, na kwa hili la Mengi kama kweli alifahamu kuwa hawa ndo mafisadi na ushahidi anao kwanini asifuate taratibu zinazoeleweka na yeye Mengi anazifahamu, hawa watu wakashughulikiwa kwa njia hizo badala ya kubwatuka na kuw "sensitize" Watz (ambao tokea hapo weshadata kwa ugumu wa maisha), wakajenga chuki za bure?
Hoja ni kwanini asifate sheria, wakati hakuzuiliwa kufanya hivyo na mtu yeyote, hata hao aliowaita mafisad papa.
sasa hatari yake ndo hii, heshima yake Mengi, imepotea, anaonekana ovyo tu kama aliyechanganyikiwa na nini sijuwi.
Kama alitafuta ziada ya umashuhuri, angetumia staili ile ile ya Mtikila, Mtikila anajuwa pahala pa kutafuta ugomvi na watu.

Mkuu mbona unatoka nje ya mada? Kwani 48 hrs zimeshapita ama unaongelea kitu gani?
Sasa unapomwambia Mengi atumie style ya Mtikila ili ajipatie umashuhuru si ndiyo unaonyesha upunguwani kabisa ama kutofahamu Tanzania? Mkuu wewe ni Mtanzania wa wapi?
Halafu unamfahamu Somaiya wewe? Inawezekana unamfahamu maana unaonekana wewe ni mtanzania wa ajabu ajabu tu,mimi kama mtanzania wa kawaida siwezi kumwona Mengi na kumfananisha na Mtikila eti kujitafutia umashuhuri,ndio maana nakubali Mengi kajitolea muhanga,maana imagine kuna watu wanafikiri kama wewe,kutakosekana machafuko kweli?
 
Inakuwaje hii nchi inakuwa na viongozi wanaojua kuwa kuna mtu ana maouvu lakini hawasemi au kuwafikisha waovu hao mbele ya sheria? Statement kama hii inatosha kabisa kumwondoa mtu katika uongozi. Hafai kuwa kiongozi wa Watanzania.

Kama anajua maovu ya Mengi, angelikuwa mstari wa mbele kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria yashughulikiwe na siyo asubirie maovu yake yatajwe ndiyo naye aseme "mbona huyu naye ana maovu."

Hadi Amir Jeshi Mkuu naye ana style hii hii ya kuwa na orodha za wauza unga na watoa rushwa.... Kama wanajua maovu kwanini wasiyapeleke kwenye vyombo vya sheria mara moja? Wanasubiria aina gani ya mabaya yatokee ndiyo hayo maovu tuyajue?

What a bunch of disgraced leaders! Shame.

Amiri Jeshi anayo pia list mijizi ya bandarini...What a disgrace. Theseso called leaders have turned our once proud nation into a banana republic.
 
Swadakta, nimekupata ndugu, ila kuna umuhimu pia wa kukubaliana na ku-acknowledge uwepo wa entity mbali mbali katika hili sakata zima. Mfano mmojawapo ulio uongelea ni hii ya media. Nakubaliana na yale unayoyasema katika mambo ya maadili ya vyombo vya habari.

Kuna entity nyinginezo, kama vile raia wanaopata kuwa na viongozi watenda haki na wanao tekeleza majukumu yao. Kuna entity ya viongozi, kuna ile ya blogsphere (tuliyomo sisi), kuna entity ya sheria na mahakama, pia kuna entity ya Taifa na image yake, bila kusahau entity ya watuhumiwa.

Zote hizi entities zinahusika kwa namna moja au nyingine katika hili swala. Kuna kutofautiana, kuna sehemu za kukubaliana. Je, yapi ni muhimu na yapi siyo? Does the end justify the means or vice versa sisi kama Taifa?
Pia tusisahau kua RA kwa kiburi anachpatiwa na watawala alidiriki hata kukataa summons za kamatyi ya Bunge ambalo yeye pia ni mbunge. Jamani hawa mapapa dawa yao ndio hiyo tuu. Na utaratibu alionzisha Mengi ndio swadakta wa kutajana coz this country kuna "Conspiracy of Silence" hata katika mitaa yetu hicho kitu kipo. Kama unaona umeonewa chukua sheria mbona sisi hatuajitwa mapapa wa ufisadi msisahau lisemwalo lipo!!!!
 
Viongozi si ndio mafisadi hao hao. Sasa kweli mnategemea mafisadi watajifungulia mashtaka? Halafu mbona anaandamwa Rostam tu? Mkapa je? Au yeye leo hii sio fisadi?
 
hapo sikubaliana na wewe kabisa hatua za kisheria zimeshachukuliwa muda mrefu uliopita lakini vyombo vyertu vya uchunguzi vinaonekana kuwaogopa hawa mapap wa ufisadi. Mara ngapi zimetolewa rai za kukamilisha uchunguzi wa KAGODA, upo ushahid mpaka wa affidaviti ya mwanasheria kumhusu RA kuchota fedha za EPA.

Kwakuwa viongozi wetu wansukumwa na donors anachofanya mengi ni kuwa alert donors kuwa lipo tatizo la mapap wa ufisadi na Iam sure kuwa baada ya muda kidogo domors wakiagiza hatua zitachukuliwa tuu. Bravo Mengi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom