Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
Anasema yeye na familia yake wameajiri watanzania takribani 6,000 na wanawalipa vizuri na hawalalamiki na TRA wanaweza kuthibitisha.

Anasema Mengi kumtuhumu kuwa ana akaunti nje ya nchi ni uwongo kwani hata yeye Mengi ana akaunti nje ya nchi.

Anasema Mengi anadai wao wameanzisha magazeti yenye dhamira ya kumchafua lakini naye vilevile ameanzisha magazeti kama hayo, yeye amepata wapi fedha za kufanya hivyo?
 
Hawa jamaa wanatusaidia sana! Kamata wote wakajieleze mahakamani. Kumbe kweli yote ni mijizi..........

You are dead wrong. Usiwe mwepesi wa kulishwa uwongo. Subiri atoe data kama za Kagoda ndiyo tumuweke Mengi group hili la wahujumu Uchumi.

Hapo bado ni kujifuta vumbi usoni kwa mikono yanye majivu, hajasafishika mtu hapo
 
Kama RA hana mpya zaidi ya hayo tunayoyajua,akaribishe maswali kwa wajumbe
 
Anasema Mengi aliongea na watu akiwa kwenye ndege akawambia Jumatano inayofuata atammaliza Rostam, na alipompigia simu Mengi alikanusha.

Anasema habari nyingi za kumchafua zimekuwa zikiandaliwa na Mengi. Anasema yeye huwa anakana kuhusika na anasema Mwanahalisi walitumiwa na Mengi kumchafua. Waandishi wakacheka. Anasema anajua atalalamika sana kuwa anaonewa lakini ukweli ndio huo kwani tabia na mwenendo wake vinaonekana kumdhihirisha.
 
Waungwana,si tukae kimya wakati hizi live reports zinawasili?Tutapata nafasi ya kuchambua baada ya Invisible kutueleza kwamba press conference imekwisha.
 
Wakuu hajaruhusu maswali... Akiruhusu nitawambia!

Anasema Reginald Abdallah Mengi ndiye kinara wa ufisadi Tanzania
 
Mengi anawapa hela walemavu yeye anawapa nani hela, vibaraka wake?

walemavu wangapi?

Unajua jinsi wafanyakazi wa IPP group of companies wanavyosota na mshahara mdogo na overload ya kazi? Unajua kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi kwenye haya makampuni?

Je unajua bidhaa zinazotengenezwa na haya makampuni ziko chini ya kiwango?
 
Anasema kwa kifupi huo ndio ufisadi wa Bwana Mengi na ushahidi ataupeleka kwenye vyombo husika.
 
Rostam anazidi kuudhi umma wa watanzania, itachukua karne kuwaelezea watanzania kuwa yeye ni msafi kuliko Mengi..sie wakristu tuansema.."vitaumbwa upyana nchi itageuka"...he is real FISADI PAPA.

Sory wana JF, hivi ni press conference ya kumwelezea historia ya Mengi au ni conference ya kujibu tuhuma husika...huyu milele hana hoja, cha msingi ni kumwomba asubiri siku Mengi akifa apewe nafasi ya kusoma risala ya Marehemu labda ndio atakuwa wa kwanza kuushauri ulimwengu kuwa marehemu alikuwa mtu mbaya saaaanaa..kwani tumezoea kila anayekufa huwa anasifiwa.

Hamumuoni hata jinsi alivyo/.....nusu mbele nusu nyuma
 
Waasia wamezoea kukaa mijini dunia nzima..kazi yao ni kunyonya tu na hawana msaada wowote..Tanzania wanafaidi coz NHC ni very cheap kulipia rent...ukweli ndo huo..
 
Anasema Mengi hata hadhi ya kujifanya anaweza kupambana na ufisadi ilhali yeye ni fisadi.

Anasema Mengi ni Nyangumi wa ufisadi anayeficha ufisadi wake kwa kupitia migongo ya wengine.
 
Waungwana,si tukae kimya wakati hizi live reports zinawasili?Tutapata nafasi ya kuchambua baada ya Invisible kutueleza kwamba press conference imekwisha.

Kwani wewe umelazimishwa usome kila kitu. Acha watu wajinafasi raha ya ngoma uingie ucheze, kama wewe kiuno kinauma basi kaa pembeni angalia tu, na si lazima kuangalia wachezaji wote. tafuta anayekuvutia basi concetrate naye.
 
Anasema Mengi hana hadhi ya kujifanya anaweza kupambana na ufisadi ilhali yeye ni fisadi.

Anasema Mengi ni Nyangumi wa ufisadi anayeficha ufisadi wake kwa kupitia migongo ya wengine.
 
Kwani wewe umelazimishwa usome kila kitu. Acha watu wajinafasi raha ya ngoma uingie ucheze, kama wewe kiuno kinauma basi kaa pembeni angalia tu, na si lazima kuangalia wachezaji wote. tafuta anayekuvutia basi concetrate naye.
Nami sikukulazimisha ukae kimya!Anyway,endelea kuongeza idadi ya posts zako!
 
Rostam anazidi kuudhi umma wa watanzania, itachukua karne kuwaelezea watanzania kuwa yeye ni msafi kuliko Mengi..sie wakristu tuansema.."vitaumbwa upyana nchi itageuka"...he is real FISADI PAPA.

Sory wana JF, hivi ni press conference ya kumwelezea historia ya Mengi au ni conference ya kujibu tuhuma husika...huyu milele hana hoja, cha msingi ni kumwomba asubiri siku Mengi akifa apewe nafasi ya kusoma risala ya Marehemu labda ndio atakuwa wa kwanza kuushauri ulimwengu kuwa marehemu alikuwa mtu mbaya saaaanaa..kwani tumezoea kila anayekufa huwa anasifiwa.

Hamumuoni hata jinsi alivyo/.....nusu mbele nusu nyuma

you are dead wrong! unless proven guilty.... anasema kaajiri watanzania 6,000, na amechaguliwa na watanzania kama wewe na mimi! sijui watanzania gani unawasema hapa mkuu!

mtarukaruka wee, nawaambia kila siku acheni kujadili mt mmoja mmoja, mtapatashida ONDOA CCM WOTE!
 
Anasema Mengi hana hadhi ya kujifanya anaweza kupambana na ufisadi ilhali yeye ni fisadi.

Anasema Mengi ni Nyangumi wa ufisadi anayeficha ufisadi wake kwa kupitia migongo ya wengine.

True true.

Kamanda Mwema, Rostam na Mengi wapelekwe rumande Keko halafu wataendelea na malumbano kizimbani. Laiti ningekuwa Rais.
 
Kaulizwa kwanini yeye atumie njia ya kujibu hoja kwa njia ya Mengi (Press Conference)?

Anajibu kuwa yeye hakuwa na dhamira ya kufanya hivyo lakini yeye ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi hivyo aliona vyema atumie njia hii kukana tuhuma alizokuwa amepewa na akaona vema alifahamishe taifa limjue Mengi ni nani na iwe rahisi watanzania waache kusikiliza porojo za Mengi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom