Tamko la LHRC na waandishi wa habari leo kuhusu mgomo wa madaktari!

Declaration of Geneva (1948)
Physician's OathAdopted by the General Assembly of the World Medical Association, Geneva, Switzerland, September 1948 and amended by the 22nd World Medical Assembly, Sydney, Australia, August 1968.

CIRP Introduction

The World Medical Association is an association of national medical associations. This oath seems to be a response to the atrocities committed by doctors in Nazi Germany. Notably, this oath requires the physician to "not use [his] medical knowledge contrary to the laws of humanity." This document was adopted by the World Medical Association only three months before the United Nations General Assembly adopted the Universal Declaration of Human Rights (1948) which provides for the security of the person.

Physician's Oath

At the time of being admitted as a member of the medical profession:

  • I solemnly pledge myself to consecrate my life to the service of humanity;
  • I will give to my teachers the respect and gratitude which is their due;
  • I will practice my profession with conscience and dignity; the health of my patient will be my first consideration;
  • I will maintain by all the means in my power, the honor and the noble traditions of the medical profession; my colleagues will be my brothers;
  • I will not permit considerations of religion, nationality, race, party politics or social standing to intervene between my duty and my patient;
  • I will maintain the utmost respect for human life from the time of conception, even under threat, I will not use my medical knowledge contrary to the laws of humanity;
  • I make these promises solemnly, freely and upon my honor.

Citation:
  • Declaration of Geneva (1948). Adopted by the General Assembly of World Medical Association at Geneva Switzerland, September 1948.
Sema wewe tukisema wengine naona hatueleweki,Halafu ati kuna watu wanajiita wanaharakati,wanasheria wa haki za binaadamu ambao wanachochea migomo chini ya mwamvuli wa maslahi ya madaktari na kuungana na Madaktari wanaogoma ili hali binaadamu wanapoteza maisha? haki za binaadamu hizo ni kwa madaktari tu Lakini kwa walalahoi waachwe wajifie tu,maana wao haki hizo haziwahusu.Hapa ndiyo jamii yetu ilipofika.Fani imevamiwa.........................!Utu umepotea.......................!
 
Hapo juu umewataja ''walalahoi ambao hali zao ni duni kupindukia''...
Je ni nani aliepelekea hali za hao jamaa kuwa duni kupindukia?
ni madaktari au ni mabepari walioko Serikalini?

Hapna madaktari wetu hawahusiki kwa namna yoyote na uwepo wa walala hoi,

Sababu za umasikini ni nyingi sana lakini Serikali kama chombo kilichopewa dhamna ya kutawala nchi haiwezi kusema haihusiki kwa namna yoyote.

Lakini hayo madai ya madaktari yakitekelezwa yote kama yalivyo yatapunguza au kuongeza umasikini? Sio kwamba yatawapaisha zaidi madaktari kuwa karibu zaini na tabaka la mabepari huku watu wa chini wakididimia zaidi?

Kama issue ni ufisadi suluhisho ni kukemea ufisadi lakini sio na sisi kuingia katika ufisadi. Kma issue mabunge na wanasiasa wanakula zaidi kuliko wataalamu mimi nipo na nyinyi lakini suluhisho sio nasisi kula kama wao au zaidi yao bali kutaka matabaka haya yakomeshwe. Harakati hizi hazipaswi kuwahusisha madaktari katika udaktari wao bali zifanyike katika ulingo wa siasa. Siasa ni eneo ambalo halina mwenyewe hata daktari akivua joho lake la udaktari na kuingia katika siasa anaweza kuwa mwanasisas mzuri tu na kutumia siasa kufikisha anachokiona ni sawa
 
Achana na hayo makombo ya waliokutuma uende ukasome udaktari uje utibu bure wagonjwa.

Kinachowapagawisha ni wasiwasi wenu wa utawala kuanguka halafu mnajifanya mnawapenda sana wagonjwa.

Kama mnawapenda wagonjwa na kuthamini uhai kama mnavyolalama hospitali zisingekuwa taabani na wala msingekuwa mnauwa watu msitu wa pande na kwenye maandamano ya amani.

Acheni unafiki
Na wewe kama kazi haina maslahi siuwache?Kwanini umnga'ang'anie muajiri ambaye hana maslahi na wewe,Mnagoma lakini Posho na Mishahara bado mnavuta ,wagonjwa wakija mnawadai rushwa kabla ya kuwapa huduma,au mnawaelekeza wawaone hospitali binafsi kwa maslahi yenu,huo ndiyo unafiki!Achaneni na serikali kwasababu siyo muajiri pekee, hakuna maslahi nenda kwenye maslahi,ili nafasi iwe wazi na serikali itangaze ajira kwa raia na wasio raia tuone kama nafasi zitashindwa kujazwa.
 
Inapofikia wanaona kwamba maslahi hayapo kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine ni bora zaidi kuliko kugoma. Unapogoma na kuendelea kupokea mshahara na posho zinazotokana na kodi zetu sisi huku tunakufa kwa kukosa matibabu Serikali haiwezi kuajiri mtu mwingine kwenye ajira ambayo bado ina mtu. Matokeo yake watu wanakufa wakati madawa, vifaa vya matibabu na wataalamu wenye utayari wa kufanya kazi wapo.

Katia matatizo yaliyomkuta daktari wetu, tumeona yeye akihudumiwa vizuri kwa kutumia madawa na vifaa vya Serikali huku wengine wanakataliwa kupata huduma kana kwamba binaadamu wote si sawa
 
Lazima ujifunze na ujue kuwa serikali sio JK na mawaziri na wakuu wa wilaya na wengine kama hao.

Kwa hiyo mimi na wao tumeajiliwa na wananchi na iwapo wananchi watataka nitoke nitatoka.

Wao ni mimi wote ni waajiriwa ila wao wamepewa jukumu la kuongoza lakini wanatumia vibaya nafasi hiyo kwa wizi na kuzorotesha huduma ikiwemo ya afya.

Swala la wizi na blah blah wanaliweza lakini wakiambiwa kuboresha huduma kwenye hospitali zinazotumiwa na wananchi wengi wanajifanya hawasikii wakikumbushwa wanaamua kuwaua wale wanaoona wanaongea sana kitu ambacho hakitaondoa tatizo.

Kama mnafikiri tatizo kubwa ni maslahi na si mazingira na vitendea kazi kwa nini basi msiboreshe hivyo halafu mje mseme kwa wananchi mmeboresha vitendea kazi na mazingira ya kutolea huduma lakini bado drs wanagoma.

Kuua drs hakutamaliza vifo vya wajawazito, mlundikano wa wagonjwa, kulala chini na ukosefu wa vifaa tiba.
 
Kwenye hizo nukata za matusi na kashifa sitakujibu nitamuachia moderator kama yupo aamue kama umenitendea haki kunitukana kwa kuniita mnafiki na kwamba na kwamba ninaongea makombo ya watu unaodai walionituma. Mimi sijapewa kupaji cha kushindana kwa matusi na sidhani kama hivyo ndivyo tunapawa kujadiliana katika mtandao wenye hadhi kama JF.

Hamna mtu anataka madaktari wafanye kazi bure wala hamna daktari anaefanya kazi bure hapa Tanzania. Issue ni namna madaktari tunavyoweka maslahi ya kimapato juu kuliko maslahi ya maisha ya wagonjwa wetu kinyume na kiapo cha miiko ya udaktari tulikula. Suala la Serikali kupinduliwa unaliibua wewe na sijui unalihusisha vipi na maandamano ya madaktari.

Sijui unaweza kutoa ushahidi gani wa mimi kuhusika kuuwa mtu katika msitu wa Pande. Kama huna hoja ya kujibu hoja sio vibaya kukaa kimya kuliko kutoa tuhuma nzito kama hiyo kwa mtu usiomjua wala asiyekujua.

Kama kuna dosali katika posts zangu ni vizuri ukanikosoa na kunirekebisha na wala sitashangaa. Maana, haya ninayotoa ni maoni ambayo kwa nafsi yangu na upeo waangu wa ufahamu nadhani kwamba ni sahihi. Lakini kama binaadamu naweza kukosea lakini sio sababu ya kutukanwa na kuzushiwa kashifa kubwa na chafu kama hizo.

Kwanza nashukuru wewe sio moderator.

Pili lazima uachane na ushabiki pale ambapo maslahi ya taifa yapo hatarini.

Mwisho kukemea upotoshaji sio matusi isipokuwa ukweli siku zote unagonga katikati ya kidonda.
 
Inapofikia wanaona kwamba maslahi hayapo kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine ni bora zaidi kuliko kugoma. Unapogoma na kuendelea kupokea mshahara na posho zinazotokana na kodi zetu sisi huku tunakufa kwa kukosa matibabu Serikali haiwezi kuajiri mtu mwingine kwenye ajira ambayo bado ina mtu. Matokeo yake watu wanakufa wakati madawa, vifaa vya matibabu na wataalamu wenye utayari wa kufanya kazi wapo.

Katia matatizo yaliyomkuta daktari wetu, tumeona yeye akihudumiwa vizuri kwa kutumia madawa na vifaa vya Serikali huku wengine wanakataliwa kupata huduma kana kwamba binaadamu wote si sawa

Ingekuwa binadamu wote ni sawa mngeboresha huduma na nyie mngekuwa mnatibiwa hapa hapa Tanzania sio kwenda India hata kuangalia afya.

Wananchi wa kawaida wanakufa kwa kukosa dawa za malaria. Hata dawa za malaria na vyandarua mpaka tutegemee misaada.

Wagonjwa wanalala chini nyie mnanunua magari ya anasa halafu hapa mnatuletea propaganda zisizo na kichwa wala miguu.

Hata ukijaribu kujificha kwenye maneno yako mimi nitakutambua tu na huwa najibu hoja ninazoona zinapotosha jamii na ukiangalia kwa wastani nina post 70 kwa mwaka sawa na wastani wa posti 5 kwa mwezi.

Lazima utambue kuwa ajira yangu sio hisani toka kwa wanasiasa ni haki na lazima pia niwezeshwe kutekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa ujuzi wangu na weledi, tiba haitakiwi kushindikana kwa kukosa dawa na vifaa bali kwa ujuzi.

Swala la kudai maboresho ya sekta ya afya ni mojawapo wa wajibu wa mwanataaluma yeyote wa afya na hili litaendelea bila kujali ameajiliwa katika sekta ya umma au la.

Mmepewa dhamana ya kuongoza Tufukuzeni mlete drs kutoka Iran. Hata hivyo hili halitayumbisha msimamo na wala hilo halitakuwa mwisho wa harakati ya mageuzi ya sekta ya afya.

Na pia wewe unaposema vifaa vipo inaonyesha wazi kabisa ni miongoni mwa wale msiotumia hospitali za hapa nchini, kwa hiyo hujui hata hali ya wodi zetu zikoje.
 
Masuala ya wewe kunitambua mimi au kutonitambua yasikupe shida. Lakini bahati mbaya mimi sio mwanasiasa wala mfanyakazi wa Serikali kama unavyonidhania.

Umahili wako wa kuandika posts nyingi katika JF hilo halina ubishi na nakupongeza kwalo. Pia naunga mkono changamoto yako kwa Serikali ya kuboresha huduma za afya ili zinufaishe watu wa kawaida.

Vifaa katika mahospitali yetu vipo na mimi na familia yangu huwa natibiwa katika hospitali hizo hizo tofauti na hisia zako. Ukweli tu ni kwamba havijafikia kiwango cha kuhimili matatizo yetu yote ya afya.

Haki ya ninyi na watu wengine kupata ajira mnayo na sio fadhira. Lakini haki ya kuacha kazi pale mnapoona maslahi ni madogo ni haki yenu ya kimkataba pia. Madaktari ni watanzania wenzetu wanaoishi katika mazingira tuliyonayo. Madai ya kuongezwa mshahara na malupulupu hadi kufikia 7,000,000/= kwa mwezi hayatutendei haki sisi wananchi wa kawaida. Leo tunalia mishahara mikubwa ya wabunge leo madaktari mnazidi kutuchanganya ziadi kwa kutaka mishahara isiyoendana na uchumi wetu tena mnataka mpatiwe mara moja na ikishindikana muendelee kupoteza maisha yetu kwa migomo.

Suala la Serikali kushindwa au kutoshindwa ni suala la kisiasa zaidi. Linaweza kuamuliwa kwa kura na sio migomo ya madaktari.
 
Lazima ujifunze na ujue kuwa serikali sio JK na mawaziri na wakuu wa wilaya na wengine kama hao.

Kwa hiyo mimi na wao tumeajiliwa na wananchi na iwapo wananchi watataka nitoke nitatoka.

Wao ni mimi wote ni waajiriwa ila wao wamepewa jukumu la kuongoza lakini wanatumia vibaya nafasi hiyo kwa wizi na kuzorotesha huduma ikiwemo ya afya.

Swala la wizi na blah blah wanaliweza lakini wakiambiwa kuboresha huduma kwenye hospitali zinazotumiwa na wananchi wengi wanajifanya hawasikii wakikumbushwa wanaamua kuwaua wale wanaoona wanaongea sana kitu ambacho hakitaondoa tatizo.

Kama mnafikiri tatizo kubwa ni maslahi na si mazingira na vitendea kazi kwa nini basi msiboreshe hivyo halafu mje mseme kwa wananchi mmeboresha vitendea kazi na mazingira ya kutolea huduma lakini bado drs wanagoma.

Kuua drs hakutamaliza vifo vya wajawazito, mlundikano wa wagonjwa, kulala chini na ukosefu wa vifaa tiba.

Nakubali kwamba wananchi ni bosi wa Raisi pamoja na ninyi wafanyakazi wa Umma. Raisi ni muajiriwa wa moja kwa moja wa Wananchi na kweli wana nguvu zote za kukatisha ajira yake. Kwa niaba ya hao hao wananchi, Raisi ndio muajiri mikuu wa watumishi wote wa umma na ana nguvu zote za kukatisha ajira zao ili mradi tu azingatie Katiba na sheria za nchi ambazo ndizo nyenzo alizopewa na wananchi kutawala kwa niaba yao.

Zipo njia za kisheria za kumlalamikia au kumshita Raisi kwa wananchi lakini katu sio migomo ya madaktari. Kama vile Raisi alivyoajiriwa na wananchi kwa njia ya kisiasa, atashitakiwa kwa wananchi kwa njia za kisiasa vile vile. Lakini kwakuwa madaktari hawakuajiliwa kwa njia ya kisiasa bali kwa sheria na mikataba, ajira zao pia zinapswa kushughulikiwa kwa namna hiyo hiyo.

Madakatri kama watanzania mnaruhusiwa kuacha kazi katika utumishi wa umma na kuanzisha au kujiunga na vyama vya siasa kama mnataka kumlalamikia Raisi kwa mabosi wake.
 
Hayo bwana Kigogo ni madai mengine.

Wapo wanansiasa waliokuwa na madai kama haya haya na wakafikia hata kutomtambua Raisi kama Raisi wa nchi. Lakini baade walibadilisha misimamoo yao na sasa wanashilikiana na kumtambua Raisi kama kawaida.

Bila kuwa na takwimu ya Raisi aliiba kura ngapi na za nani, madai kama hayo yanaweza kubaki kama madai ya miaka yote ya kisiasa.

Yanga akifungwa na simba na kinyume chake yanga kukubali moja kwa moja kwamba ameshindwa huwa ni mwiko. Atesema refa alinunuliwa, wachezaji walinunuliwa, uwanja ulikuwa mbaya nk. Mara nyingine huwa huchukuliwa kama utani wa kunogesha ushindani katika soka kati ya miamba hii miwili
 
Kwanza nashukuru wewe sio moderator.

Pili lazima uachane na ushabiki pale ambapo maslahi ya taifa yapo hatarini.

Mwisho kukemea upotoshaji sio matusi isipokuwa ukweli siku zote unagonga katikati ya kidonda.

Sasa kati yangu na wewe ni nani anaeleta ushabiki bila kujali maslahi ya umma? Wewe unashabikiwa migomo ya madaktari licha ya ukweli kwamba inasababisha vifo vya wananchi wasio na hatia. Kwa maoni yangu, maslahi ya umma ni kutokuwepo migomo inayosababisha watu kupoteza maisha yao. Labda ufafanue kwa maoni yako maslahi ya umma ni yapi.

Suala la kutukanwa au kutotukanwa niwaachie wasomaji waamue. Hata hivyo, nashukuru katika post hii umetumia lugha inayomezeka japo ujumbe wako unaweza kuwa mzito au mwepesi.

Kidonda hutoneshwa kama kipo na pia kwa sababu. Bahati nzuri haya ninayoyasema mimi yanatoka moyoni na kwa dhamira safi kwa nchi yangu. Sina ninapotonesheka ila nasikitika tunapotumia lugha zenye lengo la kutoneshana. Mimi ni mnyonge wa lugha hii lakini siku mkikutana na watu mahili wa lugha hizi, mnaweza kuleta mtikisiko katika Forum yetu
 
Sema wewe tukisema wengine naona hatueleweki,Halafu ati kuna watu wanajiita wanaharakati,wanasheria wa haki za binaadamu ambao wanachochea migomo chini ya mwamvuli wa maslahi ya madaktari na kuungana na Madaktari wanaogoma ili hali binaadamu wanapoteza maisha? haki za binaadamu hizo ni kwa madaktari tu Lakini kwa walalahoi waachwe wajifie tu,maana wao haki hizo haziwahusu.Hapa ndiyo jamii yetu ilipofika.Fani imevamiwa.........................!Utu umepotea.......................!
watz sijui mukoje?cant u think outside the box 4 a minute?hivi katiba ya nchi inasemaje kuhusu utu au uhai wa mtu?oath ya madaktari kwenye suala hilo ina tofauti gani kimantiki na ile ya hao wanasiasa tuliowapa mamlaka ya kuongoza serikali?ni nini chanzo cha mgogoro kati ya serikali na madaktari?je ni madr au ni serikali?madr wanasemaje kuhusu madai yao na wanasuggest yatekelezwe vipi kulingana na hali ya uchumi iliyoko sasa?nilisikiliza kipindi chanel 10 cha Jenerali on monday akiongea na viongozi wa jumuiya ya madaktari,Kwa ungesikiliza ungesikitika sana kwa jinsi serikali isivyo serious kwenye jambo la msingi kama hili linalogusa utu/uhai wa raia wake waloapa kuulinda.shida tunasikia sana upande mmoja, wa serikali ila kwa mtu huru anayetaka kuwa critical zaidi ataona pia lack of seriousness ya gvt kwenye hii saga
 
Hamna atakayesema kwamba madai ya madaktari kwa ujumla wake hayana msingi. Hata Raisi wakati akinena na wananchi alinainisha kuhusu hili na kusema kwamba madai mengi kati ya hayo yamekubalika.

Kwamba wanasiasa wanakula viapo na wanakiuka baadhi yao ni mambo ambayo tunayajadili kila siku. Lakini hiyo haiwezi kuhalalisha madaktari kwenda kinyume na viapo vyao. Wanasiasa kama wanasiasa zipo njia za kuwashughulikia zikiwemo za kisiasa na kisheria. Za kisiasa zipo mikononi mwa wananchi kwa ujumla wao ima kwa kupitia kura au kuwakilishwa na wabunge wao. Na hayo yamekuwa yanafanyika mara kadhaa. Kisheria kama kuna ushahidi wa moja kwa moja kutumia mahakama na hayo pia kwa mara kadhaa yamefanyika.

Kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa wanaokiuka viapo vyao visiwafanye madaktari kukiuka viapo vyao bila kijali maisha ya watu wao. Waendeleee kudai haki wanazostahili kwa njia zinazokubalika kulingana na fani yao ya udaktari. Sheria za nchi na za kimataifa zinaweka taratibu hizo bayana. Hamna sababu yoyote kufanya migomo kwa kushinikiza Serikali ikubali kupandisha mishahara na malupulupu ya madaktari kufikia zaidi ya milioni saba katika hali hii ya uchumi tulionao. Mafao makubwa kama hayo bila shaka yatahitaji ridhaa ya wananchi kupitia wabunge wetu ambao ndio tutakuwa waathirika wa kwanza wa ongezeko kubwa kama hilo la matumizi. Hata Raisi kwa mazingira ya uchumi kama haya tuliyonayo na kwa bajeti hii tuliyonayo hana uwezo wa kuwapa hilo.

Hili halihitaji maneno mengi sana kueleweka.

Ndio maana Serikali inawaruhusu kufanya kazi katika muda wa ziada kwenye hospitali nyingine za binafsi kuongezea mapato.
 
Declaration of Geneva (1948)
Physician's OathAdopted by the General Assembly of the World Medical Association, Geneva, Switzerland, September 1948 and amended by the 22nd World Medical Assembly, Sydney, Australia, August 1968.

CIRP Introduction

The World Medical Association is an association of national medical associations. This oath seems to be a response to the atrocities committed by doctors in Nazi Germany. Notably, this oath requires the physician to "not use [his] medical knowledge contrary to the laws of humanity." This document was adopted by the World Medical Association only three months before the United Nations General Assembly adopted the Universal Declaration of Human Rights (1948) which provides for the security of the person.

Physician's Oath

At the time of being admitted as a member of the medical profession:

  • I solemnly pledge myself to consecrate my life to the service of humanity;
  • I will give to my teachers the respect and gratitude which is their due;
  • I will practice my profession with conscience and dignity; the health of my patient will be my first consideration;
  • I will maintain by all the means in my power, the honor and the noble traditions of the medical profession; my colleagues will be my brothers;
  • I will not permit considerations of religion, nationality, race, party politics or social standing to intervene between my duty and my patient;
  • I will maintain the utmost respect for human life from the time of conception, even under threat, I will not use my medical knowledge contrary to the laws of humanity;
  • I make these promises solemnly, freely and upon my honor.

Citation:
  • Declaration of Geneva (1948). Adopted by the General Assembly of World Medical Association at Geneva Switzerland, September 1948.

Hivyo viapo hawa madaktari wetu naona hawavitambui. Shame!
 
Back
Top Bottom