Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Katiba inayopendekezwa na Mahakama ya Kadhi

Yanapotokea mahafa Mnawaitaji kwenye maombezi Mnapo fungua vikao na mikutano mnawaitaji wafunge nakufungua, mnapofariki mnawaitaji kwenye maziko, mnapo zaliwa mnawaitaji mbatizwe, mnaponunu shamba au nyumbakujenga mnaitaji haibariki.. jitafakarini namaneno yenu

mkuu ccm ni wanafiki sana, kila siku wanawapigia kelele na kuwaomba viongozi wa dini waiombee nchi amani, wanasahau kuwa kuwa kazi ya viongoz wa dini ni kuwaongoza waumini wao katika njia za Kweli na Haki!
 
Ongezea na yale matusi makubwa ya nguoni mliyomtuma Samwel Sitta kutukana mababa Askofu

Mama lemo mbona hivyo? Tetea amani nchini kwako. Hv unajua hata hao watoto uliowazaa nje ya ndoa wataishi katika nchi ambayo ww unataka ichafuke.
 
Kabla hujasoma makala haya ni vema utumie muda mfupi kumuomba Mwenyezi Mungu kwa imani yako akuongoze kuutambua ukweli. Usishawishiwe na kitu kingine katika kuusoma isipokuwa kujua ukweli. Katika kuujadili, usiongozwe na kitu kingine isipokuwa kile unachoamini kuwa ni ukweli au kinachokuwezesha kujua ukweli, na katika kuufanyia kazi, daima uzingatie ukweli.

Muombe akujalie moyo wa subira na uvumilivu, akuepushie jazba na mihemko. Akupe uwezo wa kusikiliza na kutafakari hoja za wale unaotofautiana nao kimaoni na kiimani. Akuwezeshe kuupokea, kuupenda na kuufurahia ukweli hata kama katika hali ya kawaida ukweli huo unauma.

Uamuzi wa kuandika makala haya ulikuwa mgumu kwangu kutokana na ukweli kwamba ninayokusudia kuandika yanatofautiana na matamko ya maaskofu, watu ambao huaminiwa na kuheshimiwa sana na jamii nzima wakiwemo wenye dini tofauti na yao. Katika hali hiyo, sitashangaa ikiwa nitakabiliwa na vitisho, vikwazo na kukatishwa tamaa. Hata hivyo, sitarajii kukata tamaa wala kuogopa vitisho.

Mungu ibariki Tanzania

Kabla sijaanza, ni muhimu niwakumbushe ndugu wasomaji kuwa Historia na hata vitabu vitakatifu huthibitisha kuwa uongozi katika dini sio utakatifu wala ukamilifu. Miongoni mwa wahalifu wakubwa waliowahi kutokea duniani wamo pia waliokuwa viongozi wa dini, hivyo hatuna sababu ya kuamini kila lisemwalo au kuelekezwa na viongozi wa dini bila kulitafakari kwa akili zetu wenyewe.

Kuna mifano mingi ya viongozi wa dini kujihusisha na uhalifu lakini ni vizuri nitaje ile ambayo wengi wetu tumeishuhudia na bado tunaikumbuka. Kwanza, miongoni mwa washitakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda ni maaskofu na mapadri, na baadhi ya mauaji hayo yamefanyikia makanisani kwa maelekezo yao.

Pili, hivi karibuni kanisa limekumbwa na kashfa ya viongozi wake kulawiti na kudhalilisha kingono watoto waliokuwa chini ya uangalizi wa kanisa hilo. Kwa muda mrefu watumishi wa kanisa hilo wamekuwa wakiwalinda na kuwafichia siri wahalifu hao hadi watu wengine nje ya kanisa walipofichua siri hiyo.

Tatu, bado Watanzania hawajasahau masaibu waliyopata baada ya kutapeliwa na kampuni ya kikanisa ya DECI, maarufu kama kampuni ya kupanda na kuvuna pesa. Viongozi wake ambao ni maaskofu na wachungaji waliwadanganya, na wengine bado wanawadanganya watu kuwa DECI ni jibu la umaskini kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya wao kukesha wakiomba na kufunga kwa muda mrefu wakimlilia awaondolee waja wake baa la umaskini.

Mimi huwa najiuliza: Kama tungetahadharishwa mapema kabla ya matukio haya, ni wangapi miongoni mwetu wangeamini kuwa yanaweza kutokea?.Ukweli ni kwamba ni wachache sana, na ndio maana hata watuhumiwa wa utapeli wa DECI walipokamatwa watu waliandamana wakitaka waachiwe na kuiona serikali iliyowakamata kuwa ndiyo isiyowatakia mema wananchi wake.

Nimetaja mifano hiyo kwa lengo moja tu la kuthibitisha ukweli kwamba uongozi katika dini sio utakatifu hivyo hakuna sababu, na kwa kweli ni ujinga wa kiwango cha juu sana, kupokea maelekezo, hasa ya kidunia, ya viongozi wa dini bila kujiridhisha kwa akili zetu kuwa maelekezo hayo ni sahihi.

Maaskofu wa Tanzania wamekuwa na kawaida ya kutoa matamko ambayo yanatia shaka kuhusu dhamira yao halisi. Hawana kawaida ya kujibu hoja za wengine, hivyo ni vigumu kupata ufafanuzi toka kwao. Kwa sababu hizo, nimelazimika kuandika makala haya ambayo natarajia yatazua mjadala miongoni mwa watu wa kawaida utakaosaidia kuweka wazi dhamira yao na pengine kuondoa shaka iliyopo kuhusu dhamira hiyo.

Ni ukweli ulio wazi kuwa matamko yao ni ujumbe maalum. Ili ujumbe wowote ufike kama ulivyokusudiwa, ni muhimu kwa mtoa ujumbe kuwatambua walengwa wa ujumbe wake na kuchagua njia bora ya kuuwasilisha ili uweze kufika, kupokelewa na kufanyiwa kazi kama alivyokusudia.

Hata hivyo, maaskofu wa Tanzania kupitia Jukwaa la Wakristo na mikusanyiko yao mingine wamekuwa na kawaida ya kutoa matamko ambayo moja kwa moja huilenga Serikali,

Wakati mwingine huyachapisha na kuyasambaza hata kabla matamko hayo hayajawafikia walengwa. Hapo ndipo huwa najiuliza: Lengo lao hasa ni nini?.Katika matamko yao mara kwa mara hutaka kuwaaminisha watu kuwa wao ni wapigania haki, amani na maelewano na hasa baina ya Waislamu na Wakristo.

Hata hivyo, busara ya kawaida inaonyesha kuwa maaskofu peke yao hawawezi kupigania haki, amani na kusuluhisha migogoro baina ya Waislamu na Wakristo, kama wanavyotaka tuamini, bila kushirikiana na serikali, viongozi wa dini ya Kiislamu na watu wengine wenye imani tofauti na Ukristo.

Pamoja na ukweli huo ulio wazi, wao wamekuwa wakikaa peke yao na kutoa matamko ambayo kwa tafsiri ya kawaida ni maagizo au amri za kutekelezwa bila kuhojiwa. Kibaya zaidi ni kwamba amri hizo hazitolewi moja kwa moja kwa walengwa na kutoa fursa ya utekelezaji wake bali huchapishwa na kusambazwa mara tu wanapoyatoa.

Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni kwa makusudi kuwafanya wananchi waamini taarifa za upande mmoja kwa kuhakikisha kuwa hawapati fursa na haki ya kusikiliza upande mwingine. Kwa maneno mengine ni kuzuia watu kujua ukweli.

Kwa ujumla, kutowashirikisha wadau wengine au angalao kuwaachia fursa ya kushiriki na badala yake kuwapa amri kwa njia isiyo rasmi ambayo haina hata uhakika wa kufikisha amri hiyo, kuisambaza au kuacha amri hiyo isambae kwa wananchi bila kujali kama imewafikia walengwa au haijawafikia, kunaweza kuwa na tafsiri kadhaa miongoni mwa hizi zifuatazo:

1. Matamko hayo (ya maaskofu) ni amri ya kutekelezwa isiyopaswa kuhojiwa na mtu yeyote.

2. Hakuna mwenye uwezo wa kufikiri na kutoa maamuzi bora kuliko wao (maaskofu), hivyo hakuna anayeruhusiwa kuhoji uamuzi wao, na hilo ni lazima lieleweke kwa kila mtu bila kujali nafasi yake katika jamii.

3. Wenye mamlaka na waliopo kwenye nafasi za kutoa maamuzi hawastahili kushika nafasi hizo isipokuwa tu kama wanazishika kwa kuwawakilisha maaskofu au wanafanya kazi kwa kibali cha maaskofu na mara zote hufuata miongozo ya maaskofu.

4. Maaskofu hawa wana dhamira tofauti na wanavyotaka watu waamini. Kutokuwa kwao tayari kutoa ufafanuzi wa matamko yao inaweza kuwa mojawapo miongoni mwa njia za kuficha dhamira yao hiyo.

5. Hawana nia ya kusuluhisha migogoro baina yao na wadau wengine, badala yake wanataka kukuza migogoro hiyo kwa kutafuta sababu za kuiendeleza. Kwa sababu hiyo, hawataki kusikia wala kuruhusu wananchi kusikia maoni ya wadau wengine kabla na hata baada ya kutoa matamko. Hawataki kufafanua amri zao na kuhakikisha kuwa zinaeleweka, na kwa ujumla hawataki watu wafikiri na kuamua kwa akili zao bali wapokee tu yale wanayowaambia.

6. Kuchonganisha serikali na wananchi wake pamoja na kuwachonganisha Waislamu na wasio Waislamu kwa sababu wanazojua wao.Maaskofu wamekuwa wakitoa mfululizo wa matamko ambayo huwafikia wananchi moja kwa moja na kuwahusu moja kwa moja.

Katika hali ya kawaida, tungetarajia maaskofu hao pia wawe wakitoa taarifa kuhusu kutekelezwa au kutotekelezwa kwa yale ambayo walikwishayatolea matamko huko nyuma na taarifa hizo zifike kwa njia ile ile waliyotumia kufikisha matamko hayo.Hata hivyo, maaskofu hao hawana kawaida ya kutoa mrejesho nyuma (feed back) kuhusiana na matamko yao. Kama wanatoa, hawafanyi hivyo kwa uwazi ule ule wanaoutumia kutoa matamko wala kulenga watu wale wale.

Hali hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa ni namna mojawapo ya kufunika dosari za matamshi yao ya nyuma badala ya kuzikiri na kwa makusudi kuacha athari za baadhi ya dosari hizo kuenea katika jamii.

Hali hiyo pia inaweza kuwa ni kupima muitikio wa jamii kuhusu matamko yao na ikibidi kuyabadili ili kukidhi malengo yao wanayoyajua wao.
 
Mkuu
Kama wachangiaji wa mwanzo walivyosema nami naungana na wao kukupuuza.
Nadhani tafakari matamko yao tena.
 
Pamoja na mtoa mada kujaribu sana kuonyesha weledi wake, ni dhariri kabisa ulichoiandika umekiandika kwa kusukumwa na chuki dhidi ya Maaskofu na Ukristo kwa ujumla. Uhalifu wote ulioutaja wa viongozi wa dini ulishindwa kabisa ku-balance. Umetaja uhalifu wa mapadri na maaskofu utadhani mashehe na Mamufti wanaobariki watu kukatwa vichwa katika matukio ya kigaidi wao ni Malaika. Nani asiyejua kwamba matukio yote ya kigaidi yana baraka ya baadhi ya viongozi wa dini yako? Au ugaidi sio uhalifu bali ni ibada au siyo? Ungekuwa umeonyesha weledi wako kama ungetaja madhaifu ya pande zote mbili hali kadhalika nguvu za pande zote mbili.
Isitoshe, kwanini mnang'ang'ania chombo chenu cha kidini kuwa sehemu ya mhimili wa dola? Kwanini msikianzishe wenyewe, mkisimamie na kukiendesha wenyewe? Kwanini ni lazima kiwe mhimili wa dola? Hapo kuna jambo kubwa lililofichika nyuma ya pazia. Hatutaki serikali ya kidini na huo ndio msimamo wetu. Kama ni dini wacha tuziendeshe makanisani, misikitini na mahekaluni. Serikali ibaki kuwa ya wote pasipo kufungamana na dini yeyote. Huu ndio mfumo unaotufaa watz. Hata kama mnaamini kwamba ninyi ni 82% ya watanzania wote kama mlivyoaminishwa, takwimu ambazo hazina ushahidi wa kitaalamu. Bado ijulikane nchi hii ni haki sawa kwa wote hata kwa yale makundi madogo kabisa. Hakuna Kuwa na Kundi la mabwana na wengine kuwa watwana.
 
Mama lemo mbona hivyo? Tetea amani nchini kwako. Hv unajua hata hao watoto uliowazaa nje ya ndoa wataishi katika nchi ambayo ww unataka ichafuke.
Jamani nyie wabongo nani amewatia upofu. Sasa ni nani anayetaka kuchafua amani - ccm na upuuzi wake wa kutumia kete ya udini kwa kucheza na akili za Waislamu au Maaskofu wanaotoa angalizo la kuzingatia Katiba kwamba vyama vya siasa na serikali visijiingize katika masuala ya dini ambayo kwa vyo vyote vile yataleta mpasuko wa kitaifa?
 
huyu nafikiri alikuwa alikuwa anataka kuandia barua ila akakosea adress akaituma uku ila ndio walewale tumsamee bure
 
Maaskofu mtakula sadaka zetu kwa nguvu lakini hamtatulazimisha kuikataa Katiba, kura yangu ni siri.

Ukiwa kibaraka ujue pia kutumia akili zako kama zipo. Ni mamluki tu wasiotumia akili zao cause they fight without even knowing the cause. You represent them. Hopeless kabisa. Una hela gani ya kuwapa maaskofu sadaka wewe? Hiyo hiyo ya b7?
 
Kama hujui cardinal pengo ambae ni kiongozi wa dini tena mkubwa anawaponda maaskofu wa ukawa kwa kutaka kuleta machafuko nchini.
 
Back
Top Bottom