Mzee Dingi10
New Member
- May 7, 2019
- 2
- 0
Habari za asubui wanajamvi?!
Mimi ni mhanga wa uhamisho baada ya Serikali kusitisha uhamisho nilikuwa kwenye proceess za mwisho kabla ya uhamisho kufungwa.Hivyo sikubahatika kuhama kwani Tamisemi walidai wanaboresha uhamisho na soon ungelifunguliwa. Lakini cha kushangaza mpaka leo hakuna kuhama kwa mfanyakazi yeyote.
Kasumba iliojikita ni kwamba mtumishi anatakiwa kulipa 700000 mpaka 1000000 ili aweze kuhama na hazipiti wiki mbili unakuwa umehamia kwenye kituo chako.
Anachofanya mfanyakazi anayehama nikuandika barua ya geresha ya kuomba kuhama ambayo iyo barua huishia halmashauri ya mwalimu alioajiriwa kama ushahidi geresha na wapo wengine huwa hawaandiki kabisa lakini haipiti wiki 2 wanakuwa wamehamishwa.
Nina wajua wanaofanya mchezo huuu wakuwatoza watumishi pesa na kuwaamisha katika wiki zisizopungua 2.
Hivyo ushauri kwa serikali watu hawa wathibitiwe najua wapo wengi au kama ni mfumo rasmi ambao wizara ya Tamisemi inautambua basi waweke utaratibu maaalum kwani ajili ya malipo hayo kwani vishoka wamekuwa wengi na matapeli wamekuwa wengi nimepigwa 900,000 mwezi uliopita.
Hivyo tunaiomba Tamisemi kuwa makini hasa wale waliopo kwenye vitengo uchapaji wa barua za uhamisho majina yao ninayo.
Lakini kama ni mfumo rasmi basi uratibiwe vyema ili serikali ijipatie mapato kuliko kuishia kwenye mifuko ya watu