Tambwe Hizza: Kikwete ni bora kuliko Nyerere!

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,515
20,005
katika kuonyesha hali ya kujipendekeza kupita kiasi au kutojua mambo,tambwe hiza jana usiku katika kipindi cha kurunzi ya mlimani aliropoka eti kikwete ni bora kuliko nyerere eti kwa sababu tu ya serikali ya mseto ya zanzibar iliyompa seif hamad umakamu wa kwanza wa rais,..na kuhusu dowans,tambwe alisema jk ana uvumilivu sababu angekuwa kiongozi mwingine angekuwa kashainnua mitambo ya dowans....
 
HUYO ni kichaa na sijui ndo mana anaachwa aropoke kila anachojikia kusema
 
Acha uhuni na upotoshaji wewe, nenda mlimani wakupe record ya jana. alichosema ni kuwa wakati wa Mwalimu changamoto zilizopo sasa hazikuwepo. Ni kweli Tambwe hiza anaongea pumba most of the times but penye ukweli weka ukweli bila chumvi. Swala la kununua mitambo ya dowans alisema kama JK angekuwa si mvumilivu yaani mwenye jazba kama yeye (tambwe hiza) angeinunua hiyo mitambo zamani sana, ingawa hajui kuwa Rais hana hayo mamlaka ya kununua vitu bila kufuata utaratibu wa PPRA.
 
hatuna kitu hapa kwa ubora upi..............ombwe ...................despite nyereres shortcoming he did his best those years...bt mkwele with this 21 century...nothing to be proud of kuomba omba daily kwa watu...despite all resources n mgao unanichapa 16hours daily....wacha nifanye kazi mimi wanangu wapate kwenda academia skul..4 thr bright future..:coffee:
 
Unajua Tambwe ameshajulikana ni mtu wa pumba, hivyo hata akitoa nondo za uhakika siku moja, watu wanachukulia ni pumba zile zile. Point kama hiyo ingesemwa na mtu mwingine ingekuwa sustainable. Lakini kwa Hiza hakuna kitu.

Namshauri afanye propaganda kwa njia nyingine, hii kwenda laivu anazidi kujimaliza.
 
Tutawafunga midomo baada tu ya sisi wenyewe kubadilika. Walopokaji hawana nafasi katika jamii makini, jamii inayojibidisha kutetea kile kilicho chao, jamii ambayo kazi ndiyo msingi wa maisha. Hivi sasa Tanzania ni nani anayetaka kufanya kazi? Hakuna watu wanataka kulipwa bila kufanya kazi na hasa wasomi, wamekuwa ni chumvi ya kurudisha nyuma maendeleo. Hii hasa ndiyo sababu ya watu wasiokuwa na IQ kulopoka na sisi tunawasikiliza tu. Kama leo watu kumi wangefika ofisini kwake na kumconfront kesho asingerudia tena. Lakini kwa vile anafanya na hakuna anayemweleza hivyo tabia imekuwa kilema sasa.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi bado mnamsikiliza huyo MWENDAWAZIMU? mi nilivyo-tune hiyo station kumuona tu huyo shoga basi siku-tune tena hapo.
 
Pamoja na pumba zake Tambwe, mbona vyombo vya habari bado vinamfuata sana na hasa Tv zetu? Anajipeleka?
 
...bora kwa mkeo na binti yako! Hivi hawa watu vipi? Watanzania si vipofu ati, tunaona na wala hatuhitaji mtu kutuchagulia mtu bora. Nyerere si Mungu lakini angalau hakufuga mafisadi! Tunaomba akawaambie mkewe na binti yake maneno asitulete uozo wake hapa!
 
Anatetea mkate wake. Jana nilisema why don't our African leaders got the balls to tell the truth? Kumlinganisha Nyerere na Kikwete ni km kumlinganisha Arnstein na Mwalimu wa vidudu.... Serikali ya mseto Nyerere alishauri tokea hajafa, kiburi cha wazanzibari hadi wakauana. Anasema Kikwete ni mvumilivu? Do we really needs tolerant leaders who root poverty among Tanzanians cuz of their tolerance? We want leaders who are action-oriented and result based. The qualities that Kikwete don't have......... Japo anatetea mkate let the truth stand, be defended and be agitated till end.....
 
Acha uhuni na upotoshaji wewe, nenda mlimani wakupe record ya jana. alichosema ni kuwa wakati wa Mwalimu changamoto zilizopo sasa hazikuwepo. Ni kweli Tambwe hiza anaongea pumba most of the times but penye ukweli weka ukweli bila chumvi. Swala la kununua mitambo ya dowans alisema kama JK angekuwa si mvumilivu yaani mwenye jazba kama yeye (tambwe hiza) angeinunua hiyo mitambo zamani sana, ingawa hajui kuwa Rais hana hayo mamlaka ya kununua vitu bila kufuata utaratibu wa PPRA.

wewe ndio mhuni usiyeweza kuchambua mambo,yule ***** kamdiss nyerer btn the lines,..au ulitaka atamke kabisa kuwa kikwete ni bora kuliko nyerere??
 
Is this true kwa kweli?? I doubt it! Najua Hizza suffers from verbal diarrhoea but eti kasema live Kikwete ni bora kuliko Nyerere is far fetched in my view! Only a mad man can misuse Nyerere's name like that! Hizza is not that daft!
 
Back
Top Bottom