Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,514
- 21,997
Hii inawahusu wote wanahangaika kutafuta maombezi kwa mitume na manabii kwamba waombewe ili tamaa za ngono itoweke nawaombeni mjifunze kitu hapa.
Mpendwa usihangaike kukusanya sadaka ya Kumpelekea nabii eti akufungue uache ngono, hakuna kitu kama hicho. Hata huyo nabii unayetaka akuombee huwa anakutamani akuonje na ukizubaa kidogo tunda linaliwa tena sio kimasihara bali kwa kukusudia.
Iko hivi..... Mungu haondoagi tamaa zetu za ngono kwa sababu ngono ni hitaji lililo rasmi la mwili. Hii ni kama vile ilivyo kwa Mungu kutoondoa hitaji letu la chakula hivyo kaweka njaa ili tule na tushibe.
Haja ya ngono imejengwa na Mungu mwenyewe ndani ya mwili wa mwanadamu kwa makusudi maalum hivyo hata kukemea roho ya uasherati hakuwezi kukuweka safi kingono unaweza kwenda na maji siku upwiru ukikomaa na wewe.
Jifunze kitu kwa mfano huu.... Yesu alimsamehe mwanamke ambaye alikamatwa katika tendo la uzinzi, alimhoji maswali machache tu kisha akamtangazia msamaha na akamshauri aache(asitende) dhambi (uzinzi) tena. Hapo Yesu alimaanisha uzinzi ni chaguo, na SIO pepo mchafu. Iwapo uzinzi lingekuwa pepo, basi Yesu angelikemea kwa wema ili limtoke huyo mwanamke, hakufanya hivyo kwa sababu uzinzi ama kuwa uzinzi ni chaguo la mtu na sio la pepo mchafu.
Wa kulala naye huwa ni chaguo la mhusika. Ndiyo maana Mungu anatuamuru tuwe wanyoofu kingono. Anasema, "Usizini." Iwe umeoa au umeolewa, Mungu anasema, “Ikimbieni zinaa - 1 Wakorintho 6:18.
Ikiwa hujaoa ama kuolewa na unawaka tamaa kupeleka ama kupelekewa moto mara kwa mara, ni vyema ukichukua hatua ya kupata mwenza na ukafunga naye ndoa muendelee kupelejeana moto kihalali (1Kor 7:8-9).
Ikiwa umeoa /umeolewa, heshimu ndoa yako na uweke kitanda chako kiwe safi (Ebr 13:4). Hivyo kila mtu anaweza kudhibiti hamu yake ya ngono kwa kuheshimu ndoa yake.
Biblia inakazia njia moja ya kuepukana na uasherati nayo ni kufanya ngono mara kwa mara katika ndoa, kwa maana hakuna kunyimana (1Kor 7:2-5).
Sasa basi kumwombea mtu aache ngono ni sawa na Kumwombea mtu akose chakula, ombezi hilo huwa haliwezeshwi na mungu.
Ubarikiwe.