Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA
Na Mwandishi wetu

BAADA ya Timu Maalum ya Rais ya kuchunguza wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (EPA) kukabidhi taarifa yake kwa Rais Jakaya Kikwete mwezi uliopita, taasisi mojawapo kati ya tatu zilizohusika imeenguliwa.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeengiliwa kwa agizo ‘kutoka juu’.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali ngazi ya juu kunatokana na mchango wa tasisi anayoiwakili mjumbe huyo kuonekana mdogo.

Timu hiyo inatakiwa kukamilisha kazi yake mwishoni mwa mwezi ujao kama ilivyoelekezwa na Rais Kikwete.

Kazi zilizobaki kwa timu hiyo ni pamoja na kusimamia urejeshwaji wa sh11 bilioni kutoka kwa makampuni yaliyohusika na ubadhilifu huo ndani ya Benki Kuu.

Pamoja na kubakia na kazi hiyo, timu hiyo imebaki na jukumu la kusimamia upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia serikali kupata taarifa za makampuni ambayo yameficha mali zake nje ya nchi kwa kutumia ushirikiano wa polisi wa kimataifa ‘Interpol’.

Taarifa za ndani ya serikali zinaonyesha kuwa Takukuru wameondoshwa katika timu iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, Said Mwema pamoja na Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea.

Taasisi hiyo imeondolewa, haijajulikana bayana kama ni Rais Jakaya Kikwete ndiye alitoa maamuzi hayo.

“Kimsingi ni kama Takukuru iliondoshwa katika mchakato huu katika hatua za mwisho, wakati timu ilikuwa inaandaa ripoti kwa ajili ya kuifikisha kwa Rais kama ilivyokuwa imeelekezwa,” kilisema chanzo chetu.

Aidha chanzo hicho kilisema kitendo cha kuondoshwa kwa taasisi hiyo nyeti pengine inatokana na kazi za msingi za kamati hiyo kumalizika na kubakia majukumu ya kuwapeleka watuhumiwa mahakamani pamoja na kuwafuatilia walioficha mali nje ya nchi.

Chanzo chetu kinasema lengo kubwa la kuwahusisha Takukuru ilikuwa ni kutumia uwezo wao wa kiuchunguzi kuisaidia timu hiyo kuharakisha mambo zaidi.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa huenda Takukuru wameondolewa katika timu hiyo kutokana na kuvuja kwa kazi iliyokuwa ikifanyika.

“Baadhi ya siri za timu hiyo ilikuwa inaoongozwa na mwanasheria mkuu wa serikali zilikuwa zinavuja kila baada ya kikao, hivyo kuipa timu wakati mgumu wa kuendelea na kazi waliyopewa,” alisema.

Pamoja na fununu hizo, lakini pia habari za uhakika zinasema hata mipango ya kuwasiliana na Interpol zimekuwa zinafanywa na watu wawili tu, ukimwondoa Hosea.

Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma, Rais Kikwete alisema timu ilikuwa imekusanya Sh 53,738,835,392

Aidha Rais Kikwete alisema timu hiyo pia iliwabana baadhi ya watuhumiwa na kwamba wapo ambao wamekubaliana mpaka hadi Oktoba 31 mwaka huu wawe wameshalipa.

Hali hiyo inaonyesha kuwa tayari kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na Takukuru kwa kushirikiana na vyombo vingine ilikuwa imekamilika na kwamba mpaka hapo timu ilipofikia wanaweza kufanya kazi bila Takukuru.
Source: Mwananchi
 
Hivi vichwa vya habari ni special kuuza magazeti, title inavutia na conclusion inaonyesha there was no anything bad for TAKUKURU kuondolewa! lakini katika paragraph za mwanzo mwandishi anakuwa kama eti hajui reasons za TAKUKURU kuondolewa. Mbaya zaidi inaonekana eti tuamini labda Kikwete amewaondoa TAKUKURU!

Tutasema vingi au mengi ya kujipa moyo, mata BOT mafisadi wamechukuliwa hatua, Mara Mabadiliko makubwa yatakuja TAKUKURU mara hoo, watapelekwa mahakamani.Enyi watanzania mdanganywao nani atawaaminisha kuwa hakuna kitu chema kitakacholetwa na huyu RAIS? everything he does is just to magnetize society.

Waberoya

'Stand still'
 
Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA
Na Mwandishi wetu

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeengiliwa kwa agizo ‘kutoka juu’.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali ngazi ya juu
kunatokana na mchango wa tasisi anayoiwakili mjumbe huyo kuonekana mdogo.

Taarifa za ndani ya serikali zinaonyesha kuwa Takukuru wameondoshwa katika timu iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, Said Mwema pamoja na Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea.

“Kimsingi ni kama Takukuru iliondoshwa katika mchakato huu katika hatua za mwisho, wakati timu ilikuwa inaandaa ripoti kwa ajili ya kuifikisha kwa Rais kama ilivyokuwa imeelekezwa,” kilisema chanzo chetu.

Aidha chanzo hicho kilisema
kitendo cha kuondoshwa kwa taasisi hiyo nyeti pengine inatokana na kazi za msingi za kamati hiyo kumalizika na kubakia majukumu ya kuwapeleka watuhumiwa mahakamani pamoja na kuwafuatilia walioficha mali nje ya nchi.

Chanzo chetu kinasema
lengo kubwa la kuwahusisha Takukuru ilikuwa ni kutumia uwezo wao wa kiuchunguzi kuisaidia timu hiyo kuharakisha mambo zaidi.

Habari zilizopatikana
zinaeleza kuwa huenda Takukuru wameondolewa katika timu hiyo kutokana na kuvuja kwa kazi iliyokuwa ikifanyika.

“Baadhi ya siri za timu hiyo ilikuwa inaoongozwa na mwanasheria mkuu wa serikali zilikuwa zinavuja kila baada ya kikao, hivyo kuipa timu wakati mgumu wa kuendelea na kazi waliyopewa,” alisema.

Pamoja na fununu hizo, lakini pia habari za uhakika zinasema hata mipango ya kuwasiliana na Interpol zimekuwa zinafanywa na watu wawili tu, ukimwondoa Hosea.

Source: Mwananchi

Ukiwa na crummy press kama hii lazima utaelekea kujenga Taifa la wajinga kwa sababu hakuna anaejua chochote kinachoendelea, hakuna press.
 
Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA
Na Mwandishi wetu

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeengiliwa kwa agizo ‘kutoka juu’.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali ngazi ya juu kunatokana na mchango wa tasisi anayoiwakili mjumbe huyo kuonekana mdogo.

Taarifa za ndani ya serikali zinaonyesha kuwa Takukuru wameondoshwa katika timu iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, Said Mwema pamoja na Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea.

“Kimsingi ni kama Takukuru iliondoshwa katika mchakato huu katika hatua za mwisho, wakati timu ilikuwa inaandaa ripoti kwa ajili ya kuifikisha kwa Rais kama ilivyokuwa imeelekezwa,” kilisema chanzo chetu.

Maelezo hayo hapo juu yanataka kuonyesha kwamba TAKUKURU hawahusishwi tena kwa kukiuka kiapo ama kuharibu uchunguzi, ama kutokubaliana na uchunguzi unaoendelea au kutokana na hatua ambazo pengine zinaandaliwa kuchukuliwa dhidi ya Dk. Edward Hosea. Hii inataka kuonyesha kwamba Hosea ni mhalifu kuliko hata Elisifa Ngowi ambaye amehusika moja kwa moja katika EPA na maskandali mengine ikiwa ni pamoja na "kumchuna" mamilioni Marehemu Daudi Ballali na wengine kwa kutumia vitisho na ulaghai akitumia kuwapo kwake TISS. Maelezo hayo yanataka kutulazimisha tuone sasa serikali iko makini na inawachukulia hatua watendaji wasio waadilifu.

TAARIFA ZA KUONDOLEWA TAKUKURU NA YOTE KATIKA AYA HIZO KWA MAONI YANGU NI UPOTOSHAJI WA HALI YA JUU NA WENYE LENGO LA KUTUZUGA. WAKAMATWE WAHUSIKA NA KUPELEKWA MAHAKAMANI.

Aidha chanzo hicho kilisema kitendo cha kuondoshwa kwa taasisi hiyo nyeti pengine inatokana na kazi za msingi za kamati hiyo kumalizika na kubakia majukumu ya kuwapeleka watuhumiwa mahakamani pamoja na kuwafuatilia walioficha mali nje ya nchi.

Chanzo chetu kinasema lengo kubwa la kuwahusisha Takukuru ilikuwa ni kutumia uwezo wao wa kiuchunguzi kuisaidia timu hiyo kuharakisha mambo zaidi.

Kama kazi ya TAKUKURU kiuchunguzi imekwisha basi kazi iliyobaki ni ya DPP kupeleka mahakamani na kwa upande mwingine kwa polisi kuwasiliana na polisi wa kimataifa, lakini TAKUKURU pia wana mahusiano kiutendaji na taasisi kama hizo za kimataifa kama vile za Uingereza na Uswisi pamoja na India ambazo zina uwezo wa kufuatilia mali na nyendo za wahusika wa EPA na kwa kuwa kazi za kiuchunguzi huwa hazina ukomo, huwezi kuwaambia wachunguzi wa TAKUKURU basi wafungashe virago, hiyo pia si kweli. Pia kuna taarifa za uhakika kwamba ni TAKUKURU pekee waliomhoji Marehemu Ballali kabla hajakwenda Marekani na ni TAKUKURU pekee wanaojua siri ya Kagoda kwa kuwa walichukua doc za CRDB zinazowahusisha vigogo halisi (si Halisi mimi) ambao wanahusika na kampuni ya Kagoda Agricultural kwa hiyo wachunguzi hao bado ni muhimu katika kukamilisha na hatimaye kusimamia ama kuwa mashahidi katika mashitaka dhidi ya wahusika kwa hiyo haiingii akilini kwamba wameenguliwa. HAINA MAANA KABISA.

MAONI YANGU: Kwa maoni yangu ni kwamba naweza kuamini kwamba sasa huyo mtu wa JUU aliyetoa maelezo, amefanya uamuzi wa kuwasamehe kabisa watuhumiwa wa EPA tena baada ya kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM kule Dodoma. Hiyo inaweza kuingia akilini na pengine NDIO UKWELI.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa huenda Takukuru wameondolewa katika timu hiyo kutokana na kuvuja kwa kazi iliyokuwa ikifanyika.

“Baadhi ya siri za timu hiyo ilikuwa inaoongozwa na mwanasheria mkuu wa serikali zilikuwa zinavuja kila baada ya kikao, hivyo kuipa timu wakati mgumu wa kuendelea na kazi waliyopewa,” alisema.

Hii tena ni mbinu chafu tena zinazolenga kuwaingiza ama kuwatuhumu moja kwa moja TAKUKURU kuwa wanatoa siri na mwandishi kwa udhaifu wakeanatumika kutishia mbubujiko wa habari. Pia habari hii imetokea ndani ya TAKUKURU ukiwa ni ule muendelezo wa mapambano ya kutaka kumuondoa HOSEA na kwa hakika ni katika kuvuruga ushahidi wa EPA na ule wa Ballali ambao TAKUKURU ni taasisi pekee iliyo na ushahidi na maelezo ya kisheria kwani hata timu ya Mwanyika haijaweza kumhoji Ballali na hawajapata nyaraka zote za Kagoda wakati TAKUKURU walizipata hata kabla ya wakaguzi wa kwaza wa Deloite kugundua siri za wizi wa EPA.

Pamoja na fununu hizo, lakini pia habari za uhakika zinasema hata mipango ya kuwasiliana na Interpol zimekuwa zinafanywa na watu wawili tu, ukimwondoa Hosea.

Mwandishi anatuambia 'watu' wawili, anataka kutuambia Mwanyika na Saidi Mwema, jambo ambalo si kweli. Kwanza hata katika timu ya Mwanyika, kiutendaji Mwanyika na Mwema hawakuwa wanafanya kazi wao moja kwa moja. Kazi zilikuwa zinafanywa na kina Manumba, Kasala, Ubisimbali, Samali, Huseni, Valentino, Kisai na wengineo kwa upande wa polisi na kwa upande wa Mwanyika (sheria) kazi kubwa ilikuwa ikifanywa na vijana wake akiwamo DPP Feleshi na timu yake kwa hiyo hata mawasiliano ya kimataifa yanafanywa kitengo cha polisi wa kimataifa na TAKUKURU hata Hosea hakuwa anafanya kazi zote pamoja na kuwa kama mwanasheria na mchunguzi alikuwa akifanya sehemu ya kazi mwenyewe kama ilivyo kwa Saidi Mwema kwa baadhi ya upangaji na utekelezaji wa mikakati ya kazi za kikachero.

Waandishi na Wana JF siku zi nyingi tuanza kujiandaa na UZUGAJI MKUBWA kuhusu EPA na kesi kibao za UFISADI
 
Jamani tuweni serious kidogo na vitu tunavyovileta umu.....hivi vingine tutavisoma tu kwenye magazeti au hata kwenye website za hayo magazeti..kuleta humu habari kama hii ni maudhii sasa...
 
Ni kweli ni maudhi, lakini nadhani wanaoudhika wachangie ili wajue HATUZUGIKI
 
Hiyo hatujali kwani ni kujisafisha staili na time will tell. Msijali tunawasha moto wakibanika wanakulana wenyewe. Ndio mbinu tunayotaka kutumia sasa hivi.
 
Kampeni za Uchaguzi zinaanza mwishoni mwa mwaka ujao,ili Muungwana amalize ngwe yake ,tapiga danadana mpaka 2010 ,hapo ndio tutafahamu alikuwa anaenda kufanya nini marekani kila siku.
 
Back
Top Bottom