TAKUKURU wakanusha habari ya Musiba, ni baada ya wao kuguswa

Mbwa ukicheka nae atakufuata hadi msikitini,ni wakati wa mavuno,bado mfuga mbwa siku akiishiwa chakula nae atavuna mapando.
 
Mr funeral ni untouchable loudspeaker si waziri IGP, cdf,kange anybody anaweza mtachi,kanuni ya kutafuna usema hivi,wakishamaliza kuwatafuna wengine wataanza tafunana wenyewe.
 
Hapa kuna mchezo wa sanaa.
1. Chombu makini kama hiki hakiwezi kutaja majina ya watuhumiwa au wachunguzi/ waendesha mashitaka hadharani, ingetafuuta namna nyingine ya kuwazungumzia... Kueleza majukumu yao unahatarisha maisha yao au ndugu zao.

2. Chombo makini kama hiki huwezi kutuhumiwa kiasi hiki ukaishia kumwandikia Mhariri bila kumshitaki mahakamani.
 
Kuanzia uchaguzi wa 2010 rushwa imekuwa agenda kubwa. Mkurugenzi wa Takukuru alipoondolewa haraka haraka baada ya uchaguzi wa 2015 binafsi niliamini hatimaye vita dhidi ya rushwa ilikuwa inapata utashi wa kisiasa. Kwambà pengine viongozi wetu wapya waliamini Mkurugenzi yule hakuwa na kasi ya kutosha! Muda siyo mrefu tangu wakati huo nilibadili mtazamo; nadhani nilikuwa nimekosea kwani kwa maoni yangu kasi ya kupambana na rushwa imepungua. TAKUKURU imepooza sana. Ninavyoona mimi ni kama TAKUKURU haipo huru tena kufanya kazi zake kwa weledi. Badala yake tumeona mara kadhaa TAKUKURU ikicharuka baada ya kupokea maagizo. Ndipo nikaanza kuamini kuwa Mkurugenzi yule hakuondolewa kwa sababu ya utendaji hafifu bali hatua ile ilikuwa sehemu ya mkakati wa kuifanya TAKUKURU chombo cha serikali kinachofanya kazi kwa maelekezo na udhibiti wa serikali. Sababu mojaeapo ya kufanya hivyo ni kuwa rushwa kubwa kubwa hapa nchini mara nyingi kama siyo zote, huhusisha wanasiasa. Kuanzia hapo Wakurugenzi wa Takukuru wamekuwa askari kwani hao ndio wepesi kupokea maagizo na maelekezo bila kujali sheria za nchi wala JD yake. Mkurugenzi aliyeondolewa alipata kuripotiwa kutoridhika na kuingiliwa na wanasiasa katika majukumu yake.
 
Asante kwa ufafanuzi huo mrua - Mungu atawashindia dhidi ya hujuma zinazofanywa na wasiopenda maendeleo
 
Hapa kuna mchezo wa sanaa.
1. Chombu makini kama hiki hakiwezi kutaja majina ya watuhumiwa au wachunguzi/ waendesha mashitaka hadharani, ingetafuuta namna nyingine ya kuwazungumzia... Kueleza majukumu yao unahatarisha maisha yao au ndugu zao.

2. Chombo makini kama hiki huwezi kutuhumiwa kiasi hiki ukaishia kumwandikia Mhariri bila kumshitaki mahakamani.
Kama kweli Musiba ameweza kupata mpaka majina ya wafanyakazi wa TAKUKURU na kesi zao ina maana ana inside information, yule mjamaa simpendi kabisa ila kwa hili nahisi kama kuna kaukweli maali
 
Kwanini musimpeleke mahakamani kama hizi tuhuma hazina ukweli, musipofungua kesi dhidi yake basi ni wazi rusha ipo hapo takukuru.
 
Brigedia Jenerali mtaongeza heshima mkiachana na kujiingiza kwenye siasa. Inakera mnapoonekana waziwazi kutumika kisiasa. Mnatakiwa kuwa juu ya siasa na mtende siyo kwa uwazi tu bali kwa haki.
 
Waliokuwa wanamlea wameanza kufikiwa na bado atafikiwa hadi anayemtuma.

Namuomba Musiba aendelee hivyo hivyo baada ya Takukuru ainge ndani ya Jeshi la polisi kuna rushwa ya kufa mtu mle, akitoka mle alimlike JWTZ halafu amalizie ikulu. Tutaelewana tu.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JUNI 17, 2019

KUKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZENYE TUHUMA DHIDI YA MAAFISA WA TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zilizochapishwa katika magazeti mawili ya leo Juni 17, 2019. Taarifa hizo zimechapwa katika gazeti la FAHARI YETU toleo Na 163 la Jumatatu Juni 17, 2019 ukurasa wa kwanza ikiwa na kichwa cha habari VIRUSI WA RUSHWA NDANI YA TAKUKURU HAWA HAPA' pamoja na Gazeti la TANZANITE Toleo Naa 478 la Jumatatu Juni 17, 2019 ukurasa wa kwanza ikiwa na kichwa cha habari I MTANDAO HATARI WA RUSHWA NDANI YA TAKUKURU WABAINIKA'.

Tunapenda kuufahamisha umma kwamba taarifa hizi ambazo zimeandikwa kwa kufanana katika magazeti yote mawilt NI ZA UPOTOSHAJI WENYE LE-NGO LA KUDHOOFISHA UTE-NDAJI KAZI WA TAKUKURU hasa katika kipindi hiki cha mapambano na Wakwepa Kodi, Wabadhirifu wa mali za umma pamoja na Wahujumu wa Uchumi.

TAKUKURU inafahamu fika kwamba ipo vitani na kwamba kadri tunavyoongeza kasi ya mapambano ndivyo vivo hivyo ambavyo WALARUSHWA pamoja na wanaonufaika na vitendo vya rushwa wanaendelea kutafuta mbinu za kudhoofisha mapambano dhidi ya rushwa na kuwakatisha tama watumishi wa TAKUKURU

Tunapenda kuuhakikishia umma kwamba TAKUKURU ipo imara na itaendelea kuwafichua na kuwashughulikia kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nan 11 ya Mwaka 2007, wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa bila ya kujali cheo, wadhifa, jinsia wala itikadi.
Katika taarifa hii imeelezwa kwamba ndani ya TAKUKURU kuna 'mtandao wa wala rushwa' na kuainishwa tuhuma mbalimbali dhidi ya wafuatao:

VICK MARANDU:
Anatuhumiwa kukwamisha uchunguzi dhidi ya Habinder Seth na James Rugemalira na kusababisha uchunguzi huo kutokamilika:

UFAFANUZI:
Tunautaarifu umma kwamba mtumishi tajwa hajawahi kuhusika katika kuchunguza kesi iliyohusisha washitakiwa tajwa hapo juu wala kushiriki katika timu ya uchunguzi wa kesi hii.

KesÎ inayowahusisha washitakiwa tajwa hapo juu kwa sasa ipo mahakamania
Kesi hii ni Kesi ya Uhujumu Uchumi Nau 27/2016

KASIMIJ EFREM
Anatuhumiwa kupata fedha kutoka kwa watuhumiwa watano (5) wanaotuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi kupitia matumizi ya 'EFD Machines' na kuwatumia 'MAWAKALA' Colman Lubisi na Zameen Murji kupokea fedhaa

UFAFANUZI:
Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa tajwa ulifanyika na kukamilika.
Kutokana na uchunguzi huu Kesi Kubwa nne (4) zimefunguliwa katika MAHAKAMA KUIJ DIVESHENI YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI maarufu kama Mahakama ya MAFISADI.

, Kesi hizo ni ECO Na. 2/2019; Na. 3/2019', Na. 4/2019; na Na 8/2019. Kesi nyingÎne ECO Na. 7/2019 washitakiwa wameshasomewa mashitaka kwa ajili ya kufikishwa katika Mahakama Kuua
Colman Lubisi SI WAKALA bali ni mtumishi wa TAKUKURU aliyehusika katika uchunguzi wa tuhuma hizi na hivi leo yupo katika Mahakama ya Mafisadi akitoa ushahidi dhidi ya kesi mojawapo (ECO Na. 3/2019) dhidi ya washitakiwa tajwa.

(iii) KASOMAMBUTO MBENGWA
Huyu si mtumishi wa TAKUKURU tangu Januari 2019.

RICHARD MPUNGU NA MR MAEMBE
Hawa wanatuhumiwa kupoteza faili la kesi ya Ngorongoro Crater.

UFAFANUZI:
Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii ulifanyika na kukamilika
• Kesi ilifunguliwa katika Mahakama ya Arusha - Sekei
• Namba ya Kesi ilikuwa EC Na. 71/2015.
• Kesi hii ilishatolewa hukumu ambapo Mshitakiwa alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu (3) jela.

(v) MR MAKALE
Huyu si mtumishi wa TAKUKURU tangu Januari 2019.

OMARM NZARO
Anatuhumiwa kuwa na ukwasi wa kutisha
UFAFANUZI:
Tunaomba ushirikiano katika kufahamu mali zinazodaiwa kuwa za mtumishi huyu kwa majina bandia

(vii) NAKEMBEWVA
Huyu si mtumishi wa TAKUKURU tangu januari 2019.

(viii) LEONARD SWAI
Anatuhumiwa kukwamisha kesi za watu wenye fedha

UFAFANUZI:
Huyu ni Mwanasheria aliyesimamia chunguzi za kesi zinazotajwa katika taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti ambazo kwa sasa zipo katika Mahakama ya Mafisadi Vilevile ndiye Mwanasheria aliyekuwa akiendesha kesi hizo tano (5) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi KISUTU zilizoainishwa katika hayo magazeti kabla ya kesi hizo kufikishwa katika Mahakama ya Mafisadi.

Leonard Swai ndiye aliyeendesha kesi nyingine zilizowatia hatiani washitakiwa katika kesi ya Jinai Naa 121/2013 — Jamhuri VS Togolani Kimweri iliyohusu jengo la ghorofa
29. Kesi ya Ardhi pamoja na Kesi ya matumizi ya Mitandao.

(ix) MOHAMED MSANGI
TAKIJKURU haijawahi kuwa na mtumishi kwa jina tajwa.
Vilevile, tunapenda kuujulisha umma kwamba, wiki iliyopita TAKUKURU imewakamata matapeli wanaofanya utapeli kwa kutumia majina ya watumishi wa TAKIJKURU.

Katika uchunguzi huu tumewakuta na SARE ZA JESHI LA POLİSİ, FEDHA BANDIA, VİTAMBULISHO BANDIA pamoja na nyara mbalimbali za Serikali. Taratibu za kuwafikisha mahakamani zinakamilishwa. Matapeli hawa pia wamekamatwa wakiwa na laini mbalimbali za makampuni tofauti ya simu wanazozitumia kufanya utapeli.
Kwa ufafanuzi tajwa hapo juu, umma utagundua kwamba taarifa hizi ni za UPOTOSHAJI zilizoandikwa na wasio na mapenzi mema na Taifa letu. Mtoa taarifa hii amekosa UZALENDO na kutaka kuleta matokeo HASI ya mapambano dhidi ya wala rushwa na mafısadi, yanayoongozwa na Jemedari wetu Mheı Rais wa Serikali ya Avvamu ya Tano - Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,

Kwa taarifa hii tunapenda kuukumbusha umma kwamba uchunguzi unaofanywa na TAKUKURU haufanywi na mtu mmoja bali ni timu ya wachunguzi. Pia tunawakumbusha Watanzania kuwa TAKUKURU ipo wazi muda wote kupokea taarifa za malalamiko dhidi ya watumishi wake kwani hakuna aliye juu ya sheria na mtumishi yeyote anayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa huchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufıkishwa mahakamani kama ambavyo kwa sasa kuna kesi mbili zinazoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Hata hivyo, tayari tumemuandikia barua Mhariri Mtendaji wa magazeti husika ili atupatie ushahidi utakaoweza kuthibitisha tuhuma hizi.

Tunaujulisha umma pia kwamba TAKUKURU ina ofisi katika kila Mkoa na kila Wilaya. Vilevile mtoa taarifa anaweza kuwasiliana nasi BURE kupitia simu za kiganjani kwa mitandao yote kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS); kwa kupiga simu au kwa kubonyeza * 113 # na kufuata maelekezo.

TAKUKURU inaendelea kuwashukuru wale wote wanaoendelea kutupatia taarifa pamoja na ushirikiano katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini ambayo TAKUKURU imepewa dhamana na Watanzania ili kuyaongoza mapambano hayo kwa mujibu wa Sheria.

Tuliahidi na tunaendelea kuwaahidi Watanzania kwamba tutatekeleza wajibu wetu KWA HAKI BILA YA UPENDELEO WALA KUMWONEA MTU.

IMETOLEWA NA:
Brigedia Jenerali JOHN MBUNGO
NAIBU MKURUGENZI MKUU
TAKUKURU
17.612019


View attachment 1130237
View attachment 1130238
View attachment 1130238
View attachment 1130240
View attachment 1130239
View attachment 1130241
View attachment 1130242
Sijasikia Tuhuma za Musiba lakini kwa majibu haya, ni wazi kwamba MUsiba yuko na taarifa nzuri sana za watu wa TAKUKURU. Bahati mbaya anayemjibu Musiba hakutumia njia sahihi. Njia nzuri ilikuwa ni kukubaliana na Musiba na kusema wazi kinachoenedelea.

Kuhusu ulajirushwa na lengo la TAKUKURU, TAKUKURU lazima ijipime. Vijana wake kama walivyo TRA hawana mfano mzuri wa mafanikio kwa juhudi zaidi ya Rushwa. Walio juu yao wote wamefanikiwa kujenga na maisha mazuri kwa kutumia ofisi zao kintume na malengo. Hii ni tabia ya siku nyingi. Vijana hawa wanakula rushwa na mara nyingi kesi za uchunguzi zinazimwa kwa rushwa.

btw. TAKUKURU tuambieni mke wa boss wenu wa zamani akiitwa Ntukamazina aliishia wapi na mishahara ya waalimu. Mke huyu alikuwa mtumishi wa hazina na ndiye alisem,ekana kutafuna malipa ya waalimu yaliyodumu kwa miaka yote ya nyuma. Mashitaka yake yalifika wapi, na hasa kwa kumtumia mumewe akiwa boss TAKUKURU?
 
Hapa kuna mchezo wa sanaa.
1. Chombu makini kama hiki hakiwezi kutaja majina ya watuhumiwa au wachunguzi/ waendesha mashitaka hadharani, ingetafuuta namna nyingine ya kuwazungumzia... Kueleza majukumu yao unahatarisha maisha yao au ndugu zao.

2. Chombo makini kama hiki huwezi kutuhumiwa kiasi hiki ukaishia kumwandikia Mhariri bila kumshitaki mahakamani.
Hats mimi nimeshangaa.
 
IMG-20190618-WA0046.jpeg
 
Back
Top Bottom