TAKUKURU kujenga jengo la millioni 900 Karatu ina maanisha nini?

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Jana kwenye taarifa ya habari nilimuona Dr. Hosea wa TAKUKURU akifungua jengo huko Karatu (sikumbuki vizuri) la thamani ya millioni 900 na kuahidi kujenga mengine matatu sijui wapi. Picha ya haraka niliyoipata ni kuwa kumbe rushwa haitakaa iishe, inabidi ijengewe maofisi mengi tu nchini. Hii ina maanisha kuwa mafisadi wataendelea kuwepo muda wote bila mabadiliko? Ningekuwa kiongozi ningerudisha AZIMIO LA ARUSHA hata kesho, tena lifundishwe mashuleni kuanzia chekechea. Yani nchi imekosa maadili namna hii jamani?
 
Ina maanisha wanataka kupambana na rushwa, na kama jengo limekamilika ina maana wakazi wa Karatu watapata ongezeko la viji ajira from admin workers, watu wa kupambana na rushwa, au hata watunzanji wa hilo jengo hizo ni faida zake na kwingine watapojenga zitaenda faida hizo hizo zitazofaidisha jamii. Na kama watafanya kazi vizuri hao TAKUKURU itasaidia kwenye kuongeza pato la taifa.

Au mwenzetu unafikiria in terms of majembe tu na kulima, Azimio la Arusha la nini in the this century.
 
Jana kwenye taarifa ya habari nilimuona Dr. Hosea wa TAKUKURU akifungua jengo huko Karatu (sikumbuki vizuri) la thamani ya millioni 900 na kuahidi kujenga mengine matatu sijui wapi. Picha ya haraka niliyoipata ni kuwa kumbe rushwa haitakaa iishe, inabidi ijengewe maofisi mengi tu nchini. Hii ina maanisha kuwa mafisadi wataendelea kuwepo muda wote bila mabadiliko? Ningekuwa kiongozi ningerudisha AZIMIO LA ARUSHA hata kesho, tena lifundishwe mashuleni kuanzia chekechea. Yani nchi imekosa maadili namna hii jamani?
Poor thread.
 
Poor thread.

Rushwa ni zoezi la kudumu Tanzania ingawa kuna TAKUKURU kama Taasisi ya kuzuia na inavyoonekana kama kunajengwa majengo ya kudumu basi na rushwa kumbe ni zoezi la kudumu ambalo halitazuilika.
 
Back
Top Bottom