Taifa Stars yafuzu AFCON, kutwaa milioni 500 za Rais Samia

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Na Mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi ya Shilingi milioni 500 aliyotoa kwa Timu ya Taifa Stars ikifuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo Septemba 7, 2023 nchini Algeria, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo, amewapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuwa safari ya matokeo hayo haikuwa nyepesi hadi dakika ya mwisho.

“Kwa niaba ya Serikali, Mhe. Rais, Mhe. Waziri pamoja na wadau wote, tumekuja hapa kuongeza hamasa. Kubwa mtakumbuka wakati wa kujiandaa na mechi ya Uganda kule nyumbani Mhe. Rais alitoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 500, timu ikifuzu. Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, zimekwisha letwa Wizarani kwa ajili yenu” amesisitiza Katibu Mkuu Bw. Yakubu.

Timu ya Tanzania, Taifa Stars imefuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kutoka sare ya bila kufungana (0-0) na Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F uliochezwa katika Uwanja wa May 19, nchini Algeria.

Taifa Stars ikiwa na alama 8 imeungana na Algeria yenye alama 16 katika kundi hilo kushiriki mashindano ya AFCON yatakayofanyika Ivory Coast na kuziacha nje ya mashindano hayo timu za Uganda waliomaliaza na alama 7 na Niger waliomaliza na alama 2 huku Tanzania ikishiriki mashindano ya AFCON kwa mara ya tatu kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.

IMG-20230908-WA0172.jpg
 
Mil.500 hapana aisee.

Hiyo pesa inapeleka mradi wa Maji kwa.watu zaidi ya elfu 5

Inajenga Kituo Cha Afya

Inajenga shule Mpya kabisa ya msingi au ya Sekondari

Inajenga km 1 ya lami za Tarura

Inatosha kuweka taa za barabarani km 3

This is too much,pesa ni nyingi sana walau ingekuwa mil.100
Tuliza kwato zako,
Wewe siyo Samia,kama zimekuuma toa wewe 1m kama una jeuri
 
Mil.500 hapana aisee.

Hiyo pesa inapeleka mradi wa Maji kwa.watu zaidi ya elfu 5

Inajenga Kituo Cha Afya

Inajenga shule Mpya kabisa ya msingi au ya Sekondari

Inajenga km 1 ya lami za Tarura

Inatosha kuweka taa za barabarani km 3

This is too much,pesa ni nyingi sana walau ingekuwa mil.100
nchi ya ajabu sana, vitu vya kijinga ndiyo vinapewa kipaumbele
 
Mil.500 hapana aisee.

Hiyo pesa inapeleka mradi wa Maji kwa.watu zaidi ya elfu 5

Inajenga Kituo Cha Afya

Inajenga shule Mpya kabisa ya msingi au ya Sekondari

Inajenga km 1 ya lami za Tarura

Inatosha kuweka taa za barabarani km 3

This is too much,pesa ni nyingi sana walau ingekuwa mil.100
Hata hivyo,bado wachezaji kwa Taifa Stars wanahitajika.Wakuhifadhie namba ngapi mkuu?
TAHADHARI:Kuna baadhi ya wachezaji duniani wamewahi kupoteza na uhai wao wakiwa wanacheza football.
 
Na Mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi ya Shilingi milioni 500 aliyotoa kwa Timu ya Taifa Stars ikifuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo Septemba 7, 2023 nchini Algeria, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo, amewapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuwa safari ya matokeo hayo haikuwa nyepesi hadi dakika ya mwisho.

“Kwa niaba ya Serikali, Mhe. Rais, Mhe. Waziri pamoja na wadau wote, tumekuja hapa kuongeza hamasa. Kubwa mtakumbuka wakati wa kujiandaa na mechi ya Uganda kule nyumbani Mhe. Rais alitoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 500, timu ikifuzu. Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, zimekwisha letwa Wizarani kwa ajili yenu” amesisitiza Katibu Mkuu Bw. Yakubu.

Timu ya Tanzania, Taifa Stars imefuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kutoka sare ya bila kufungana (0-0) na Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F uliochezwa katika Uwanja wa May 19, nchini Algeria.

Taifa Stars ikiwa na alama 8 imeungana na Algeria yenye alama 16 katika kundi hilo kushiriki mashindano ya AFCON yatakayofanyika Ivory Coast na kuziacha nje ya mashindano hayo timu za Uganda waliomaliaza na alama 7 na Niger waliomaliza na alama 2 huku Tanzania ikishiriki mashindano ya AFCON kwa mara ya tatu kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.View attachment 2743121View attachment 2743120View attachment 2743123View attachment 2743122
Tuna Rais dhaifu mno. Hekima yake iko chini sana. Tuendelee kumwombea kwa Bwana Yesu Kristo, mwana na Mungu aliye hai.
 
Back
Top Bottom