Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
Kitendo cha Raisi Mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi BMW kusema uongo mbele ya jamii ya watanzania haimshushi yeye tu heshima bali inadhalilisha cheo kizima cha uraisi na utu uzima alio nao. Maraisi waliostaafu kwenye nchi nyingi duniani huwa ni walezi wa Taifa husika, hujiepusha na uzushi na uongo na kuegemea kwenye hekima na kujenga taifa moja lenye utu na mshikamano wa kitaifa.
Wasi wasi unaoonyeshwa na familia ya Nyerere ya kifo cha baba yao inatia wasi wasi kama kweli maradhi aliyokuwa nayo Nyerere ndio yaliyompeleka kwenye haki au walimuwahisha kwa tamaa ya mali na utukufu wa hapa duniani.
Ila yote haya ni mwanzo wa taifa huru na la wakweli, tunakwenda kuwajibika kwa maneno yetu na matendo yetu. Na laani kwa viongozi wote wa kitaifa kutumia lugha za uongo, udhalilishaji na maudhi ili tu kusaidia mtu kwenda dodoma. Dodoma sio sehemu ya kupeleaka kila mtu inabidi kama taifa tujue nini tunataka. Mkapa ametia aibu na anapaswa kujua hilo.