Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

snipers

Senior Member
Feb 29, 2016
119
178
Juzi nimeenda Mlimani City kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa Mary Brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na ya kwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!

Mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mimi simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu.

Nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu. Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
 
Miss natafuta kinachonishangaza kwa jinsi alivyo mrembo hata kama atakuwa na vyeti feki akienda kuomba kazi ofisini kwa mwanaume yoyote rijali atapata tu. Kwa nini anaamua kufanya kazi ile?
TATIZO NA NYIE MKIOMBWA SMARTPHONE KIDIPLOMASIA HAMTOI MDADA KACHOKA VITOCHI
BABY BABY HAIJAZAA MATUNDA
 
Siku hizi wadada wanatumiwa sana kwa wizi kwa sababu ya udhaifu wao hinyo huwa tunawahurumia na ndipo wanapata nafasi

Ni somo zuri umelitoa hapo watu wawe makini
 
Back
Top Bottom