n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,006
- 2,667
Wakuu hali ya hewa inasomeka kitahadhari zaidi.
Kuna tishio la ongezeko la mvua muda mchache ujao.... soma taarifa ya Hali ya Hewa hapo chini
Kuna tishio la ongezeko la mvua muda mchache ujao.... soma taarifa ya Hali ya Hewa hapo chini
View attachment TAHADHARI _31-10-2012.pdfJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Simu pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 Imetolewa: 31 Oktoba, 2012
TAARIFA YA ONGEZEKO LA MVUA
Imetolewa na
Taarifa Na. 20121031-01 Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 10:30 Alasiri Daraja la Taarifa:
1:Taarifa 2:Ushauri
3:Tahadhari
4:Tahadhari Kubwa:
Taarifa Aina ya Tukio
Linalotarajiwa
Ongezeko la mvua Eneo Katika baadhi maeneo ya mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga,
Geita,Simiyu, Singida, Dodoma, Rukwa, Tabora, Njombe, Iringa na
Mbeya
Maelezo Katika kipindi cha siku mbili zijazo (1-2/11/2012) kunatarajiwa
kuwa na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa
tajwa hapo juu. Hali hii inatokana na kuwepo kwa viashiria vya
ongezeko la unyevunyevu angani sambamba na kuwepo kwa
makutano ya upepo katika maeneo hayo.
Maelezo ya ziada Hii ni taarifa ya awali, Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea
kufuatilia mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa na itatoa taarifa
zaidi kwa kadri zitakavyo patikana
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA