JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,032
Posted by John Mnyika | May 13, 2012
WanaJF wenzangu, katika kipindi cha kati ya 2011 mpaka 2012 kuna mwelekeo ambao naona ni vyema kila unapoibuka mkauchukulia kwa tahadhari. Kwa nyakati mbalimbali kila ninaposhughulikia masuala ya kitaifa yenye kuwagusa baadhi ya watu ndani ya serikali au CCM huanza vita vya mtandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhoji kuhusu utendaji kazi wangu jimboni sanjari na utekelezaji wa ahadi za kampeni.
Watu hawa hawahoji ahadi za Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alizozitoa jimboni Ubungo mwaka 2005 na zingine zaidi akazitoa 2010; natambua kuwa wanao uhuru wa kuacha kuhoji ahadi hizo kwa sababu wanazozijua wao na kuhoji ahadi zangu nilizoahidi za kuwawakilisha wananchi, kuisimamia serikali na kushiriki kikimilifu katika kutunga sheria zote zikiwa na lengo la kuwezesha maendeleo.
Hata hivyo katika kutumia uhuru wao huo wa kikatiba ni vizuri pia wakatimiza wajibu wa kufuatilia utekelezaji tunaousimamia kwa kuzingatia kuwa toka nichaguliwe nimekuwa na kawaida ya kutoa mrejesho wa hatua kwa hatua wa kazi ambazo nazifanya za kuwatumikia wananchi jimboni, hivyo ni vizuri rejea ikafanyika katika taarifa hizo na kama kuna maswali ya ziada nipo tayari kuyajibu kwa kila nitakapopata wasaa.
Kwa ajili ya urahisi wa rejea na kutokana na maswali ambayo hujirudia kwa masuala ambayo tayari yameshatekelezwa na nimeshayatolea ufafanuzi kwa nyakati mbalimbali, nafanya utaratibu ili mwaka wa fedha 2011/2012 utakapoisha niweke utekelezaji wote kwenye ripoti moja ya mwaka iwe rahisi kwa rejea. Kwa sasa mnaweza kutembelea http://mnyika.blogspot.com (JOHN MNYIKA) upo mrejesho wa utekelezaji hatua kwa hatua kuhusu namna nilivyotimiza wajibu wa kuisimamia serikali katika kuwezesha maendeleo jimboni, mafanikio tuliyopata mpaka sasa, changamoto tunazokumbana nazo na namna tunavyoendelea kuzikabili.
Hatahivyo, naomba ieleweke kwamba uwepo wa mikakati ya propaganda kwenye mitandao na wakati mwingine hata kwenye baadhi ya vyombo vya habari hautanirudisha nyuma katika kushughulikia masuala ya kitaifa yenye maslahi ya umma. Izingatiwe pia kwa nafasi ya ubunge mliyonituma kuwawakilisha nina wajibu kwa taifa; hivyo sitaacha kuendelea kushughulikia matatizo ya kimfumo katika nchi yetu kwa hofu tu ya kuhojiwa kuhusu masuala ya jimbo. Izingatiwe pia nina nafasi ya uongozi katika chama ambayo inaniweka katika mstari wa mbele wa mapambano na wakati mwingine kupokea mashambulizi kutoka kwa wapinzani wetu.
Katika kipindi hiki pia cha kuelekea hukumu ya kesi ya uchaguzi tarehe 24 Mei 2012 tayari zimeanza propaganda kwenye mitandao ya kijamii lakini pia napata simu toka kwa wananchi na pia mrejesho toka kwa viongozi mbalimbali kwenye mikutano yetu jimboni kuhusu ujumbe ambao unasambazwa na makada wa CCM vijiweni.
Naendelea kuyatafakari masuala na matukio yote na nitazungumza wakati muafaka na hata ikibidi kuwataja wahusika kwa majina. Ujumbe wangu kwa wote mlioamua kunitangaza kuwa adui yenu rejeeni historia yangu ya harakati kabla ya kujiunga na siasa 1999 mpaka 2004, na kazi zangu za kisiasa 2005 mpaka 2010; mtanielewa vizuri zaidi. Kuvunja ofisi ya mbunge kuchukua vifaa na nyaraka au kutuma watu mliowatuma hakuwezi kunirudisha nyuma, badala yake mnanipa moyo zaidi wa kusonga mbele nikijua kwamba matokeo yameanza kuonekana.
Kwa wote ambao mnaniunga mkono kwa hali na mali; naendelea kuwashukuru, nimefika hapa nilipo kwa sababu yenu; kwa pamoja tumeshinda, kwa pamoja tutaendelea kushinda. Nimewaandikia mchukue tahadhari juu ya propaganda chafu, wakati mkiendelea na mijadala yenye tija kwa taifa. Endeleeni na uhuru wenu wa kutuhoji na kutukosoa, nami nitaendelea na wajibu wa kuwatumikia na pia kuwajibu kama sehemu ya kuwajibika; maslahi ya umma kwanza.

Last edited by a moderator: