Tahadhari juu ya Homa ya Manjano

Kagondo

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
296
79
Shirika la kimataifa la Save the Children limetahadharisha kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano katika nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Angola.

Pia imesemekana kuwa hivi karibuni unaweza kuenea katika nchi za mabara ya ulaya , Amerika na Asia.

Ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya aedes, wanaopatikana katika nchi nyingi za Afrika Magharibi.

Mwezi March mwaka huu baadhi ya vyombo vya habari nchini vilitahadharisha juu ya ugonjwa huu nchini Tanzania ikiwa ni hataua za kujihadhari, kwani kwa wakati huo taarifa za awali zilionesha kuwa, ugonjwa huo upo nchini Kenya na Angola.

Tahadhari hii inakuja kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuwa makini hasa wale wanaosafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine kwani UGONJWA HUU una KINGA PEKEE lakini HAUNA TIBA.

Vyanzo: Channel Ten March 21, 2016
Dira ya Dunia BBC Agosti 16, 2016.
 
kumbe congo na angola

Mwezi March mwaka huu baadhi ya vyombo vya habari nchini vilitahadharisha juu ya ugonjwa huu nchini Tanzania ikiwa ni hataua za kujihadhari, kwani kwa wakati huo taarifa za awali zilionesha kuwa, ugonjwa huo upo nchini Kenya na Angola.
 
Chajo zake zinapatikana wapi?
Sina hakika ila nahisi hospitalini,,,,,ila huwa naona wanazigawa kwenye mikusanyiko ya watu, mfano, mwezi wa nne waligawa kanisa flani hvi ,,,,,walikuwa wauguzi wa afya, japo sikuona kama walikuwa na mhamasisho sana
 
Back
Top Bottom