Tafakari!

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Japo sija fanya utafiti rasmi, kuna mtu kanielezea kitu juzi na mimi kwa kutafakari tu naamini ni ukweli.

Juzi tumekaa na mmoja wa marafiki zangu ambae kiumri ni mkubwa zaidi yangu. Akaniuliza MwanaFa hivi unadhani Tanzania mtu aliye soma kwa wastani anazaa watoto wangapi na kwa wastani asiye soma anazaa watoto wangapi?

Nilikua sija lifikiria hili ila nikamuambia kwa kuangalia wale walio nizunguuka naweza sema kwa haraka haraka kwamba aliye soma huwa na wastani wa watoto wawili au watatu na asiye soma ana kuwa na wastani wa watoto sita au saba.

Akaniambia uko sahihi hizo ndiyo rough figures. Akaniambia je una kubali kwamba mtoto wa aliye soma nae ana nafasi kubwa sana kuwa msomi kama mzazi/wazazi wake na yule mtoto wa asiye soma kuna asilimia kubwa na yeye asifike mbali kimasomo?

Nikamuambia tena ndiyo hiyo ni kweli kabisa. Hata sisi kwenye ukoo wetu wali ambao wazazi wao walifika juu kielimu wengi wao na wao walifika juu kielimu na wale ambao wazazi wao wali pata elimu wastani au ndogo wengi wao wakaishia hivyo hivyo.

Hapa tena akaniambia kwamba observation yangu ipo sahihi. Sasa basi aka niambia nitafakari. Akasema kwa kutokana na logic hiyo basi ina maana msomi ata toa wasomi wawili au watatu na asiye soma nae ata toa watoto sita au saba ambao nao wata kuwa si wasomi. Akasema huoni hapa taifa letu tuna produce wasomi wachache sana ukilinganisha na wale ambao hawata kuwa wasomi?

Hizi zote ni rough figures tu ambazo tumeelezeana kutokana na simple logic and observation. Nadhani hata nyie wenzangu hamtabisha kwenye hili. Sasa basi kama kwenye kila kizazi tuna toa wasomi wachache kuliko wasio sema hii tayari si mzunguuko mbaya? Je ndiyo maana taifa lina zidi kudidimia siku hadi siku kutokana na kulea kizazi kisicho soma?

Kama tuta kubali kwamba hili tatizo lipo basi kama bado hatuja fanya ili takiwa serikali ifanye official research. Ikisha jua kwamba kweli tatizo lipo na kwa kiasi gani basi hatua ya pili ni kutafuta njia za kuwezesha na kuencourage watoto wanao tokana na wazazi wasio fika mbali kielemu wao wafike mbali kielimu.

Imefika muda sasa nchi ianze kutumia data and figures kuangalia kiundani haswa matatizo yetu ni yapi na yana ukubwa kiasi gani na kutoka hapo tutafutie ufumbuzi. Je wakuu mna lionaje hili?
 
Ni kweli mwanaFa,
familia yenye maendeleo ya kielimu na kifedha hata watoto huwa na akili ingawa mara zingine mambo huenda vice versa.
Familia zetu za kimaskini huwa tunawaza tutakula nini. Ni ngumu kuwaza kuwekeza kwa ajili ya watoto maana kugonga menu 3 zenyewe per day huwa ni ngumu. mawazo kila siku hadi akili zinadumaa.
Mlo mzuri, mazingira mazuri ya kuishi ni vitu muhimu katika kujenga akili ya mtoto.
Watoto wa kimaskini wanakuwa affected tangu wapo tumboni mwa mama zao.
Mama mjamzito anashindwa kuafford vyakula ambavyo vinahitajika kutokana na hali yake, haishi katika mazingira mazuri na si ajabu yupo katika mgogoro mkubwa na mumewe.
Mama huyo mjamzito bila shaka atazaa mtoto tofauti (kiafya, kimwili na kiakili) na yule mama ambaye hakuwa na stress zozote katika kipindi chake cha ujauzito.
Katika kusolve tatizo nafikiri tuanzie tangu awali yaani pale mwanamke anapojiandaa kubeba mimba.
 
Hujafanya kweli utafiti,kwa taarifa yako watoto wa viongozi wengi wa nchi hii wanamatatizo makubwa (wavuta unga wa kulevya, bangi, wasumbufu shuleni, wanasababisha migomo mashuleni)sana ya kimalezi kiasi kwamba huwezi kulinganisha na malezi ya kijana aliyetoka familia za kimaskini.Nikikupa home work kidogo unaweza kuja na mengi.Nenda UDSM Faculty ya engineering na pale UCLAS chukua sensa kwa kuzingatia family earnings za vijana wale.

Nakuhakikishia utakuja na jibu tofauti na assumption yako.Engineers wengi nchi hii ni watoto wa familia maskini
 
Mkuu Husninyo,

Uliyo sema yote ni kweli. Na kuongezea ni kwamba kwa watoto wengi (si wote kutokana na mazingira) role model wake wakwanza na wakubwa ni wazazi. Kwa hiyo kama mzazi kasoma ni motisha kubwa sana na mtoto asime aidha kwa kutoka kuwa kama baba/mama au kwa kuogopa tu ile aibu ya kwamba mzazi kasoma lakini yeye haja soma.

Kwa bahati mbaya mtoto wa ambae haja soma unless awe yeye mwenyewe ana mawazo ya kuona mbali ni vigumu kwake kuona umuhimu wa elimu. Na hata kama mzazi ana muencourage asome ana weza atumie kisingizio cha mzazi kuto kusoma na yeye kuto kusema.

Na mwisho pia ni kwamba wazazi wengi (si wote) ambao hawaja soma wao wenyewe hawaoni umuhimu wa mtoto kusoma kwa hiyo elimu ya mtoto haiwi tena priority kwake. of course kuna exception na kwetu tu kuna mfano kwa sababu mimi babu haku bahatika kusoma ila ali tambua umuhimu wa elimu mpaka kuwekeza kwenye elimu ya mzee wangu na kuhakikisha ana malizo chuo. Wazazi ambao hawaja soma na wana tambua umuhimu wa elimu ni wachache sana.

Nadhani hili tatizo si la serikali tu bali ni la kijamii pia kwa sababu kama tunavyo ona haya yote yana tokana na mazingira na mentality za familia mtoto anapo toka.
 
umekosea hpo kwnye idad ya wtoto wanaozaliwa na wasomi! Wasomi wa zaman ndo walkuwa wanazaa watoto wa 2- 3! Wasomi wa ck hz mtoto m1 2!
 
Jana nilisoma mahali Pinda akisema "tatizo la umasikini TZ ni kutokana na kukua kwa idadi ya watu kinyume na kiwango cha uzalishaji kwenye kilimo".
Nimetanguliza hii kwa sababu alinishangaza Mh. Pinda kwa nini kaliona leo hili la "taathira za idadi ya watu kwa maendeleo" baada ya miaka 50 ya uhuru na utawala wa chama chake? Haihitaji utafiti wa kina kugundua kuwa familia zenye watoto wachache zina nafasi kubwa zaidi ya kushughulikia mahitaji muhimu kama vile chakula, mavazi, elimu na afya hata kama familia itakuwa masikini kwani itakuwa na "matumbo machache" ya kulisha na kuhudumia. Lakini tumezowea kusikia ikisemwa "tajiri na mali yake, masikini na wanawe", falsafa ambayo tumekuwa tukiitumia masikini kwa kudhani kuwa na watoto wengi ndio mtaji wa masikini. Pengine huko nyuma falsafa hii ilifanyakazi, wakati mahitaji yalikuwa machache, wakati familia iliweza kuishi kwa kilimo, uvuvi au ufugaji. Lakini kwa leo falsafa hii haifanyikazi tena kwani mambo yamebadilika. Ingawaje, kama alivyodokeza mmoja hapo juu, inawezekana kuwa kinyume: kuna familia za masikini zina wasomi na za wasomi zina wasiosoma, lakini hii ni chache sana.

Kwa nyakati tunzoishi, ikiwa familia ina wasomi, ina maana baba na mama watakuwa na ajira au mwamko wa kupambana na maisha kiasi cha kuongeza pato na kuweza kuwahudumia watoto wao.
 
Mkuu mimi nakuunga mkono kwa asilimia ndefu....

Najaribu kuangalia rafiki zangu ambao nilipiga nao primary enzi hizo wengi (wakiume kwa wakike) ambao hawakuendelea na shule ya sekondari mpaka sasa wengine wana watoto wa 5 hadi 6 wakati mimi mizunguko yote ya shule mpaka nakuja kumalizana nayo sasa hivi nina ka-kid kamoja tu.....

Pia hali ya mazingira ya hawa rafiki zangu haioneshi kuwepo na matumaini yoyote ya hawa watoto kuweza kufikia ciwango vikubwa kwa kuwa hakuna mpango kamambe wa wazazi kuwafikisha mbali....forecast ni elimu ya msingi na huko kwingine ni kudra za hapo baadae
 
Japo sija fanya utafiti rasmi, kuna mtu kanielezea kitu juzi na mimi kwa kutafakari tu naamini ni ukweli.

Juzi tumekaa na mmoja wa marafiki zangu ambae kiumri ni mkubwa zaidi yangu. Akaniuliza MwanaFa hivi unadhani Tanzania mtu aliye soma kwa wastani anazaa watoto wangapi na kwa wastani asiye soma anazaa watoto wangapi?

Nilikua sija lifikiria hili ila nikamuambia kwa kuangalia wale walio nizunguuka naweza sema kwa haraka haraka kwamba aliye soma huwa na wastani wa watoto wawili au watatu na asiye soma ana kuwa na wastani wa watoto sita au saba.

Akaniambia uko sahihi hizo ndiyo rough figures. Akaniambia je una kubali kwamba mtoto wa aliye soma nae ana nafasi kubwa sana kuwa msomi kama mzazi/wazazi wake na yule mtoto wa asiye soma kuna asilimia kubwa na yeye asifike mbali kimasomo?

Nikamuambia tena ndiyo hiyo ni kweli kabisa. Hata sisi kwenye ukoo wetu wali ambao wazazi wao walifika juu kielimu wengi wao na wao walifika juu kielimu na wale ambao wazazi wao wali pata elimu wastani au ndogo wengi wao wakaishia hivyo hivyo.

Hapa tena akaniambia kwamba observation yangu ipo sahihi. Sasa basi aka niambia nitafakari. Akasema kwa kutokana na logic hiyo basi ina maana msomi ata toa wasomi wawili au watatu na asiye soma nae ata toa watoto sita au saba ambao nao wata kuwa si wasomi. Akasema huoni hapa taifa letu tuna produce wasomi wachache sana ukilinganisha na wale ambao hawata kuwa wasomi?

Hizi zote ni rough figures tu ambazo tumeelezeana kutokana na simple logic and observation. Nadhani hata nyie wenzangu hamtabisha kwenye hili. Sasa basi kama kwenye kila kizazi tuna toa wasomi wachache kuliko wasio sema hii tayari si mzunguuko mbaya? Je ndiyo maana taifa lina zidi kudidimia siku hadi siku kutokana na kulea kizazi kisicho soma?

Kama tuta kubali kwamba hili tatizo lipo basi kama bado hatuja fanya ili takiwa serikali ifanye official research. Ikisha jua kwamba kweli tatizo lipo na kwa kiasi gani basi hatua ya pili ni kutafuta njia za kuwezesha na kuencourage watoto wanao tokana na wazazi wasio fika mbali kielemu wao wafike mbali kielimu.

Imefika muda sasa nchi ianze kutumia data and figures kuangalia kiundani haswa matatizo yetu ni yapi na yana ukubwa kiasi gani na kutoka hapo tutafutie ufumbuzi. Je wakuu mna lionaje hili?

Observation inakaribia kuwa sawa na ukweli ila empirical study inatakiwa ku-confirm hypothesis hii. Ukiangalia tokea wakati wa ukoloni sera ilikuwa ni kusomesha watu wachache ili waje kuwa wasaidizi wa serikali ya ukoloni na waliobakia likawa ni kutoa ujinga yaani mtu aweze soma barua na maelekezo ya watawala tu. Mfumo huu ulirithisiwa na serikali ya TANU baada ya uhuru kwa kuweka sera kuu kuwa Elimu ya msingi ni lazima kwa kila mtamzania baada ya hapo kila mtu ataangaliwa uwezo wake(on your own) na ilifikia wakati wazazi wasiopeleka watoto wao shule za msingi walikuwa wanashitakiwa. Elimu ya juu ikaachwa kuwa ya wachache wanaoonesha uwezo wa ziada kwenye mitihani kwa kufaulu kwa kiwango cha juu wakawa wanapelekwa shule chache za serikali. Then wanachujwa na baadae wachache Chuo kikuu(Kwenye form hizo kulikuwa na kipengele cha mtu kuthibitisha uwezo wa kupata elimu ya juu mojawapo ni kufaulu vizuri level za chini), sisi enzi zetu pale mlimani ilikuwa mtu anachagua bweni la kukaa hata kama atataka kuwa na vyumba kwenye mabweni tofauti kwani facilities zilikuwa nyingi zaidi ya watumiaji.

Baada ya serikali ya CCM kugundua kuwa kuboresha elimu na kuwanufaisha wananchi wengi ni kujichimbia kaburi kwa chama hicho kwani katika watu wasiokuwa na mapenzi ya dhati zaidi ya kimasilahi kwa CCM ni wasomi, wakaweka mikakati ya kudunisha na kuongeza vyuo vikuu kwa mwendo wa konokono, nchi kama Kenya ina vyuo vikuu vya umma around 21, hesabu Tanzania. Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 ni mfano mmojawapo wa mkakati wa kupunguza wasomi Tanzania ili CCM Ipate uhai wa angalau kutawala kwa miaka kama kumi ijayo kama si minne iliyobaki kwa kutumia kundi la watu wenye uelewa finyu wa haki zao kuwa tayari kuwayumbisha kwa propaganda za udini na ukabila. Leo hii ukiangalia watu ambao wanaoendeleza upupu huu wa udini utagundua kuwa majority ya perpetrators ni watu walioshia darasa la saba.

Serikali inaweza kabisa kuamua kuweka sera ya elimu ya lazima kuwa ni elimu chuo (level ya diploma) Ila kama mtakumbuka aliyekuwa msemaji wa serikali awamu ya kwanza ya Kikwete aliwahi sema kuwa kama vyuo vingi vya kati vitageuzwa kuwa vyuo vikuu na kutoa degree, taifa litakuwa na watu wengi wenye degree bila kuwa na kazi kitu ambacho si kizuri kwa usalama wa taifa(CCM).

CCM wanafanya mazingira ya kupata elimu ya juu kuwa magumu watoto wa walalahoi ili kuhakikisha Tanzania inakuwa ni nchi ya wajinga 80% na wasomi 20% ndiyo maana chaguzi nyingi CCM inapata kura za kishindo plus chakachua.
 
mwanafa hiyo ni kweli kabisa mimi nina mfano wa ninapokaa jirani yangu mama hajamaliza darasa la saba na baba kamaliza darasa la saba, mimi nina masters mke wangu ana degree tumebahatika kupata mtoto mmoja 4yrs na wao wanawatoto watano wa mwisho analingana na wangu ila yeye mkubwa kidogo cha kushangaza wangu tayari alikwisha anza nursery akiwa na two and half yers wakati wa jirani yangu ana 6 hata vidudu hajaanza na ukiangalia wazee wake hawana hata habari ya shule ni mtoto mmoja tu ndio anasoma tena form two kwa kufauru na anapenda shule

hii nimekupa kama mfano maana tunahitaji viongozi waliangalie hili maana wazazi wanachangia sana watoto wao kuwa na future au la, mimi mwenyewe baba angu ana masters na nilipofeli form four alinitafutia alternative ya kusoma kuanzia cheti of which angekuwa mzazi asiesoma asingeniimiza kwenye hilo na nilisoma vyuo vya serikali na kulipiwa ada
 
Mkuu Husninyo,

Uliyo sema yote ni kweli. Na kuongezea ni kwamba kwa watoto wengi (si wote kutokana na mazingira) role model wake wakwanza na wakubwa ni wazazi. Kwa hiyo kama mzazi kasoma ni motisha kubwa sana na mtoto asime aidha kwa kutoka kuwa kama baba/mama au kwa kuogopa tu ile aibu ya kwamba mzazi kasoma lakini yeye haja soma.

Kwa bahati mbaya mtoto wa ambae haja soma unless awe yeye mwenyewe ana mawazo ya kuona mbali ni vigumu kwake kuona umuhimu wa elimu. Na hata kama mzazi ana muencourage asome ana weza atumie kisingizio cha mzazi kuto kusoma na yeye kuto kusema.

Na mwisho pia ni kwamba wazazi wengi (si wote) ambao hawaja soma wao wenyewe hawaoni umuhimu wa mtoto kusoma kwa hiyo elimu ya mtoto haiwi tena priority kwake. of course kuna exception na kwetu tu kuna mfano kwa sababu mimi babu haku bahatika kusoma ila ali tambua umuhimu wa elimu mpaka kuwekeza kwenye elimu ya mzee wangu na kuhakikisha ana malizo chuo. Wazazi ambao hawaja soma na wana tambua umuhimu wa elimu ni wachache sana.

Nadhani hili tatizo si la serikali tu bali ni la kijamii pia kwa sababu kama tunavyo ona haya yote yana tokana na mazingira na mentality za familia mtoto anapo toka.

kweli mkuu, mimi niliwahi kuuliza wanafamilia, mbona ukoo hivyo, elimu haba, pesa hakuna.
Wazee wakaniambia tatizo sio wao, tatizo babu na bibi yangu hawakuandaa mazingira mazuri ya watoto wao.
Ningepata nafasi ya kumuuliza babu na bibi na wenyewe wangewalaumu wazazi wao.
Mlolongo wa lawama ungezidi kushuka chini.
Wazazi wanachangia kwa kiasi chao ila watoto nao waamke.
Nilikuwa na anko wangu(RIP) mmoja alikataliwa na baba yake, mama yake akashindwa kumtetea , mtoto manyanyaso yalizidi akatokomea.
Muda mrefu sana ukapita, akarudi mkubwa kasoma na kazi anayo.
Wazazi wake haohao wakawa waomba misaada, ndugu zake waliozaliwa tumbo moja nao hawakufika popote kimaisha, yule anko ndio akawasaidia saidia maisha.
Haya maisha, unapoona mzazi hana future na wewe, amka maana mwisho wa siku itakuwa ni kilio chako wewe na familia yako.
 
Primary tulikuwa wanafunzi zaidi ya 400 waliomaliza darasa la saba, walifaulu 26 tu kwenda shule za serikali, miaka hiyo private ni za kuhesabu ina maana wengi wao waliishia mtaani.

Kati ya hao 26 walipangwa shule moja ya serikali,kwenye matokeo ya form four waliokwenda kidato cha sita ni 8 tu kati ya 26.

Kati ya hao nane waliofika mlimani chuo kikuu bila kuunga unga ni watatu tu.

Lakini nimekutana na school mates wengi sana wa tangia primary ambao hawakuendelea na masomo, they are doing some small business na maisha yao sio mabaya. Hivi elimu ya darasani pekee ndio kigezo cha kuwa na maisha bora?

Primary industry kama ufugaji, kilimo na uvuvi vikiboreshwa vitatusaidia sana ambao hatukupata bahati ya kufika hadi chuo kikuu tukiongozwa na maafisa kilimo from SUA kama wataalamu.
 
Hujafanya kweli utafiti,kwa taarifa yako watoto wa viongozi wengi wa nchi hii wanamatatizo makubwa (wavuta unga wa kulevya, bangi, wasumbufu shuleni, wanasababisha migomo mashuleni)sana ya kimalezi kiasi kwamba huwezi kulinganisha na malezi ya kijana aliyetoka familia za kimaskini.Nikikupa home work kidogo unaweza kuja na mengi.Nenda UDSM Faculty ya engineering na pale UCLAS chukua sensa kwa kuzingatia family earnings za vijana wale.

Nakuhakikishia utakuja na jibu tofauti na assumption yako.Engineers wengi nchi hii ni watoto wa familia maskini

Mkuu nadhani huja nielewa kitu kimoja kwa hiyo ngoja nikueleze upya tuone kama uta kuwa na mtazamo tofauti. Hapa observation yangu siyo kutokana na kipato cha mzazi bali elimu ya mzazi. Mzazi ana weza asiwe na uwezo mkubwa wa kipesa lakini akawa na elimu nzuri na pia mtu ana weza akawa tajiri mkubwa na akawa hana elimu. Hypothesis hapa ni kwamba kiwango cha elimu cha mzazi kina changia kwa kiasi kikubwa kiwango cha elimu ata kayo kuja kupata mtoto na wala sija taja uwezo wa kifedha.
 
Mkuu Mammamia,

Ni kweli labda fikra za jamii yetu pia ina changia. kama ulivyo sema hapo juu "Tajiri na mali zake na masikini na wanae". Ila mimi naona hii falsafa ni ya kibinafsi kidogo kwa sababu mzazi ana zaa watoto wengi kwa kudhani kwamba hiyo ina ongeza nafasi ya watoto wata kao kuja kumsaidia. Kwa hiyo mzazi hapo hazingatii future ya mtoto bali ana angalia ni jinsi gani ata kuja kusaidiwa baadae.
 
Mkuu Hofstede,

Hata mimi I was thinking along the lines kwamba nchi nyingi ambazo zina strong hold governments or parties zina dumaza elimu maksudi kusudi kuweza kuendelea kutawala. Hili nilisha wahi kudiscuss na mtu na hapo nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja.

Pia kuhusu wakolini kukazania elimu ya kusoma na kuandika tu ni kweli sisi wenyewe tume kuja kuendeleza hilo tatizo. Kuna wakati Speaker Makinda alitoka jukwaani na kusema wana taka kutengeneza taifa la "form four". Kilicho nichekesha ni kwamba aka toa maelezo marefu yasiyo na msingi wakati solution ya kufanya hivyo ni kusema sasa kwamba watoto ni lazima wafike form four. Aidha Bunge lina weza hata kutunga sheria kwa kusema mtoto lazima abaki shule mpaka afikishe miaka 16. Kwa miaka ya siku hizi watoto wengi wenye umri wa miaka 16 wata kuwa tayari wamefika sekondari haswa ukizingatia tayari tuna sheria inayo sema mtoto yoyote mwenye miaka 7 lazima aanzishwe shule.

Kuna vitu logical na basic tuna weza kufanya kuimprove hali zetu na nchi zetu sema kwenye matawi yetu ya serikali hatuna great thinkers bali wapiga siasa tu.
 
Primary tulikuwa wanafunzi zaidi ya 400 waliomaliza darasa la saba, walifaulu 26 tu kwenda shule za serikali, miaka hiyo private ni za kuhesabu ina maana wengi wao waliishia mtaani.

Kati ya hao 26 walipangwa shule moja ya serikali,kwenye matokeo ya form four waliokwenda kidato cha sita ni 8 tu kati ya 26.

Kati ya hao nane waliofika mlimani chuo kikuu bila kuunga unga ni watatu tu.

Lakini nimekutana na school mates wengi sana wa tangia primary ambao hawakuendelea na masomo, they are doing some small business na maisha yao sio mabaya. Hivi elimu ya darasani pekee ndio kigezo cha kuwa na maisha bora?

Primary industry kama ufugaji, kilimo na uvuvi vikiboreshwa vitatusaidia sana ambao hatukupata bahati ya kufika hadi chuo kikuu tukiongozwa na maafisa kilimo from SUA kama wataalamu.

Mkuu hapa argument siyo kwamba elimu ndiyo njia pekee ya kutokea kimaisha....la hasha. Hapa linalo jadiliwa ni kiasi gani kiwango cha elimu cha mzazi kina changia kiwango cha elimu mtoto ata kayo fikia na yeye. Hapa hakuna anae sema kufika chuo au kusoma ndiyo njia pekee ya kuwa na maisha bora. Tunaangalia tu uhusiano wa elimu ya mzazi na ya mtoto. Kwani si kila msomi ana maisha mazuri na si kila tajiri ana elimu nzuri.
 
Mkuu mada hii ni nzuri japo kuwa haijafanyiwa utafiti. Hata kwa kuangalia historia zetu wenyewe humuu jamvini, utagundua kuwa lilozungumzwa ni kweli kabisa. Mifano ipo hai na kama tungekuwa honest humu ndani, na mtu aeleze kizazi chake na ni wangapi wameenda shule, utakuta wakuhesabu. Ule usemi wa umetumwa na kijiji kusoma, japo kuwa huwa ni utani lakini unaukweli ndani yake. Utakuta katika kijiji kizima mtoto ama kijana anayefika kidato cha nne ndiye anayeonekana msomi. Wazazi wengi vijijini priority yao siyo mtoto kwenda shule, visingizio ada hata kama anakauwezo ka kumlipia mtoto ada. Kwa kuwa yeye anaendesha maisha yake, haoni umuhimu wa kumsomesha mtoto wake. Kama mzazi huyu angekuwa na ufahamu nakujua umuhimu wa elimu, basi angefanya hima mtoto aende shule. Sasa angalia kwenye boma lake, anaongeza idadi ya wake na watoto bila hata kujua watakuwaje. Ukiuliza watoto wote hawa watakula nini? Utaambiwa kila mtoto anakuja na ridhiki yaake. Kazi kwelikweli elimu inahitajika ili kuokoa kizazi chetu.
 
Japo sija fanya utafiti rasmi, kuna mtu kanielezea kitu juzi na mimi kwa kutafakari tu naamini ni ukweli.

Mada nzuri japo hujafanya utafiti kama ulivyosema .Naomba nikurudishe nyuma kwanza Tunavyosema msomi tunaamisha nini.?Mipaka au vigezo au mwanzo wa mtu kuitwa msomi ni ni nini?

  • Ni yule mwenye cheti cha degree tu au hata advnced dploma?
  • Ni wale wanaoitwa ma Dr , prof tu au wale watu wana
  • Ni mtu anayefanya kazi ya kuvaa tai(Wakili mhasibu, etc) na ana ofisi na kusika kalamu au hata hata yule anayevaa ovaroli fundi wa friji na TV naye anaweza kuwa msomi?

Na mimi naweza kumalizia bila utafiti kwa kusema ni hawa wasomi wengi ndio wanazaa na kufanya reproduction nje ya ndoa. N a hao wasiokuwa wasomi hata akizaa watoto sita mara nyingi ni na mke au mme au wake halali.
 
Wakumwitu,

Discussion niliyo kuwa nayo na huyo mwenzangu ilikua kama chemsha bongo au kwa Kiingereza wanaita food for thought. Nia yangu ni kuangalia kama kweli kuna ukweli ndani yake na nipo very interested kuja kuifanyia utafiti zaidi pindi nita kapo maliza chuo. Ila kwa jinsi wadau walivyo changia inaelekea kwamba nilicho sema kina ukweli japo utafiti una hitajika ili facts, figures and data ziweze kutumika katika kusulihisha taizo.
 
Mada nzuri japo hujafanya utafiti kama ulivyosema .Naomba nikurudishe nyuma kwanza Tunavyosema msomi tunaamisha nini.?Mipaka au vigezo au mwanzo wa mtu kuitwa msomi ni ni nini?

  • Ni yule mwenye cheti cha degree tu au hata advnced dploma?
  • Ni wale wanaoitwa ma Dr , prof tu au wale watu wana
  • Ni mtu anayefanya kazi ya kuvaa tai(Wakili mhasibu, etc) na ana ofisi na kusika kalamu au hata hata yule anayevaa ovaroli fundi wa friji na TV naye anaweza kuwa msomi?

Na mimi naweza kumalizia bila utafiti kwa kusema ni hawa wasomi wengi ndio wanazaa na kufanya reproduction nje ya ndoa. N a hao wasiokuwa wasomi hata akizaa watoto sita mara nyingi ni na mke au mme au wake halali.

Mkuu msomi hapa tunaongelea mtu yoyote aliye hitima taasisi yoyote ya elimu ya juu. Kwa maana hata messenger wa ofisini mwenye elimu ya lasaba ana weza akavaa shati na tai na engineer pamoja na degree yake/zake ana weza akavaa ovaroli kwa hiyo mavazi si kigezo.

Kuhusu hilo unalo sema la wasomi wengi kuzaa nje ya ndoa hilo sito kubaliana au kupingana na wewe. Kwa kuwa mtu aliye soma ana nafasi kubwa ya kuwa ya rasilimali zaidi yawezekana kabisa ni rahisi zaidi yeye kumaintain uhusiano na watoto nje ya ndoa ili hali masikini uwezo huo ana weza asiwe nao. Ila hata kama na huyo msomi akizaa nje ya ndoa je hao watoto nao wana nafasi gani ya kufikia kiwango cha elimu ya baba yao? Najua watoto kadhaa nje ya ndoa ambao baba zao wamesoma na wao waka fikia kiwangohicho hicho (japo sisemi no wote).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom