Tafakari juu ya Uongozi wetu na mwelekeo wa taifa letu.

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Katika Taifa lolote Viongozi ndio wanaobeba maono na dira ya nchi. Ubora wa Taifa lolote lile unategemea sana maarifa na busara za Viongozi wao. Kwahiyo Aina ya nchi, ujenzi wake, mpangilio wake na utamaduni wake imara utegemea sana viongozi.
Kwahiyo aina ya nchi yeyote ile inategemea uwezo wa kiakili na wa ki maarifa wa viongozi wao. Viongozi wanawajibu wa moja kwa moja wa kuleta mabadiliko katika taifa lolote lile. Mabadiliko yeyote katika taifa lolote lile huletwa na viongozi wao. Taifa imara hujengwa na viongozi imara wenye maono na malengo ya kizalendo kwa watu wao. Kwahiyo aina ya taifa tulilonalo inaonyesha uwezo na mipaka ya viongozi wetu katika kufikiri na kuleta mabadiliko. Viongozi wenye dhamira ya dhati kwa watu wao wanapenda kuona maisha ya watu wao yakibadilika na kuwa bora.

Mantiki ya uongozi ni kuonyesha njia, Hauwezi kuonyesha njia pasipokuwa na maono, Kiongozi lazima ajue anapaleka wapi watu wake na aina gani ya taifa yeye na watu anaowaongoza wanataka walijenge kwa faida ya wote. Kiongozi hubeba matumaini ya taifa, Watu humwangalia yeye na kumtegemea kutatua matatizo yanayokabili umma. Kiongozi pia hujenga mentality ya watu. Ukinionyesha Kiongozi nitawajua watu wake. Naamini watu huchagua watu bora miongoni mwao kuwa viongozi wao. Kwahiyo Kiongozi mjinga huwakilisha wajinga wenzake, Watu wenye akili hawawezi kuchagua viongozi wapumbavu. Jamii za kijinga huzaa viongozi wajinga, Jamii za kifisadi huzaa mafisadi vile vile na wanaweza kumwacha kiongozi mzuri sababu ya ufisadi wao na kutokupenda kweli. Ili taifa letu libadilike lazima tuwatafute watu wetu bora popote pale walipo tuwape madaraka watuongoze hii ni kwa faida yetu wenyewe kwakuwa Taifa kama kitu kilichoundwa husambaratika kama hakuna maono na busara za kulilinda taifa hili na kuliendeleza.

Tunahitaji Viongozi ambao watasimamia kweli, watasimamia haki na umoja wetu kama taifa ili kulilinda na kuliendeleza Taifa letu kwa vizazi vingi vijavyo lakini pia kuleta amani na maendeleo ya watu wetu. Hatuwezi kuwa wamoja kama hakuna Order katika Taifa lakini pia hatuwezi kuwa na mwelekeo kama hatuna Order katika taifa. Na Order itapatikana katika utii wa sheria, hatutaweza kuendelea kama Taifa kama hatutazingatia Haki na utawala wa Sheria. Lakini pia kama hatutarejesha upya akili zetu kutoka katika ubinafsi kuja katika Utaifa na kuwa Tayari kulitumikia. Taifa letu liko katika confusion kubwa tunahitaji dira. Ninaamini tuna nguvu kazi kubwa kama tukiwa wamoja na wazalendo tunauwezo wa kulitoa taifa hapa lilipo, Lazima tuwe na roho ya kulitumikia Taifa hili na kulijali hapa ndipo tulipozaliwa na mababu zetu walipokulia.


Tukishindwa kujiongoza wenyewe tutakuwa kielelezo cha upumbavu wetu na kutostaarabika kwetu kwa kutokukubali kwetu kuwa wamoja na kufanya mambo yetu kiustaarabu kwa faida ya wote. Ufisadi unaua bond katika jamii na madhara yake ni makubwa. Hatuwezi kusalimika na kupigana wenyewe kwa wenyewe kama hatutaacha ufisadi na kutii sheria. Kama hatutaacha tamaa Zetu zisizokuwa na mipaka na kujenga nchi kwa kupendana na kujaliana. Ni lazima tukumbuke tunawajibu sisi tuliopo sasa duniani kujenga mazingira mazuri kwa vizazi vyetu vijavyo. Tamaa isiyokuwa na mipaka huleta migogoro katika taifa. Haiwezekani tuendelee kuishi hivyo, Hali hii sio nzuri kwa majaliwa ya Taifa letu. Kwa heshima kubwa na taadhima iliyopo ndani yangu nawaomba tuzingatie Utaifa wetu na Tutimize wajibu wetu kwa taifa letu kwa kutendeana Haki na kuheshimiana.
Tukijua kwamba sisi watu wa Taifa hili sio watu tofauti ila watu wamoja wenye malengo mamoja na tunaoishi katika taifa moja ni hatua kubwa katika kuleta uzalendo na maendeleo yetu. Tuwe Tayari kulipigania na kulilinda Taifa letu, Tuwe tayari kunyanyua Bendera ya taifa letu kwa sifa na nguvu, Tukiwa wamoja na tukipendana hakuna kitakachotushinda, Tutasawazisha milima. Hakuna atakayesimama mbele yetu kama tukiwa wamoja, kama tukiwa na malengo mamoja na kama tukifanya jitihada kujikwamua kama Taifa katika sayansi na uvumbuzi na kama tukiwa tayari kulilinda taifa letu mpaka kufa ili liendelee kuwepo kwa faida ya vizazi vyetu.


Mawazo yetu yana influence kubwa katika ujenzi wa taifa letu hivyo tuwe makini sana na maneno tunayoongea kuhusu taifa letu. Lazima yawe yenye manufaa kwetu na yenye kutujenga sio kutubomoa kama Taifa. Sehemu yeyote tuliyopo iwe bar au sehemu nyingine lazima tuongee maneno ya kujenga taifa letu, Maneno ambayo yata influence Jamii yetu kulitumikia taifa lao wenyewe. Maneno ambayo yatajenga courage ya kulitumikia taifa hili na kuliletea glory and honor. Taifa letu lisiogope vita litayarishe vijana wetu kuwa tayari kupigana ili kulinda heshima na uhuru wetu, Wafanye hivyo kwa mapenzi ya roho kwaajili ya mapenzi ya kulinda heshima ya Taifa letu.


Taifa letu tutaendelea kuwa walalamikaji na watu wasiokuwa na furaha kama hatutapendana na kuwa wamoja na kuwa na collective effort katika matatizo yanayotukabili ni lazima tuwe na sauti moja. Tukifanikiwa kwa pamoja katika malengo yetu Taifa zima litakuwa na furaha, Tutaweza kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini kwakuwa matajiri watakuwa tayari kufanya effort kunyanyua raia wenzao kama watakuwa na upenzi na uzalendo kwa Taifa walilozaliwa. Watalipa kodi. Kwasababu kodi ndizo zinazosaidia katika ulinzi wa rasilimali zao. Watu wawe na uhakika wa mali zao kuwa salama. Tutajenga mazingira ambayo kila raia atakuwa na uwezo wa kutumia kipaji chake na kuzalisha kadili awezavyo, Hatuwezi yote hayo pasipo kuwa wamoja. Vitu pingamizi katika maendeleo yetu kama rushwa lazima tuviondoe ili tuwe na jamii yenye furaha na endelevu yenye Maendeleo. Natumaini tukizingatia haya niliyoandika na mengine ambayo mnayo nyinyi, Taifa hili litaendelea.
Kila binadamu ana uwezo wake, na pia anaweza kuwa mchango mkubwa katika Taifa hili kama tukitumia vipaji vyetu vyema.
Ningependa ushauri na maoni yenu jinsi ya ujenzi bora wa Taifa letu na ustawi wake. Aksanteni.
 
Back
Top Bottom