Tabora: Wabunge wa CHADEMA waachiwa kwa dhamana; Kupokewa kwa maandamano Igunga

Kwa vyovyote iwavyo, hii kesi kama wataifikisha mahakama ya Tabora mjini itakuwa na manufaa makubwa kwa CDM, Maana itatoa fursa kwa wakaazi wa Tabora kuhudhuria na kusikiliza jinsi ambavyo CDM walivyo watetezi wao na kuwajengea ujasiri wanatabora wengi kuacha woga wa polisi na hata kuwafanya wajiunge na CDM. Nafikiri CCM kama wataipotezea hii kisi watakuwa wameliona hilo. Maana mbali na umaarufu kwa CDM kuongeza TBR pia mbinu zao za kutafuta ushindi kwa vyovyote zitawekwa wazi nchi nzima. Na si tu kuwekwa wazi bali piakuwafanya wakuu wa mikoa na wilaya kuonekana useless miongoni mwa wananchi wasiokuwa na imani na CCM. Yaani hii kesi ni kama vile Kitendo cha Salva kukanusha kuwa JK hakununuliwa suti, angekaa kimya leo hii ni wachache sana wangekuwa wanaelewa habari ile ila kwa kukanusha wameipatia Publicty habari ile na kila mtu anajua Wikileaks iliandika nini kuhusu Rais wetu.
Mara nyingi huwa nawaambia CCM hawajui kufanya morden propaganda inatumia propaganda za kikoloni za kutisha watu, hebu jiulize swali dogo tu kwa kitendo hiki CCM imepoteza kura ngapi wangapi wameichukia CCM kupitia polisi kuwakamata wabunge wao. Hii kesi itaiuza CDM zaidi ya CCM maana inasambaza moto mkoa wa Tabora ulio ngome ya CCM.
 
Malaria Sugu wewe huyo ? Basi tutaona mengi mwaka huu,
Mkuu DOUGLAS, unajua nilipoona hilo andiko la MS nikakumbuka kusikia wimbo mmoja unaimbwa "Neema,neema, neema imefunuliwaaa!.........##~~~" si ajabu MS yamempata hayo. Tuvute subira kudhibitisha hilo.
 
Siku zote ukweli husimama na uongo hata uje na nguvu kwa kiasi gani, hauwezi kuusaga ukweli.
Ukweli ni kaa la moto linalounguza kila utumbo unaojaribu kuumeza.
Kwa hapa kwetu ukweli ni NGUVU YA UMMA na yeyote aliyejaribu kuiharibu amejikuta matatizoni. Jeshi la polisi wameungua, ccm na cuf wameungua, mafisadi ndo wanasubiri kujifia au kuhama nchi hii.
Wanaomba milima iwafunike na ardhi iwafukie kukwepa NGUVU hiyo ambayo UMMA wa watanzania umeikabidhi CHADEMA.
Peeeepleeeeezz....
 
Wana JF,

Taarifa niliyoipata hivi punde ni kwamba wapambanaji wa Chadema, Meneja wa Kampeni Sylivester Kasulumbayi (MB) na Suzan Kiwanga (MB)waliokuwa wamekamatwa kwa hila na polisi wa magamba wameachiwa huko Tabora na sasa muelekeo ni kwenye uwanja wa mapambani Igunga, Hakuna kulala mpaka kieleweke

wewe naye mwehu kama hao waliokuwa wamekamatwa. kama unapenda fujo na utovu Wwa nidhamu si uende huko Libya na Yemen. yani wamefanya upuuzi halafu unawaita wapambanaji. ama kweli CHADEMA IMEJAA MAJINGA MATUPU.
 
Tukio zima la kupigwa kwa DC Igunga limetufunza yafuatayo..
  • Funzo kwa viongozi wote wa serikali kuwa wakae mbali na uchaguzi waviache vyama vipambane vyenyewe
  • Afande Mwema awasifu wanachama wa Chadema kwa kutekeleza kwa vitendo dhana yake ya Ulinzi jamii shirikishi
  • Ni kweli haki huwa haipotei inacheleweshwa kitendo cha kuwatoa Igunga na kuwapeleka Tabora ilikuwa ni kuchelewesha haki yao
  • Kwa kitendo hiki kisiasa CDM imefaidika zaidi kulinganisha na wapinzani wao CCM
  • Viongozi kama ma DC wapewe ulinzi wa polisi muda wote wawapo kazini
 
CCM ni sikio la kufa. Chama tawala kikifanya hila za kuwaweka wapambanaji rumande kwa kutumia vyombo vya dola vilivyo chini yake ni hatua mojawapo ya kuelekea kuutema utawala. Hoja hujibiwa na hoja na wala si mabavu. Poleni wapambanaji. Karibuni tena Igunga tuteke jimbo kilaini. CCM haina chake na hatuitaki.
 
Tayari makamanda wameachiwa kwa dhamana baada ya kusomea shitaka la shambulio la aibu, kwa uoga mkubwa wamesomewa mashtaka kwenye mahakama huko Tabora, badala ya Igunga kosa lilikofanyika.

Mapambano yanaendelea

Sasa wajifunze kuwa na adabu kwa mamlaka halali.
 
Anavaa hijabu au mtandio? Huu si hata mtoto w amiaka 2 anauvuta tu?

DC-IGUNGA-NA-CHADEMA.jpg


31.jpg
 
Makamanda akina Tundu Lissu, Kasulumbai na Ester wapo Nzega Motel wanapata msosi Nzega tayari kwa kwenda Igunga. Wana vumbi balaa, kwani barabara ya Nzega Tabora haifai. Nawasilisha.
 
hata nyerer kabla ya uhuru alikamatwa na wakolono(weupe)ila haikuzuia uhuru sembuse hawa wakoloni weusi wasiojua hata bastola inatengenezwaje?
freedom is coming tomorow.

I couldn't have said any better.

Nashangaa mpaka karne hii watu bado wanategemea mambo mazuri yajilete yenyewe kwenye kishaza za fedha (silver platter)!!
 
Katika dhamana yao hakuna mashariti yoyote? Mfano; Kuto-onekana Igunga, au kuto-jihusisha na mikutano ya kampeni.
 
Back
Top Bottom