Tabasamu: Wananchi wangejua Bajeti anayotumia CAG kufanya Ukaguzi halafu ripoti yake inapigwa danadana Pasingekalika!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,995
Mbunge wa Sengerema mh Tabasamu amesema Wananchi wangejua Bajeti anayotumia CAG kufanya Ukaguzi halafu ripoti yake inapigwa danadana Pasingekalika

Tabasamu amesema kwa mfano CAG akija Sengerema anakaa siku 45 na anakuwa na Watu 9 wanakaa kwenye Hotel ya viwango Vya Juu

Tabasamu amesema mwaka jana Bajeti ya CAG ilikuwa tsh 10 bilioni na ushee, halafu anaandaa ripoti ambayo kimsingi inacover 10% tu ya shughuli zilizofanyika kwenye Taasisi inayokaguliwa unakuta tena watu tunaanza kupiga danadana

Source: ITV Kipima Joto
 
Source; ITV Kipima Joto
Hii ndo Tanzagiza, unaanza mijadala wa bajeti nyingine wakati iliyotangulia hola
 
Mbunge wa Sengerema mh Tabasamu amesema Wananchi wangejua Bajeti anayotumia CAG kufanya Ukaguzi halafu ripoti yake inapigwa danadana Pasingekalika

Tabasamu amesema kwa mfano CAG akija Sengerema anakaa siku 45 na anakuwa na Watu 9 wanakaa kwenye Hotel ya viwango Vya Juu

Tabasamu amesema mwaka jana Bajeti ya CAG ilikuwa tsh 10 bilioni na ushee, halafu anaandaa ripoti ambayo kimsingi inacover 10% tu ya shughuli zilizofanyika kwenye Taasisi inayokaguliwa unakuta tena watu tunaanza kupiga danadana

Source: ITV Kipima Joto
Kwani wanaopiga danadana si ni hao hao ccm?? Ifike hatua msilaumu matokeo. Shukeni chini hadi kwenye kiini! Shusheni injini chini. Fanyeni overhaul!
Fanyeni
 
Huyo CAG ndo kamsikia leo
Huyo Tabasamu ni Muongo Bhana. Kwanza Hana tofauti na wale wazee wanaokaa kwenye vijiwe vya kahawa huwa wanapenda kukuza Mambo.

CAG ni taasisi kubwa ina idara kila mkoa, Hao NAOT wapo pia kwenye ofisi za Hazina Ndogo za Mikoa.

Ukaguzi unafanyika kimkoa, Then taarifa zinakusanywa na kufanyiwa majumuisho ya mwisho ambayo ndo huwasilishwa kwa CAG ili amkabidhi Rais na kuyawasilisha Bungeni.
 
Hivi matumizi ya ofisi ya CAG huwa yanakaguliwa na nani? Au wanajikagua wenyewe?!
Hawezi kujikagua kwa jinsi ile ile huidhinisha malipo ya Setikali (kama mdhibiti) halafu akikagua (kwa madaraka yake ya ukaguzi) anatoa "audit query"!! Anakuwa wapi fedha aliyoidhinisha isitumike kama ilivyokusudiwa hadi anapokuja kufanya ukaguzi?
 
Serikali inajitakia tuu yenyewe hizo gharama. NAO inatakiwa kuwa kibiashara zaidi na ingeweza ajili vijana wengi zaidi na kufanya ukaguzi kwa muda zaidi.

CAG inakaguwa serikali za mkoa na halmashauri zenye mapato yao ya ndani, taasisi za kibiashara zenye income mpaka za kufuturisha na kutoa charitable donations.

Ha wote CAG ilitakiwa awatoze kwa hizo kazi, wengi wanamudu hizo gharama. Serikali ibaki inagharamia audit za wizara na kutoa kiasi tu cha ruzuku kwa CAG kuliko kuwaacha kuwa tegemezi 100%.

Yaani bandari yenye kukusanya mabillion kila mwezi serikali ilipie audit zake au TANAPA au halmashauri za majiji; hayo ni matumizi mabaya ya hela za walipa kodi. Wafanye kazi kama accounting firms za kibiashara sio kutegemea hela za serikali.
 
Back
Top Bottom