Taasisi za kidini Zanzibar zakanusha kuhusika na tamko la Uamsho la kususia zoezi la Sensa 2012

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]TAASISI MBALIMBALI ZA KIDINI HAPA NCHINI ZILIZOPATA USAJILI RASMI KWA MRAJIS MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ZIMEKANUSHA KUHUSIKA NA TAMKO LILILOTOLEWA NA AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO, SHEIKH MSELEM ALI LA WAISLAMU WA ZANZIBAR WAGOMEE KUSHIRIKI KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAAZI KITAIFA INAYOTARAJIWA KUFANYIKA JUMAPILI IJAYO.


Wakizungumza na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa Taasisi hizo wamelaani tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea Taasisi hizo.


Aidha,wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza na Taasisi za Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga kushiriki kwa Waislamu katika Sensa.


Aidha, wameihakikishia Afisi ya Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika Sensa ili kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro ya kijamii na sio kujiingiza katika siasa na kupingana na Serikali kama ambavyo imekuwa ikifanya Jumuiya ya Uamsho.


Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.


Aidha, wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja wa Taasisi za kidini Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo nyingi hazikubaliani na Sera yao ya fujo na vurugu.


Imetolewa na:




Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar


[/h]

 
Interesting... Ina Maana UAMSHO iko ndani ya SERIKALI ya MUUNGANO ya ZANZIBAR
 
Naona waislamu wanacheza mchezo wa kuigiza. Kila siku ni matamko tu hakuna kujadili maendeleo ya kaya zao na taifa.
 
Serikali imeshafeli na sasa mmekuja na mbinu feki ya walimu na madaktari, hospital watu wamegoma nyie mnasema wafanyakazi wote wapo huduma zinaendelea, mashule yote yanafanya kazi walimu hawajagoma. Mtu aliyepania kufanya kitu fulani bila mazungumzo huwezi badili nia yake, nilitaka kusikia kuwa serikali imefanya mazungumzo na waislamu na wamekubaliana kushiriki zoezi la sensa.
 
serikali dhaifu,let the do kinachowapa raha!!!
sensa yenyewe ina maswali 60.walishaona hakuna wa kuwatisha,na wako tayari kumhujum kikwete kama yeye anavyowahujumu.
 
Palipo udhia penyeza rupia. Hongera Vasco da Gamma kwa kuliona hilo. Ama kweli njaa ni mbaya!
 
Back
Top Bottom