Taasisi husika wachunguze wamisionari feki.

Rouby

Member
Dec 5, 2006
7
0
Ndugu wana JF,

Ninakerwa sana na hawa wazungu wanaokosa kazi kwao na kuja Tanzania na kujidai ni ma-exparts katika taaluma ambazo hata sisi wazawa tunazijua tena kuliko hata wao. Wengi wao wanakuja kupitia mashirika ya dini,na kujaribu ku-penetrate kwa kujidai kama vile ni madaktari,maofisa tawala au ma-engineer,wakati hawana lolote,isitoshe,wanatumia mbinu ya kama ma-valontia lakini wakishapata vibali vya kazi wanadai kulipwa mishahara tena kutoka serikalini,zipo baadhi ya hospitali za dini ambazo zimeajiri watu kama hao,tembelea hospitali nyingi teule (DDH) au VAH katika baadhi ya wilaya,mfano Ngorongoro,Songea n.k. utakuta wengi wapo kama madaktari au maofisa tawala ambao bado siamini kama uwezo wao unaozidi wasomi tulionao. Isitoshe,wanajipatia misaada na fedha kutoka katika nchi zao za Ulaya kwa kutumia majina ya taasisi tulizonazo kwa kujineemesha au kupata mitaji bila ya idhini ya taasisi hizo. Hela wanazozikusanya haziwekwi wazi ni kiasi gani,badala yake wanazitoa mifukoni mwao kama vile kutuzuga tuu. Hatuhijtaji kuwa shamba la kuwaneemesha kwa kupitia migongo yetu.

Tumechoka wadanganyika,tuamke.

WanaJF nawasikiliza.
 
sekita za migodi ndo wamejaa utadhani kwao kazi hawajui mpaka wafundishwe inauzi inatisha inasikitisha ,

wapo wapo tu
 
Imagine,wanapiga picha za wamasai,wanazipeleka kwao kuonyesha ni jinsi gani tuna shida,wanachangisha fedha za kutosha ambazo hatujui ni kiasi gani,halafu hapa tunapigwa "changa la macho" kwa kupewa kiasi kiduchu. Ndugu zangu wamasai mmegeuzwa mtaji wa wazungu. They are here doing nothing,most of the time they just sit writing proposal kujidai wanatuombea hela bila idhini yetu. Lakini nashangaa,mbona wanakuja huku kama madaktari,wataalam halafu wanafanya kazi zisizowahusu. Taasisi inayohusika inaangalia kweli kama hawa watu wanafanya kilichowaleta? Nina wasiwasi wanaweza hata kutuuza hawa.
 
Taasisi husika zimelifumbia hilo macho. Rais wetu alipoingia madarakani aliahidi kuangalia suala la ajira za wageni hapa nchini. Lakini hilo hatujaona hata likishughulikiwa, achilia mbali kushindwa. Hawa wageni wako nchini mwetu kwa wingi sana migodini kama alivyosema First Lady na hakuna wanalolijua. Wanaletwa kwamba ni wataalam, wakifika migodini wanahitaji wafundishwe na watanzania, wakikataliwa, wanawageuzia kibao kwa kusema hawawezi kazi ili wafukuzwe.
Kwa kweli nchi yetu iangalie hili.
 
Back
Top Bottom