Taarifa sahihi kuhusu ulinzi wa Dk. Willibrod Slaa dhidi ya upotoshwaji unaoenezwa

huyu mlinzi nae kilaza tu,alitakiwa awe na line special kwenye cell phone special kwa ajili ya kutoa siri za Chadema tu,halafu hiyo cell phone alitakiwa aifiche na lazima yeye ambip kwanza Mangula halafu Mangula ndo ampigie.halafu ujinga wa kupanda gari lenye number,bora hata angekuwa anatumia bajaji halafu anapiga sungogoz,au anavaa hijabu kabisa ile ya kufunika pote na anakuwa kama demu.Nyie CCM Endeleeni kutafuta watu huko CHADEMA ili wawape siri za adui yenu,wanananunulika hao wana njaa,Maana Mbowe na Slaa wanajikopesha ruzuku peke yao tu
 
Katika hili kurugenzi ya Habari chadema amja tutendea haki kabisa.Taarifa ya katika mitandao imekuja vipande vipande sana Tunaitaji Taarifa ,Zaidi kwa Kina

Tatizo Chadema kumejaa makanjanja wanaofanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa wao.Hapo ni mpaka Mbowe na Slaa watoe maelekezo.
 
Mbona hata Mbowe na Slaa wameshapokea pesa nyingi tu kutoka kwa kada wa CCM, na wao wapo kundi lipi?

Anaebisha nnaweka ushahidi kinaga ubaga.
 
Marando amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe na hatua zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu na majina ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.
Amesema kuwa pia wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi muda wa maongezi zaidi ya shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.

Unajua kwanin kakataa kutoa namba za simu?kwa sababu waandishi wa habari wangefuatilia hizo namba wangejua kuwa ni magumashi.

Kama hujaushtukia huu mchezo bado huzijui siasa za kitoto za Chadema.
 
huyu mlinzi nae kilaza tu,alitakiwa awe na line special kwenye cell phone special kwa ajili ya kutoa siri za Chadema tu,halafu hiyo cell phone alitakiwa aifiche na lazima yeye ambip kwanza Mangula halafu Mangula ndo ampigie.halafu ujinga wa kupanda gari lenye number,bora hata angekuwa anatumia bajaji halafu anapiga sungogoz,au anavaa hijabu kabisa ile ya kufunika pote na anakuwa kama demu.Nyie CCM Endeleeni kutafuta watu huko CHADEMA ili wawape siri za adui yenu,wanananunulika hao wana njaa,Maana Mbowe na Slaa wanajikopesha ruzuku peke yao tu

Hizo hadithi tu ndugu...riwaya ya kufungulia mwaka.

Hivi toka mwaka uanze Dr Slaa amewahi kuwa front page ya gazeti lolote zaidi ya Tanzania Daima?sasa hii ni namna mojawapo ya kujaribu kurudi kuwa headline kwa hadithi za kutunga na za kitoto.

Na baada ya wiki utaona anaanza ziara kupitia upepo wa "nimenusurika kuuawa".Nakubaliana na Mwigamba hizi siasa za Chadema za kutegemea matukio zinapaswa ziishe.

Wangekuwa hawategemei matukio wasingetengeneza hekaya za Abunuwasi ka hizi za "Phillip Mangula amtuma mlinzi ampe sumu Dr Slaa"...atakayeamini ana matatizo kichwani.
 
huyu mlinzi nae kilaza tu,alitakiwa awe na line special kwenye cell phone special kwa ajili ya kutoa siri za Chadema tu,halafu hiyo cell phone alitakiwa aifiche na lazima yeye ambip kwanza Mangula halafu Mangula ndo ampigie.halafu ujinga wa kupanda gari lenye number,bora hata angekuwa anatumia bajaji halafu anapiga sungogoz,au anavaa hijabu kabisa ile ya kufunika pote na anakuwa kama demu.Nyie CCM Endeleeni kutafuta watu huko CHADEMA ili wawape siri za adui yenu,wanananunulika hao wana njaa,Maana Mbowe na Slaa wanajikopesha ruzuku peke yao tu

Unadhani watonyaji wa mipango wanatoka nje ya wao wanaopanga, kaa kimya kama hujui hao mapaparazi wenu nao si wote wanapenda yafanywayo, wapo wenye uadilifu wao, Mungu awazidishie
 
Ingekuwa ni kweli hilo deal,hawangeweza kuwakamata kwa njia ya simu zao kuzidukua,kwani inafahamika wazi mbinu ya chadema kudukua simu,lazima wangekua na alternative ingine tofauti na hiyo ambayo kila siku chadema wanadai wamenasa mawasiliano.
ndo maana marando hataji namba kwani hazipo
 
Unajua kwanin kakataa kutoa namba za simu?kwa sababu waandishi wa habari wangefuatilia hizo namba wangejua kuwa ni magumashi.

Kama hujaushtukia huu mchezo bado huzijui siasa za kitoto za Chadema.

Umeshupalia huu uzi nadhani, ww utakuwa Mang'ula (maka@!!mo)
 
Ingekuwa ni kweli hilo deal,hawangeweza kuwakamata kwa njia ya simu zao kuzidukua,kwani inafahamika wazi mbinu ya chadema kudukua simu,lazima wangekua na alternative ingine tofauti na hiyo ambayo kila siku chadema wanadai wamenasa mawasiliano.
ndo maana marando hataji namba kwani hazipo

Na amekuwq very trick Marando..hajasema kuwa tumegundua fulani anataka kumuua Dr Slaa bali anasema "ni huyo kijana kasema"..una maana ni maelezo tu ya kijana..wao akuu hilo hawajui na haeana uhakika..maana yake ukienda mahakamani Marando anakuruka kuwa "haaaa..nilisema kuwa fulani amesema..., sio mimi niliyesema kuwa unataka kuua"

Sasa kwa watu waliokubali akili zao washikiwe wanabaki tu wamethibitisha kuwa mauaji yalitaka kufanyika wakati ukimsikiliza hapo Marando anaruka kijanja hiyo...!!utoto kweli huu
 
Unajua kwanin kakataa kutoa namba za simu?kwa sababu waandishi wa habari wangefuatilia hizo namba wangejua kuwa ni magumashi.

Kama hujaushtukia huu mchezo bado huzijui siasa za kitoto za Chadema.

Unajua kutoa namba ya mtu na kuhusisha na jambo lolote ni kosa kisheria? Unakumbuka mwanaha...lisi walivyofungiwa kwa hili?
 
Unajua kutoa namba ya mtu na kuhusisha na jambo lolote ni kosa kisheria? Unakumbuka mwanaha...lisi walivyofungiwa kwa hili?

Kwani ni mara ya kwanza Chadema kutoa namba za watu?wameshatoa mara nyingi sana.

Ila hii wameogopa kwa sababu uongo wake upo hadharani mno..hivyo wakitoa namba ata waandishi tu watagundua ni magumashi na badala ya hii singo kuhit itawarudia wenyewe kuwa ni waongo..ndicho kilichofanya leo wasitoe namba.
 
Taratibu mkuu unaweza kwenda mahakamani kama vipi?
 
Taratibu mkuu unaweza kwenda mahakamani kama vipi?

Nani aende mahakamani?na ukamshtaki nani wakati Marando kasema yeye hahusiki bali ni huyo kijana...??kwa maelezo hayo kama kuna mtu atawapeleka mahakamani basi ni huyo kijana kudai mafao yake na kudai fidia ya kudharirishwa na bila shaka alipigwa na kuteswa.

Lakini Mzee Mjamaa, mzalendo na Muadilifu Phillip Mangula hana ata hizo pesa za kulipa mawakili wale bure tu kwa sababu kuna chizi mmoja amekimbia na nguo zake...atawasamehe bure tu mtu wa Mungu yule.
 
Wana JF

Tuliwaahidi kuwaletea updates za taarifa kamili na sahihi kuhusu siri za mipango ovu iliyokuwa ikipangwa na 'watawala' dhidi ya CHADEMA...

Hapa chini ni updates zilizotokana na press conference iliyofanyika leo Makao Makuu ya Chama, ambapo mzungumzaji mkuu alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Wakili Mabere Marando.

Updates

Kupitia kwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Wakili msomi Mabere Marando, chama kimetoa taarifa kwa umma juu ya njama zilizokuwa zikipangwa na viongozi wakuu wa CCM wakishirikiana na baadhi ya watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya CHADEMA ikiwemo kumdhuru Katibu Mkuu Dk. Slaa kupitia kwa aliyekuwa mlinzi wake, Khalid Kagenzi.

Mwanasheria Marando, mwenye uzoefu wa masuala ya ushushushu, amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa muda mrefu CHADEMA kimekuwa kimekuwa kikilalamika kwa ushahidi kuhusu vyombo vya dola kushirikiana na CCM kukihujumu CHADEMA, suala ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Mabere amesema kuwa kupitia ‘intelligence' ya chama, CHADEMA kimenasa siri za mipango ovu iliyokuwa ikipangwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula na baadhi ya watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa (majina yanahifadhiwa kwa sasa) wakimtumia mlinzi huyo wa Katibu Mkuu kwa ajili ya;

1. Kupata habari za chama

2. Kumshawishi kupanga njama za kumuua Katibu Mkuu Dkt. Slaa

Baada ya ufuatiliaji wa muda sasa ambao ulibaini kuwepo kwa mawasiliano yasiyokuwa ya kawaida ya mara kwa mara kati ya maofisa kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa na Mangula kwenda kwa Kagenzi, ambapo ilibainika kwamba Mzee Mangula amewahi kumtumia Kagenzi fedha kwa njia ya simu, mara mbili.

Siku ya Ijumaa akiwa na Katibu Mkuu nje ya ofisi kwa majukumu ya kikazi, Ndugu Kagenzi alikuwa akimwacha katibu mkuu kwenye kikao ‘alichepuka' na ushahidi unaonesha kuwa alikwenda pembeni kuwasiliana na mmoja wa hao maofisa wa usalama.

Siku hiyo hiyo, baada ya kurejea ofisini, Kagenzi aliomba ruhusa ya kwenda nyumbani, lakini upo ushahidi unaoonesha kuwa hakwenda nyumbani kama alivyoaga bali alikwenda eneo la Morocco- Kinondoni ambapo alimpigia simu ofisa wa usalama yule yule waliyekuwa wakiwasiliana mapema kisha wakakutana naye.

Ofisa huyo wa usalama anasifika kwa mipango ya kuua watu.

Baadae Kagenzi alionekana akichukuliwa na ofisa huyo (msaidizi wa DSO katika moja ya mikoa ya kipolisi Dar es Salaam) kwenye gari aina ya Land Cruiser GX yenye nambari za usajili T 213 ARS, ambayo ilimpeleka hadi nyumbani kwake Tandale.

Jitihada za watu wa usalama wa chama kulifuatilia gari hilo zilizuiwa na gari moja lililokuwa na nambari za magari ya serikali, ambapo dereva wa gari hilo lilionekana kuwa linafanya ‘cover up', alianza kuwauliza maswali watu wa CHADEMA lakini katika namna ya kuwazuia wasiweze kuendelea kuifuatilia ile gari iliyombeba Kagenzi.

Baadae iligundulika kuwa gari ile iliyombeba Kagenzi ilikuwa inafanyiwa ‘cover up' na magari matatu ili isiweze kufikiwa iwapo inafuatiliwa!

Siku ya Jumamosi (jana), chama kiliendelea na uchunguzi wa kukusanya ushahidi zaidi juu ya mwenendo huo wa mipango ovu dhidi ya chama na viongozi wa chama ambapo kililazimika kumhoji mtumishi huyo Bw. Kagenzi; ambaye mbali ya kukiri kushiriki njama hizo pia katika mawasiliano yake ya simu na notebook yake kulikutwa namba za simu za maofisa mbalimbali wa usalama waliokuwa kwenye mpango huo pamoja na Mangula mwenyewe, zikiwa zimetunzwa kwa majina ya ‘bosi'.

Alikuwa anawasiliana na jumla ya maofisa usalama wapatao 22 kwa ajili ya kazi hiyo maalum.

Ushahidi uliopatikana umeonesha kuwa siku aliyobebwa katika gari hiyo alikuwa ametakiwa kupeleka nyaraka mbalimbali zikiwemo za benki, ambazo zingetumika kumuingiza katika utaratibu wa malipo kwa kiwango cha Tsh. 500,000/= kwa mwezi.

Marando amesema kuwa chama kimemkabidhi Kagenzi kwa Jeshi la Polisi, Kituo cha Oysterbay kwa ajili ya hatua za kiuchunguzi na kisheria kutokana na tuhuma hizo.
 
Nani aende mahakamani?na ukamshtaki nani wakati Marando kasema yeye hahusiki bali ni huyo kijana...??kwa maelezo hayo kama kuna mtu atawapeleka mahakamani basi ni huyo kijana kudai mafao yake na kudai fidia ya kudharirishwa na bila shaka alipigwa na kuteswa.

Lakini Mzee Mjamaa, mzalendo na Muadilifu Phillip Mangula hana ata hizo pesa za kulipa mawakili wale bure tu kwa sababu kuna chizi mmoja amekimbia na nguo zake...atawasamehe bure tu mtu wa Mungu yule.

mbona unatunisha sana kifua tulia usicheze na chama cha mtei hata nyerere alikiogopa mkipanga usiku asubuh tuna taarifa
 
Back
Top Bottom