Taarifa kuhusu kuahirishwa kwa hoja ya binafsi ya ajira kwa vijana ya Mh. Mwigulu Nchemba

Dr. Mwigulu Nchemba

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
416
2,037
TAARIFA KUHUSU KUAHIRISHWA KWA HOJA YANGU YA AJIRA KWA VIJANA.

mwigulu-nchemba-feb01-2013.jpg
Kutokana na kukatishwa kwa Bunge linaloisha Tar.6/09/2013 badala ya Tar.13/09/2013.Napenda kuwajulisha Watanzania wenzangu wote kuwa,hoja yangu binafsi ya AJIRA KWA VIJANA itaingia kwenye shughuli za Bunge lijalo.
Nawashukuru vijana wote waliotoa maoni/mapendekezo tayari kuhusu hoja hiyo,Lakini naendelea kupokea maoni na mapendekezo ya hatua za muda mfupi na mrefu kuhusu tatizo la ajira kwa vijana chini.
Unaweza kunitumia maoni/mapendekezo yako kupitia hapa kwenye ukurasa wa Facebook(comments au Inbox text),Pia unaweza kunitumia kwa Email yangu mwigulunchemba@yahoo.com.
Asante sana kwa ushirikiano wenu.
Mwigulu Lameck Nchemba
Mbunge wa Iramba Magharibi,
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Tanzania Bara
Mungu Ibariki Tanzania.

------------------------------------------------------------------------

HOJA BINAFSI NINAYOKUSUDIA KUIPELEKA BUNGENI KUHUSU AJIRA KWA VIJANA HII HAPA.

*Kutokana na maombi mengi ya Watanzania wenzangu kutaka kuiona hoja yangu binafsi ya AJIRA KWA VIJANA ninayokusudia kuipeleka mbele ya Bunge tukufu la nchi yangu Tanzania.Nimeamua kuwapa nafasi muisome ili muweze kuchangia maoni na mawazo yenu vyema kwenye hoya hii.

Nawaomba sana muisome hoja hii kwa makini na utulivu kabisa kabisa ilimuweze kuchangia mapendekezo/mawazo/maoni yenu mapema kabla haijapelekwa kwaajili ya Bunge lijalo.

HOJA BINAFSI YA NDG MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU

{MBUNGE WA IRAMBA MAGHARIBI (CCM), KUHUSU AJIRA KWA VIJANA 2013



Mheshimiwa Spika, Nakushukuru kwa kunipa fursa hii, ya kuwasilisha hoja yangu katika Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika,
Baada ya kuleta hoja inayotafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili vijana wawapo masomoni (Bunge la 10), kwa kuitaka serikali kuleta mabadiliko ya sharia na kuanzisha MFUKO WA ELIMU YA JUU alimaarufu vyuoni kama MFUKO WA MWIGULU, Leo hii nakuja na hoja ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo linalowakabili vijana wamalizapo masomo katika ngazi mbalimbali yaani shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi, mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa na vyuo vikuu. Ukweli ni kwamba, maisha ya wahitimu wengi yanakuwa magumu sana waingiapo mtaani kuliko walipokuwa masomoni, pia kupata kazi imekuwa mtihani mgumu kuliko kufauli mitihani ya shuleni. Hoja yangu inakusudia kuliomba Bunge lako tukufu, liazimie kwa kauli moja, kuitaka Serikali kuleta bungeni Mpango mahususi wa Ajira kwa vijana.

Mpango;

(1) Utakayowezesha kuwepo kwa MKAKATI wa muda mfupi wa kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana;
(2) Utakayowezesha kuwepo kwa MKAKATI wa muda mrefu wa upatikanaji wa ajira kwa vijana;
(3) Utakayowezesha MKAKATI wa makusudi wa kubainisha fursa na kuwezesha vijana kujiajiri.
Mheshimiwa Spika,
Msingi wa hoja yangu ni ukubwa wa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana kwa sasa na tunakoelekea, mipango iliopo na ilioendelevu havilingani hivyo havitoi matumaini ya kutosha kwa vijana katika kupunguza madhara yanayojitokeza kutokana na kukosekana kwa ajira kwa vijana hususani watoto wa masikini kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika,

• Jitihada za serikali za kupanua wigo wa elimu ya msingi, elimu ya Sekondari kwa kujenga shule za Sekondari kila kata na na Vyuo vya Ufundi kila Wilaya kama ilivyo nia ya serikali imeongeza idadi ya vijana wanaomaliza kidato cha nne na mafunzo ya ufundi (VETA) ambao hawaendelei na high school wanaoingia mtaani kutafuta ajira na kutafuta kujiajiri.
• Shule za msingi zimeongezeka tokea 10,927 (1995) hadi shule 16,331 (2012), Shule za Sekondari zimeongezeka tokea 595 (1995) hadi shule 4,528 (2012). Vyuo vya elimu ya ufundi vimeongezeka tokea 16 (1995) hadi shule 248 (2012), Vyuo vya vya elimu ya ufundi stadi vimeongezeka tokea 343 (1995) hadi shule 750 (2012) na Vyuo vya ulimu vimeongezeka tokea 31 (1995) hadi shule 105 (2012).
• Uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi umeongezeka tokea 3,877,643 (1995) hadi 8,247,172 (2012). Uandikishaji wa wanafunzi wa shule za Sekondari umeongezeka tokea 196,375 (1995) hadi 1,884,272 (2012). Wachuo wa Vyuo vya elimu ya ufundi wameongezeka tokea 4,820 (1995) hadi 112,447 (2012) na Wachuo wa Vyuo vya vya elimu ya ufundi stadi wameongezeka tokea 28,560 (1995) hadi 121,348 (2012). Wachuo wa vyuo vya ulimu wameongezeka tokea 13,381 (1995) hadi 43,258 (2012). Takribani wahitimu 6,789,953 kila mwaka wa daraja hili wanaingia mtaani kutafuta kazi. Hii ni nguvu kazi inayopotea ("Bomu linalosubiri kulipuka")
• Jitihada za serikali za kurejesha uzalendo wa vijana kwa Taifa lao kwa kurejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) imeongeza idadi ya vijana wanaohitimu JKT kwa mujibu wa sheria na kwa kujitolea. Tunakoelekea wachache tu watapata fursa ya kuajiriwa na vyombo vya ulinzi na usalama na wengine watakuwa wanajeshi bubu wenye mafunzo kamili ya kijeshi na historia tofauti za maisha yao wakiwa mtaani bila matumaini. Takribani wahitimu 60,000 hadi 100,000 kila mwaka wanahitimu mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria na kwa kujitolea na kuingia kwenye soko la ajira. Hii ni nguvu kazi inayopotea ambayo ("Bomu linalosubiri kulipuka" na hili ni bomu baya sana kwa mazingira ya sasa yenye watu wenye fani za uchochezi).
• Jitihada za serikali za kupanua wigo wa elimu ya juu kwa kuongeza vyuo vikuu kuvipandisha hadhi baadhi ya vyuo kuwa vyuo vikuu vya serikali na vyuo binafsi umeongeza sana idadi ya wahitimu. Vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki vimeongezeka tokea vyuo 12 (1995) hadi vyuo 49 (2012) na kusababisha ongezeko la udahili wa wanafunzi tokea 9,042 (1995) hadi 166,488 (2012). Nia njema ya serikali ya kuwa na Taifa la wasomi wengi wa ngazi ya stashahada, shahada, shahada za uzamili na uzamivu zimeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wahitimu nchini na umeongeza idadi ya wahitimu kwenye soko la ajira serikalini na kwenye sekta binafsi. Takribani jumla wahitimu 6,954,441 kila mwaka wanaingia mtaani kutafuta kazi. Hii ni nguvu kazi inayopotea ambayo tumeipa jina la "Bomu linalosubiri kulipuka"

Mheshimiwa Spika,

Maadam tumeshayajua mabomu haya yanayosubiri kulipuka hatuna haja kusubiri mabomu mpaka yalipuke bila kuyategua. Naliomba bunge lako tukufu liridhie mapendekezo yangu ninayopendekeza na srikali iyafanyie kazi haraka ili kuleta dhana halisi kuwa vijana katika nchi yeyote ni NGUVU KAZI YA TAIFA. Ni dhahiri kuwa vijana hawa hawawezi kuajiriwa wote serikalini, wala hawawezi kujiajiri wote hata kwa sekta binafsi kwa mazingira ya sasa. Naleta mapendekezo ya namna serikali inaweza kupanua wigo wake wa ajira kwa vijana serikalini na kupitia sekta binafsi.
Mheshimiwa Spika, Kwa upande mmoja

(1) Hakuna ofisi hata moja imetimia idadi ya watumishi kulingana na ikama zilivyoainishwa kwenye miundo ya ofisi. Taarifa hizi nimezipata wakati viongozi wa mashirika ya umma, wizara na idara mbalimbali kwa nyakati tofauti walivyoelezea vikwazo vya ufanisi katika ofisi zao wanapotembelea kamati.

(2) Kuna watu wengi sana wana kaimu nafasi mpaka wengine wana kaimu nafasi zilizokuwa zinakaimiwa yaani anakuwa Kaimu, Kaimu Afisa Utumishi, Kaimu, Kaimu Afisa Mipango nk na nafasi yake. Hivyo hizi ni nafasi tatu kwa mtu mmoja, hii inabana fursa kwa vijana wengine kupata nafasi ya kulitumikia Taifa na inapunguza ufanisi kwa kuwa watu hawa wanaogopa kufanya maamuzi.

(3) Kuna watu wanapewa ajira za mikataba na wanaongezewa mikataba kwa kigezo kuwa hakuna mtu anayeweza kuziba nafasi hiyo au hakuna mwenye uzoefu. Hii inaashiria kuwa kuna gap katika kuandaa vijana maofisini katika nyanja mbalimbali kwa wakati kiasi kwamba mpaka mtu anastaafu bado kunakuwa hakuna kijana aliyetayarishwa kwa kazi hiyo. Hii inapunguza ufanisi na kunyima fursa kwa vijana kubobea kwenye kazi na kulitumikia Taifa.

Mheshimiwa Spika,

Kwa upande mwingine; Wakati haya yakitokea kuwa kila ofisi haijatimia ikama yake ya watumishi, watu wana kaimukaimu na watu kuopewa ajira ya mikataba baada ya kusitaafu na kuongezewa mikataba,

(1) Kila mtaa kuna kijana au vijana wahitimu wana miaka (2) hadi (4) hawana kazi wanazunguka na bahasha zenye maelezo yao binafsi,
(2) Kila mtaa vijana wapo wakiomba kazi wanaambiwa hawana uzoefu wa miak miwili (2) au mitatu (3) na wakati mwingine hata mine (4) na matangazo ya kazi karibu yote tu masharti yanafanana hata katika ngazi za ofisa wa madaraja ya chini.
(3) Hakuna chuo kinafundisha uzoefu, hakuna utaratibu wa kuwafanya vijana kupata uzoefu kabla ya kuajiriwa kazi rasmii, kwa kijana wa chuo wa sasa hata pa kufanyia mafunzo kwa vitendo wakati wa likizo nayo ni kazi ngumu sana, ofisi zingine hata kijana wa kujitolea hawapokei.
(4) Wakati kila ofisi haijatimiza idadi ya watumishi, haipokei vijana wa mafunzo kwa vitendo na wakujitolea.
(5) Vijana wapo na stashahada, shahada wamekaa miaka miwili (2) hadi mine (4) na vyeti vyao wanasubiri kazi, hawana namna hata ya kujikumbusha walichosoma wala kuendelea na elimu kwa kipindi ambacho amesubiria angejishikiza mahali kwa kipindi angeweza kupata fedha ya kuendelea na masomo zaidi kabla hajapata kazi ya kudumu. Kijana mwenye stashahada kusubiri kazi miaka mitano maana yake angeendelea na masomo angeshavuka shahada

Mheshimiwa Spika,

Kufuatia hali hii; Vijana wenzangu wamekuwa sasa ni bomu linalosubiri kulipuka ili hali vijana ni nguvu kazi ya taifa, vijana wana msongo wamawazo (Stress), wamekata tamaa hawaioni kesho yao na ya Taifa lao (Future), wengine wanahasira sana na kila mtu na Wengine ni wahitimu ila wanatunzwa na wazee ambao uwezo wao ni mdogo au umeishia kwenye kuwasomesha hivyo wazee nao kuwa na mzigo mzito katika kipindi walichokuwa wanastahili kupumzika.
Mheshimiwa Spika, Mpango wa muda mfupi wa kusaidia wahitimu ni kwa Serikali kufanya sensa ya wahitimu wasio na kazi sasa, kufanya tathimini ya maoteo ya wahitimu watakaokosa kazi na wanaokaribia kustaafu katika kipindi kijacho na kuziangalia ikama katika ofisi za wizara, idara mbalimbali, mashirika ya umma, tawala za mikoa na serikali za mitaa ili,

(1) Serikali ifanye mgawanyo wa vijana kwenye nafasi za kazi zilizo wazi kufuatanza na ujuzi wao,
(2) Serikali iangalie namna ya kulinda ajira ndani ya nchi kwa ajili ya wazawa kwa kazi zisizohitaji ujuzi maalum. Ilivyo sasa kuna utamaduni umeenea kwenye mabenki ya biashara, makampuni ya simu, viwanda mbalimbali, migodi, ujenzi, mahoteli ya kitalii, shule binafsi na vyuo binafsi kujaza wafanyakazi wakigeni. Wengine wana ujuzi wa chini kuliko watanzania, wengine kingereza tu na wengine wakitumi kigezo kuwa watanzania ni wavivu, mhe spika uvivu ni hulka ya mtu mmojamoja sio wa watanzania wote.
(3) Serikali ianze kufanya attachment kwa vijana wapate uzoefu maofisini na hata kuwalipa nusu ya mshahara wa afisa aliyeajiriwa ili kuondokana na tatizo la kukosa uzoefu ambao imekuwa kigezo punde kijana aombapo kazi. Vijana wawe tayari kujitolea kulipwa hata nusu ya mshahara wa afisa ili wapate uzoefu. Kampuni zote, mashirika ya umma na idara za serikali zenye wajiriwa zaidi ya 50 zitakiwe kuchukua vijana wa kujitolea angalau 3% ya watumishi wote ili wapate uzoefu na ofisi ipate fursa ya kujua uwezo wao.
(4) Serikali iangalie upya namna inavyoandaa vijana (Succession Plan), kila alipo mtumishi anayekaribia kustaafu pawepo na vijana wawili ama watatu wanaotayarishwakuondokana na swala la mtu kuongezewa mkataba kwa kigezo kwamba hakuna mtu mwenye ujuzi huo.
(5) Pia kuna umhimu serikali kuangalia upya program walizosoma baadhi ya wahitimu ambao wameshakaa muda mrefu zaidi na kuwapeleka wakasome ngazi ya juu zaidi. Kwa mfano vijana waliomaliza stashahada na kukaa miaka (3) hadi (5) kusubiri ajira ni muda ambao wangeshapata shahada zingine.
(6) Ukubwa wa tatizo la ajira kwa ngazi za vijiji, wilaya, mikoa na kitaifa na mpango mahususi kwa kila eneo tajwa haujabainishwa. Kuna umhimu wa kuanzisha mamlaka itakayo shughulikia tatizo la ajira yaani Tanzania Employment and Unemployment Agency (TEUA) kukidhi ukubwa wa tatizo kuliko kuwa tu na kitengo katika idara ya Wizara.
(7) Program ya mafunzo kazini ianzishwe na iratibiwe na idara Mamlaka hiyo tajwa kwa mandishi na kila kampuni, mashirika ya umma au idara itoe nakala kwenye mamlaka na wizara ya kazi na ajira. Vijana hao wanaopata attachment walipe nusu mshahara na wakimaliza wapewe vyeti vya utambuzi kulingana na uwezo walioonesha. Fedha za kuwalipa zikatwe kwenye kodi ya ajira (SDL) kwa mwajiri mwenye watumishi zaidi ya 50 ili kutoa fursa kwa wajiri wadogo kutengeneza ajira.

Mheshimiwa Spika,

alama anazozipata mtu darasani kwenye mitihani zilizoko kwenye vyeti na uwezo halisi wa kazi wakati mwingine ni vitu viwili tofauti, serikali ikiwachukua vijana hata kwa kujishikiza maofisini itambua uwezo wao halisi na itaacha kuongezea wastaafu mikataba kwa vigezo kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo.

Mheshimiwa Spika,

natambua kuwa kuwachukua vijana wajishikize ni gharama lakini napendekeza Serikali ibane matumizi yake katika baadhi ya maeneo ambayo hayana athari katika ufanisi wa serikali.

Baadhi sehemu za kukata matumizi ya serikali bila kuathiri kazi za serikali ni kwenye ni;

(1) Magari, matenegezo ya magari na mafuta ya magari. Unakuta bosi anaishi Bunju halafu dreva wake anaishi gongolamboto halafu ofisi posta, au bosi anaishi kiluvya na dreve wake anaishi dreva mbagala ofisi posta. Kila siku trip hizo zinatumia mafuta mengi na uchakavu mwingi
(2) Pia abjeti za mafunzo nje ya nchi kwa watu wanaokaribia kustafuu ni ghali hivyo fedha hizo na mafunzo hayoyangeelekezwa kwa vijana. Mfano mtu mwenye mika 59 anapokwenda mafunzo na kutumia fedha nyingi pamoja na kwamba elimu haina mwisho ni kuwanyima fursa vijana.
(3) Sehemu nyingine ya kuifanyia kazi fedha zielekezo kwenye vijana wanaojishikiza ili wajifunze ni kubana Mmianya ya mishahara hewa. Taarifa ya mdgibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kila mwaka huonesha kuwa ofisi nyingi zinawatumishi hewa na wanalipwa mishahara hewa.

Mheshimiwa Spika,

Mpango wa muda Mrefu,

(1) Serikali ije na mpango wa kuwezesha sekta binafsi kuanzisha viwanda na baadhi ya ofisi za serikali kuwa na viwanda vya kimkakati nchini kwa kila ukanda ili kuachana na kuuza nje ya nchi mazao yakiwa ghafi ili kuchochea uzalishaji na kutengeneza ajira. Mfano Viwanda vya Pamba (Kanda ya ziwa , (the Sukumaland), Alizeti kanda ya Kati, Viwanda vya matunda mkoa wa Tanga, Viwanda vya Korosho Mtwara na Lindi, Viwanda vya Nyama Shinyanga, Tabora na Simiyu, Viwanda vya magunia Tanga)
(2) Serikali ije na mpango utakaowezesha wa kufufua viwanda vyote nchini vilivyokufa na kuweka mkakati wa kusaidia wale wenye viwanda vinavyozalisha vifanyekazi katika kiwango stahiki, Viwanda vyote kwenye miji na majiji vichukuliwe kuwa ni viwanda vya kimkakati viwezeshe kufanya kazi kwa kiwango stahiki (Full Capacity) ili kuweza kutengeneza ajira kwa vijana wa mijini.
(3) Serikali pia ije na mkakati wa upatikanaji wa masoko ya uhakika ya bidhaa zitakazotokana na viwanda hivi KUCHOCHEA KILIMO kwa kuwezesha mazao haya kupata bei itakayomtoa mkulima kwenye dimbwi la umasikini. Pia serikali idhibiti matumizi ya bidhaa za nje ambazo zinaweza kupatikana hapa nchini, mfano nyanya, mbogamboga mahoteli, migodini na kwenye ofisi za serikali.
(4) Serikali itengeneze bajeti ya kimkakati kuwezesha kufufua viwanda au kudhamini mikopo ili kununua mashine za agroprocessing na mashine za kisasa za viwanda vya kutengeneza bidhaa kwa ajili ya matumizi ya ndani au kutenga fedha kudhamini wawekezaji wa sekta binafsi kufanya kazi hayo.
(5) Serikali ishughulikie miundombinu ya viwanda na gharama za uzalishaji ili bidhaa zitakazozalishwa na viwanda vya ndani ziwe na kuuzwa kwa bei ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kumudu na kutoza kodi bidhaa za zinazoagizwa tokea nje ya nchi
(6) Serikali iondoe ukilitimba wa miradi kwenye kuwekeza ama kuanzisha,Hii itasaidia kuepukana na mradi husika kuchukua muda mrefu katika kukamilika kwake na kupelekea ajira kuchelewa kwa vijana.Ukilitimba kwenye uanzishwaji wa miradi inaweza kumkatisha tama kabisa kabisa muwekezaji na kupelekea kukosa fusa za ajira kwa vijana
(7) Kudhibiti rushwa kwenye uwekezaji wa kuanzisha miradi inayoweza kutoa fusa za kazi na kusaidia upatikanaji wa ajira.Serikali idhibiti wa uvujaji wa fungu linalotengwa kwenye miradi na kuishia kwenye mikono ya watu wachache,hii itasaidia kupata mradi husika kwa wakati na wenye kiwango stahiki na hatimaye kusaidia upatikanaji wa ajira kwa wakati.

Mheshimiwa Spika,

Fursa ya viwanda kutengeneza ajira kwa wahitimu vyuo vikuu, sekondari, vyuo vya ufundi na Jeshi la Kujenga Taifa na kutegua kabisa bomu linalotajwa kusubiria kulipuka ni kubwa nani jambo linalowezekana iwapo dhamira ya thati na utayari wa kufanya hivyo sasa ukiwepo.

Kwa mfano,

(i) Zao la pamba likiwezeshwa kulimwa kwa mbegu za kisasa, pamba ikahifadhiwa kwa maghala ya kisasa, ikachambuliwa kwa ginneries zenye mashine za kisasa, na nyuzi zitumike kushona nguo kwa kutumia viwanda vya nguo vya kisasa vyenye mashine za kisasa zenye hadhi kama ileile ya viwanda vya china. Soko lake la kwanza iwe kutengeneza sare za wanafunzi wote wa shule za Msingi wapatao 8,247,172 kila mwaka, sare za wanafunzi wote wa shule za Sekondari wapatao 1,884,272 kila mwaka, sare za wanafunzi wote wa vyuo vya ualimu na uuguzi wapatao 329,311 kila mwaka, sare za vijana wanaoingia JKT kwa mujibu wa sharia na wa kujitolea wapatao 350,000 kila mwaka, Sare za Polisi wote na sare za wanajeshi wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Vilevile viwanda hivyo vinaweza kutengeneza mashuka kwa ajili ya vituo vya afya vyote nchini, hosipitali zote za wilaya, mikoa hospitali teule na za rufaa pamoja na baadhi ya mavazi yanayotumiwa na jamii zenye mavazi ya asili kama wambulu, wamasai na wasukuma.
(ii) Viwanda vyote vya ngozi vifanye kazi ipasavyo na viatu vyote vya wanafunzi, Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania vitokane na ngozi ya Tanzania na viwanda vya Tanzania na kuuza katika soko la nchi jirani.
(iii) Viwanda vya magunia vifanye kazi katika kiwango stahiki na magunia yote nchini yatokane na mkonge na viwanda vya hapa nchini.
(iv) Viwanda vya korosho vifanye kazi kwa kiwango stahiki ili kusiwepo kabisa na korosho ghafi inayosafirishwa na kuuzwa nje
(v) Zao la alizeti litiliwe mkazo na kuwe na kiwanda cha kisasa cha kukamua mafuta (Double Refinery) kanda ya kati (Singida) ziwepo pembejeo, mbegu za kisasa, maghala ya kisasa na mafuta ya kutosheleza soko. Kwa sasa mafuta ya alizeti ni asilimia 15 tu ya mahitaji ya mafuta nchini
(vi) Viwanda vya kutengeneza juice itokanayo na matunda mkoa wa Tanga na Pwani vifanye kazi kwa kiwango stahiki ili kuchochea kilimo na kutengenezaajira kwa vijana
(vii) Mazao ya misitu kama mbao yatengenezewe hapa nchini ili mbao zote, samani za maofisini na madawati ya shule zote na vyuo yatokane na viwanda vya ndani na
(viii) Viwanda vingine kama nyama, samaki, kahawa nk

Mheshimiwa Spika,

mkazo katika uzalishaji, uongezeaji thamani, utengenezaji wa bidhaa yenyewe na kuuzwa katika soko la uhakika la ndani kama nilivyoahinisha utachochoea uzalishaji nahivyo kutengeneza ajira nyingi kwa makundi ya vijana niliyoyaainisha. Kuna watakao hamasika kulima Sana zao kutokana na bei nzuri na soko la uhakika, kuna watakaohusika na biashara, kuna watakaoajiriwa viwandani.

Mheshimiwa Spika,

moja ya matatizo tunayokumbana nayo mpaka tukafika hapa ni kukosekana kwa uadilifu kwa baadhi ya watanzania waliopewa jukumu la kuendesha viwanda hivyo enzi viko serikalini. Viwanda hivi vilipopobinafsishwa kwa watu binasfsi vimekutana na tatizo lingune kuwa wengi wa waliochukua viwanda hivyo wanahusika na uuzaji wa bidhaa hizo nje hivyo kukosa msukumo wa kuviendeleza viwanda hivyo na badala yake kuvigeuza godauni la kuhifadhii malighafi kabla hawajasafirisha zikiwa ghafi kwenda nje.

Kwa kuwa ni watu binafsi na wengine ni watu binafsi na wabinfsi hawana utashi wowote wa ajira zinazopotea kwa kufunga viwanda, kodi inyopotea kwa Taifa na athari kwa kupunga kwa uzalishaji wa zao husika kutokana na soko kutokuwa la uhakika, maadam wao wana godauni na wanasafirisha nje mazao wanayoyakusanya.

Mheshimiwa Spika,

Kama mtu alipewa aridhi kwa ajili ya kuiendeleza badala ya amebadili matumizi na kuanza kukodisha ama ameiacha bila kuiendeleza, hakuna sababu ya mtu huyo kuendelea kubaki na aridhi hiyo kwa kosa hilo la kukiuka mkataba. Kuna uhitaji mkubwa wa ardhi iliyotengwa kimkakati kutumika ikaleta uzalishaji ana ikaleta ajira. Kama mtu alipewa kiwanda na imepita miaka kadhaa hakiendelezi wala hakizalishi amekifunga ama hata kufanya godauni hana haja ya kuendelea kuwanacho anyang'annywe kwa kosa hilo la kukiuka mkataba.

Mheshimiwa Spika,

serikali inaweza kuchukua viwanda vyote vilivyokufa, vilivyogeuzwa magodauni, vinavyosuasua na mashamba yaliotelekezwa kuendelezwa na yaliobadilishiwa matumizi na kuwa JKT na Magereza na kutumia ardhi kwa tija na kufufua viwanda. Kwa mfano serikali inaweza kuipalipatia JKT viwanda vyote vya nguo wakatengeneze kwa aina zote za sare nilizozianisha mwanzo, serikali inaweza kulwapatia magereza viwanda vya ngozi na mbao na kuwapa majukumu ya kutengeneza viatu na samani nilizo zianisha mwanzo.

Mheshimiwa Spika,

napendekeza Serikali iyachukue mashamba yaliotelekezwa ili iwapatie JKT na Magereza kuwezesha kuzalisha mali ghafi za vitasaidia kuchukua idadi kubwa ya vijana wanaohitimu mafunzo ambao hawaendi vyuoni na wala hawaendi iwandani. Kupanua wigo wa shughuli katika vyombo hivi kutasaidia kuajiri vijana wanaopitia mafunzo ya JkT ambao hawajaajiriwa na vyombo vya usalama kuajiriwa kwenye shughuli za viwandani

Mheshimiwa Spika,

kazi ya mamlaka ya kushughulikia tatizo la ajira itakuwa kujua ukubwa wa tatizo la ajira vijijini, mijini na kitaifa. Kwa kuwa tatizo hili ni kubwa na linaendelea kukua kila mwaka, kuna umhimu wa kuwepo mamlaka itakayo shughulikia kupanga mikakati ya utengenezaji wa ajira, kujua mwelekeo wa wahitaji wa ajira, mwelekeo wa watakao staafu na kubainisha fursa za ajira na fursa za kutengeneza ajira.

Mheshimiwa Spika,

tatizo kubwa wanalopata vijana wakitaka kujiajiri ni mitaji, kutokuwa na dhamana ili wakope, kutokuwa na fedha za kuata washauri wa miradi ya conultants na kutokuwa na ofisi ya kupata ushauri wa mambo ya ujasiliamali. Mamlaka ya kushughulikia ukosefu wa ajira kwa vijana na ajira pia iwe ni ofisi ya ushauri wamambo ya miradi, elimu ya ujasiliamali, udhamini kwa vijana wenye mapendekezo ya miradi ili kufungua mwanya wa vijana wa kujiajiri.

Mheshimiwa Spika,

Mamlaka hii iwe na uhusiano na wanafunzi tangu wakiwa vyuoni ili kujenga utashi (mindset) ya biashara na kujiajiri wakiwa vyuoni. Hali ilivyo sasa wanafunzi wengi wa vyuo wanafika zaidi ofisi za vyama vya siasa, wanashauriwa zaidi na wanasiasa, wanatumiwa zaidi na wanasiasa na wanawaza zaidi siasa na wanaona siasa ndio inaweza kuwabadilishia maisha yao. Mawazo haya na wepesi huu unatokana na ukweli kwamba ofisi rahisi kwa mwanafunzi kufika ni za vyama vya siasa, na washauri ni wanasiasa. Kuna umhimu wa kutengeneza mindset vijana wawe na mawazo ya biashara, wawe na ofisi ya kuwafungua mawazo haya na kuwapitishia maandiko ya miradi yao. Kijana akishakupitishiwa andiko la mradi wake na wataalamu wa mamlaka hii arusiwe kukopa fedha kwa kutumia cheti chake cha masomo na kitambulisho cha uraia kama dhamana.

Baada ya maelezo hayo, naomba sasa niwasilishe hoja yenyewe. Hoja hii inawasilishwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2007, Kanuni ya 54 (i).

(1) KWA KUWA, kuna shida kubwa ya takwimu za vijana wasiokuwa na ajira na namna ya vijana kupata ushauri wa mambo ya miradi, kujiajiri, kupata mikopo na ajira,
(2) KWA KUWA, Ardhi ni mtaji na ardhi ni uwanja wa kutekelezea mpango wowote wa maendeleo,
(3) KWA KUWA, kuna watu walipewa Ardhi kwenye maeneo ya kimkakati (Prime Areas) ili waiendeleze kwa ajili ya uwekezaji na badala yake wameitelekeza au kuibadilisha matumizi na wengine kuwakodishia wananchi,
(4) KWA KUWA, kuna viwanda vilivyobinafsishwa na baadhi vimekufa kabisa, kugeuzwa magodauni au kusuasua kwa kiwango cha kutotokuwa na ufanisi wa aina yeyote hivyo kuikosesha serikali mapato na kuwakosesha vijana ajira.
(5) KWA KUWA, historia inaonesha kuwa serikali iliwahi kuendesha viwanda hivyo na baadhi havikuwa na ufanisi stahiki ndipo ikaamua kubinafsisha, kuvichukua na kuendesha moja kwa moja inaweza ikawa ni kurudia makosa.
(6) HIVYO BASI, naliomba Bunge lako tukufu liazimie kuitaka Serikali, kwa haraka inavyowezekana, ilete Muswada wa sheria bungeni wa kuanzisha mamlaka itakayoshughulikia kutoa ushauri wa vijana kujiajiri, kudhamini mikopo kwa vijana na kushughulikia ajira, Serikali iwanyang'anye wote waliochukua aridhi kwa ajili ya kuiendeleza kiuwekezaji na badala yake wamegeuza matumizi na kuanza kuikodisha wananchi ama hawajaiendeleza kwa jinsi ilivyokusudiwa ili ardhi hiyo itumike kwa uzalishaji wa kimkakati kwa vijana watakaokuwa kwenye sekta ya uzalishaji.

Serikali ivichukue viwanda vyote vilivyokufa na vilivyogeuzwa magodauni na vinavysuasua na kisha ikavibidhi viendeshwe na JKT na Magereza, na vingine wapewe watu wengine wenye nia na uwezo wa kuviendeleza ili viendeshwe kwa nidhamu na kuwa na tija ndani ya nchi. Na serikali iweke wazi sheria ya ukomo wa mtu akibinafsishiwa kiwanda ama kupewa ardhi na kutoendeleza kwa kipindi kinachozidi miaka mitatu apoteze uhalali wa kumiliki.

Mheshimiwa Spika, NAOMBA KUTOA HOJA.
Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (MB)
IRAMBA MAGHARIBI
 
Nothing new ... nothing special .. we need rebirth of our country's status quo ...

ccm is a group of predators
 
Unatupotezea muda tu. Sidhani kama una hoja yoyote ya maana ili Kumsaidia Mtanzania bali unataka kuuza sura yako.Kwa jinsi ninavyosikia mara nyingi siasa zako kwenye majukwaa ya siasa, unaonyesha huna ukomavu wowote. Mwanasiasa wa ngazi yako hapaswi kuwa mtu wa matusi ya namna ile tena ya kienyeji kabisa.

Unapotaka serikali ifanye utafiti kuhusu vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira niliona kama umeanza vibaya. Mlikuwa na ilani ya chama chenu katika uchaguzi wa 2010, je, mliahidi suala la ajira kwa vijana? na kama mliahidi mlikuwa mnawalenga vijana wepi kama mlikuwa hamwafahamu?
 
Huna Lolote wewe!! Umeangalia Upepo ukaona hoja yako haina mashiko imemezwa na cdm ukaona uwithdraw! M4c with no apology.
 
Mkuu Mwigulu Nchemba, ungetuwekea abstract ya hiyo hoja yenyewe ingekuwa vizuri zaidi na ungeweza kupata michango ya maana zaidi. Kusema tu ni hoja juu ya "Ajira kwa Vijana" hakutoi mwanga wowote. Thesis yako ni nini hasa katika suala la ajira kwa vijana?
 
Peleka kuzimu hoja yako. Mnatuona sisi mazu.zu eeh! Hoja ya msingi ya katiba ambayo ndo itatufanya tuwe uhuru wa kiuchumi kupitia rasilimali zetu, nyie mnaiba.ka na kuwahujumu wasema kwel. Halafu unatuletea porojo zako hapa. Humpati mtu hapa.
 
Mna wa bull Wabunge wenzenu nani atakusikiliza!!!. Tafuta avenue ya vikao vya UVCCM ukawadanyie hiyo hoja badala ya kujidai unaongea na waTZ woote ambao wakikuona wanakuogopa kama Konyi.
 
Mkuu Mwigulu Nchemba, ungetuwekea abstract ya hiyo hoja yenyewe ingekuwa vizuri zaidi na ungeweza kupata michango ya maana zaidi. Kusema tu ni hoja juu ya "Ajira kwa Vijana" hakutoi mwanga wowote. Thesis yako ni nini hasa katika suala la ajira kwa vijana?

Alishaiweka hapa awali, lakin ni ya kidumavu mno. Mtu anayetamba kuwa na first class ya uchumi, anapropose kusadikika ni aibu kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Peleka kuzimu hoja yako. Mnatuona sisi mazu.zu eeh! Hoja ya msingi ya katiba ambayo ndo itatufanya tuwe uhuru wa kiuchumi kupitia rasilimali zetu, nyie mnaiba.ka na kuwahujumu wasema kwel. Halafu unatuletea porojo zako hapa. Humpati mtu hapa.

Apeleke upuuzi wake kuzimu, hawa vijana wa ccm wanataka umaarufu na kuwalaghai vijana kwa kisingizio cha ajira, wanajua jinsi ilivyo rahisi kuteka vijana kwa kutaja ajira ambayo ni janga la kimataifa. Alianza kuja na haya mambo kigwangala, huyu naye amekurupuka.
 
Iweke hapa ili uweze kupata mawazo tofauti.

Alishaiweka hapa mkuu hapo kabla, tatizo la hawa viongozi wa ccm wanaamini mawazo yao ndiyo ya mwisho, hata uje na mawazo mazuri kiasi gani kuchangia hoja utatupwa kule.
 
Mkuu Mwigulu Nchemba, ungetuwekea abstract ya hiyo hoja yenyewe ingekuwa vizuri zaidi na ungeweza kupata michango ya maana zaidi. Kusema tu ni hoja juu ya "Ajira kwa Vijana" hakutoi mwanga wowote. Thesis yako ni nini hasa katika suala la ajira kwa vijana?

Na wewe! Una'mbomu' hivyo ati? Unafikiri anaweza akajua maana ya 'thesis' ndani ya mustakabadhi huu? Sidhani!!!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hana Lolote huyu Jamaa; Zaidi zaidi analengo la Kututoa kwenye Burning Issues kama vile, Nchi ya Wauza madawa ya Kulevya na CCM kuibaka rasimu ya katiba; Nonesense. labda utupatie mbinu za Kufabricate case za ugaidi; Ilani ya Chama chako ya Uchaguzi ya 2010, je vipaombele vimetumizwa kama ndo bado mnasuasua na sasa Unajidai kuwa na Machungu ya kutafuta suluhisho la ajira kwa Vijana. Usiwapotezee watu muda wa Kusoma post zenye Kuhabarisha. Zaidi zaidi Unataka kut
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom