System yetu ndo inafanya kila mtu tunamuona fisadi akiapata mafanikio

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
318
Muundo wetu wa serikali ya sasa umeweka mafanikio kwa wasiasa na sio wananchi wa kawaida.

Leo hii waziri o mbunge anaweza akapatiwa mkopo wa hata bilioni 1 tofauti na wananchi wa kawaida kwake inakuwa ngumu kupata huo mkopo kuna njia na vikwazo vingi kuufikia.

System yetu inawabeba wakuregenzi,viongozi kupata mikopo minafuu na hiyo mikopo kuna wengine hawarudishi sasa ukirudi kwenye uhalisia kama mtu ni waziri anaweza kupata mkopo kutoka CRDB o NMB hata milioni 500 mpaka bilioni 1 kwanini watu wasiwaone hawa watu matajiri mtaani

Kwa kutumia huo mkopo anaweza kununua nyumba ya kisasa o kujenga kabisa kufanya biashara zake na kuingiza interest za uongozi wake ndani humo

Kwanini nasema System ndo inachangia leo viongozi wetu wana nguvu kwenye maamuzi kuliko wataalamu ni hao viongozi ambao huwa wanajigawia tenda mbalimbali na kusahau raia.kwa jinsi system yetu ilivyo ni vigumu na ngumu sana kufanikiwa kama utakua mtumishi wa kawaida.

Tunaona viongozi wetu wengi wakifungua mabiashara makubwa wengine wanajenga apartment kila siku hii nikutokana na maisha yao kuwa sio shida sana kupata mikopo mikubwa yenye low interest.ndo maana watu wengi walisoma wanaacha field zao wanaingia kwenye siasa.

System yetu ndo inatufanya tufike hapa kuwa viongozi ndo wataonekana na pesa wao ndo wana haki ya kuuziwa nyumba zile za masaki kwa milioni 20 kipindi cha mkapa
Wao ndo wana haki na kupeana tenda kubwa zote
Wana ndo wana haki hawakatwi kodi
Wana haki na kupewa mikopo na hata wasirudishe
Wana haki ya kupewa 10 percent upate tenda

Tusipobadili huu mfumo hakika hata Chadema wakishika nchi leo kuna watu mtawaona wanakua matajiri wa ghafla tu kumbe system ndo imewabeba.

Kuna tofauti kubwa na mimi na kiongozi
Nikiomba mkopo hata wa milion 500 nitaambiwa ni mali za thamani hizo
Nikiomba tenda unashangaa kapewa kigogo o mtoto wake

System ndo ina haribu mambo kufanya hata wale viongozi wazuri tuwaone wachafu leo hata wataalamu wanawaogopa viongozi

Mfano barabara inatakiwa ijengwe kwa billioni 500 kiongozi anataka ijengwe kwa bilioni 600 wapige ela yao.

System ya sasa ya tz inatafanya wanasiasa na viongozi wabaki kuwa matajari na sisi wananchi wa kawaida tubaki masikini.
Je ni wangapi mna idea nzuri za biashara lakini mnakosa mikopo ya kuendeleza mnakufa na ndoto zenu lakini leo maige waziri aliyeingia bungeni 2005 leo na nyumba ya thamani kubwa ana kampuni ya maroli.

Hata sie tunaolalamika kwa System ilivyo ukipewa uwaziri tu utaonenekana wewe ni fisadi kwasababu maisha yasharahishishwa kwako unaweza kukopa na kupata tenda kibao kwanini sasa usitajirike hapo.

Mytake:
Tubadilishe system yote mtu akiingia kwenye siasa biashara zake apewe mtu kwenye tenda hizi asiingize mkono wake ili ashinde.

Ni wakati wa mabenki kutokopesha na sisi wananchi wa kawaida mikopo yenye riba nafuu na iwe rahisi kupata.

Tanzania ya kweli itabadilishwa na sisi wenyewe wala msitegemee CCM na CDM iwaletee mabadiliko.je ni wangapi humu mnapokea rushwa mna jiongezea posho kila siku makazini halafu mnakuja kulalamika mtu fulani fisadi.

Tuache sisi wenyewe kuiba maofisi kupokea rushwa na ziundwe sheria kali kuhusu hili.



Ni mimi

Majani kv

Kutoka msituni
 
System ndio inakufanya uwe tajiri baada ya kuwa waziri? Mbona kina zakaria hans pope, bakhresa ni matajiri hatuwasemi?
 
System ndio inakufanya uwe tajiri baada ya kuwa waziri? Mbona kina zakaria hans pope, bakhresa ni matajiri hatuwasemi?
Hujanielewa soma vizuri ndo urudi kuchangia system inawebeba watu wa tabaka fulani bakhresa hajaupata utajiri leo ali work hard
 
Leo hii waziri o mbunge anaweza akapatiwa mkopo wa hata bilioni 1 tofauti na wananchi wa kawaida kwake inakuwa ngumu kupata huo mkopo kuna njia na vikwazo vingi kuufikia. [/QUOTE said:
Mkopo hupewi bila vigezo hata uwe RAIS wa JMT
 
Back
Top Bottom