knock knock
JF-Expert Member
- Mar 8, 2018
- 326
- 384
Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa dunia inaihitaji sana tanzania kuliko tanzania inavyoihitaji dunia
Ndivyo munavyoaminishwa na maskio yenu yakapokea kama mlivyopewa, na ata vizazi vyenu mutavijenga katika theory hiyo hiyo lakini sivyo ilivyo, tena huwa munaenda mbali zaidi kwamba sasa Tz itatoa misaada kuzisaidia nchi ya magharibi kwa vile muna visima vya madini ya dhahabu na almasi.
Lakini ukitaka kugundua udhaifu wa hizo hoja na hali sivyo ilivyo mfano ni mdogo tu Juzi waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola alisema mashoga Tz wapo salama kwanini alitamka kauli hii huku akijua dhati kabisa anaenda kinyume na katiba ya nchi iliyoasisiwa tokea miaka 70 na adhabu yake ni miaka 30 jela? Tafsiri yake ni kwamba Tz bado ni tegemezi kwa nchi za magharibi na haina ubavu ata kuonyoosha kidole kutoka kwenye chupa.
Ukiwa unapokea elfu7 kwa siku ni vigumu kujua na kuamini ukweli na uhalisia wa mambo ndivyo mlivyoaminishwa.