Swali

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,514
11,276
Hili swali nimelikuta kwenye Blog ya Dina Marios.

Leo kwenye kipindi tulikuwa na ishu moja ambayo ilipelekea kutokee mjadala ufuatao.Hivi ni kweli kuna wanawake wanakuwa na kismati flani hivi,pindi anapokuwa na mwanaume kimapenzi yule mwanaume hufanikiwa??yaani madili yake,mambo yake yote ya kipesa yanamwendea vyema akiwa na mwanamke huyo tu.Akiachana nae basi mambo yanakwenda mrama!!!!pls wanaume naomba mnisaidie kujua hili kama kweli lipo.
Asante!!!!!

Mtazamo wangu:
Hili suala linawezekana, unapokuwa na mwanamke na mkawa mnaendana vyema kwa maana ya kuishi kwa amani na upendo wa kweli, akili inapata kutulia (stress free) na hatimaye, mtu kuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi sahihi hata kwenye shughuli anazokuwa anafanya. Ikiwa ni kinyume, basi mtu atashindwa ku-concentrate kwenye mambo yake kutokana na muda mwingi kuwaza migogoro yake na mpenziwe au migogoro yake binafsi (intrapersonal conflicts) kuhusu mpenziwe, hali itakayopelekea mtu huyo kufanya vibaya kwenye shughuli zake.
 
Well kua na kismati kupo sana ila inapotokea mtu yuko karibu na mwenzake kiasi cha kuweza kupeana ushauri na kusaidiana majukumu maendeleo yanategemeana na juhudi zaidi!!!Kuna wanaume wengine kwakweli wana potential sema hawana watu wakuwasukuma.....sasa mtu kama huyo akikutana na mwanamke mwenye akili za kumshauri na kumpiga jeki utaona mambo yake yatakavyobadilika!!
Sasa hapo ikitokea yule mwanamke asiwepo tena yule mwanaume atarudia hali yake ya kawaida.....uwezo anao ila msukumo hamna kwahiyo mambo yote yanarudi kama zamani!!

Kuna mada kama tatu hivi tumezijadili kuhusu mwanamke anavyoweza influence maendeleo au hata matatizo ya mwanaume!!Zitafute usome!!!
 
Duh,yaani saa9 tu nahisi njaa kama sijala siku mbili vile na nimekula fresh tu leo
 
Ugumu ni kujua kuwa mafanikio uliyonayo yanatokana na kismati cha mke wako, utajuaje!? Je wale wenye mali lakini wake zao ni vurugu tupu wao vipi!
 
Kuna mada kama tatu hivi tumezijadili kuhusu mwanamke anavyoweza influence maendeleo au hata matatizo ya mwanaume!!Zitafute usome!!!

Kumbe! shukrani...
 
Back
Top Bottom