Swali Tatanishi; Polisi wa Dhahabu Mbona Hawakushtakiwa Kijeshi na Kufukuzwa Kwanza?

Kwa iyo jwtz hawapelekwi mahakaman
Hakuna mahakama za kipolisi au magereza zaidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Polisi hawezi kupelekwa mahakama za kijeshi.Na Mahakama za kijeshi Tanzania zinafanya kazi na wanajeshi wanashitakiwa ila si public hearing.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fanya kitu kimoja tafuta rafiki afsa wa jeshi akupe kitabu kinaitwa volume 1 administration utaona hayo mambo yote yalivyofafanuliwa isije kuwa unabwabwaja tu huku huna evidence
Na wewe tafuta afisa wa polisi mmoja akupatie PGO uisome na uielewe usijekuwa umeshikiwa akili na keyboard and mouse.
 
Umeongea sana uonekane unajua ila wew ni zwazwa bado mzeee tafuta wajuvi wa mambo wakuambie acha kusikiliza maneno ya vijiweni na propaganda mzeee
Simple tu hata google uone kama utaletewa maelezo kuwa kuna mahakama ya kijeshi ya kipolisi. Mahakama za kijeshi ni kwa wanajeshi na hii ni dunia nzima mzee
Chukua polisi waulize je huwa mnamahakama zenu?
Na nikuambie kuwa sio mpaka uwe mwanajeshi tu ndio unaweza kuhukumiwa mahakama ya kijeshi mtu yoyote mwenye kosa ambalo linastahili kwenda mahakama ya kijeshi anapelekwa hasa hasa liwe la uharifu wa kivita au kutishia usalama wa taifa.
Ndo maana hata uganda bobby wine walitaka mpeleka kule
Na unaposikia jeshi la ulinzi wa wananchi wa Tanzania usizani heti polisi sijui magereza wanakuwa include bro acha kujipotosha
Kumbukia speech ya mwinyi bungeni
Na lazima ujue majukum ya jeshi na ya polisi ni tofauti kabisaa hata training zao hawa wanafundishwa sana. Kudeal na raia hawa maadui hata zile mbwembwe za ffu lengo ni kudhibiti raia na wahalifu sio kupigana vita mzeee
By daway kwa kukusaidia saka kitabu cha kijeshi volume 1 utaona maelekezo kila kitu labda utaacha kuaminj kuwa hujui na hujui kama hujui
Kuna yule polisi wa Uganda Muhammad Kirumira aliyeuawa miezi michache tu iliyopita. Kabla ya kifo chake kuna wakati alikuwa akishitakiwa kwenye "police disciplinary court" na kuna siku alitumia nguvu kuwaingiza waandishi wa habari kwenye mahakama hiyo ili kufanya coverage ya hiyo kesi yake. Je, hiyo mahakama ni ya kijeshi au siyo ya kijeshi?
 
Mijadala/makongamano yanayo fanyika kama haya yana tija ktk jamii kuto onyeshwa ktk vyombo vya habari na wachache kupata taarifa hizi kupitia mitandao ya jamii ni kuwarudisha nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
soma kwanza kanuni za polisi ndipo uje hapa...unadhani akiua hawezi kupelekwa mahakama ya kiraia? Sheria ya makosa ya uhujumu uchumi inasemaje? Inabagua raia? Ninavyofahamu mimi kwa baadhi ya vyombo vya dola, mtu wa chombo cha dola anahukumiwa kwanza kijeshi na kupelekwa mahakama za kiraia
Kuna watu ni vilaza kweli! Sasa usemacho wewe na nilichosema Mimi tofauti nini?
Mshangao wangu ni kuwa Kwa nini hawajalelekwa mahakama yao ili kufukuzwa kwanza?
Maana wameletwa mahakamani wakiwa wamesimamishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna hata mmoja mwenye idea na swali zuri alilouliza mtoa mada ndio wengi wenu mmejibu hovyo!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa wanajua kanuni za askari mkosefu, Huwa anashtakiwa kijeshi kwanza na kufukuzwa kazi kisha ndio anashtakiwa kiraia.

Askari hapelekwi mahakamani ya kiraia kama askari unless sio mashtaka yahusikayo na kazi yake kama ya traffic, ugoni nk.

Sasa imekuwaje askari wa kesi ya hongo na uhujumu uchumi kusimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani?

Kwa maana halisi hao bado ni askari police ila wamesimamishwa tu kazi. Hii ni nini? Au kuna mazingira ya kesi hii kuwa na usanii wa kumzuga mheshimiwa Mzee baba?

Kuna watu watakuja na povu la ushabiki wa kisiasa hapa lakini wekeni akilini Mzigo unahusu 27b na kuna wahindi humor ambao kuwatajia hela ni sawa na kumtajia mgonjwa jehenamu.

Tujiulize sana jee hili limetokea kwa Bahati mbaya kwa sababu ya woga wa Mzee baba kuingilia Kati au lilikuwa arranged scientific?
We upo nchi gani jamaa mbona washafukuzwa kazi toka wiki jana
 
Too sweet to be true!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom