Swali la Msingi: Je Watanzania wanataka kazi ya serikali iwe ni nini?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Tatizo kubwa la Tanzania sio plans pekee bali ni mfumo. Hakuna maendeleo ya maana yatapatikana Tanzania kama Watanzania hawata weza jibu hili swali hapa chini. Cha kushangaza hata hapa wanajamii bado wako nyuma kidogo kwenye hili swala muhimu.

Swali: Je Watanzania wanataka kazi ya serikali iwe ni nini??. Je ni vitu gani hasa tunataka serikali ifanye na vitu gani tunataka serikali isifanye?. Majibu yatatofautiana lakini bila jibu hapa Tanzania itakuwa inapiga danadana tu.

Mfano katiba ya USA inasema: Serikali inatakiwa kufanya vitu ambavyo wananchi hawawezi kufanya wenyewe.

Serikali na hata wananchi wa Tanzania hawajajibu hili swali bado. Hivyo serikali inafanya mambo mengi ambayo kwa mawazo yangu si kazi ya serikali? Mfano ununuzi wa matrekta ungeweza kufanywa na mashirika binafsi kama TFA.Vilevile shughuli kama za mikataba ya mashamba ya biashara ingekuwa inafanywa kwa na wanakijiji kwa msaada wa serikali na si serikali pekee, ATC ni kwanini inaendeshwa na serikali, hospitali karibu zote wafanyakazi ni wa serikali, walimu wa vyuo na shule n.k . Serikali kwa mawazo yangu inafanya mambo mengi kuliko uwezo wake ingenufaisha Tanzania kama wangefanya machache vizuri na mengine yafanywe na sekta binafsi kifanisi zaidi kama ilivyokuwa banks.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom