VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kichama na kiserikali namfahamu Komredi Kinana tangu miaka ya 80. Naujua uhodari wake kijeshi (kwakuwa nami nilitumikia mojawapo ya vyombo vya ulinzi na usalama), kiserikali na kichama. Komredi Kinana si mtu wa maneno mengi. Ni mtu wa mipango ya viwango na vitendo na mwendo.
Sikushangaa pale chama chetu kilipompa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa kutokana na makubwa yake aliyoyafanya akiwa Katibu Mkuu wetu mwaka 2012 hadi 2018. Ilikuwa miaka 6 ya ukada uliotukuka na chama kikasomba ushindi wa kishindo kama cha nyundo mwa 2014 na 2015. Namwamini Kinana.
Lakini, jana Komredi Kinana alitoa kauli yenye kutafakarisha na kuogofya. Aliitoa mbele ya ACT-Wazalendo huko Dar es Salaam. Kwamba, Rais Samia ameahidi, kudhamiria na kuamua kuwa uchaguzi wa mwaka huu na mkuu wa mwakani utakuwa huru na wa haki. Ujumbe wa haraka ni kuwa wananchi wamwamini Rais.
Komredi Kinana, yaani unawaambia wananchi kuwa u-haki na u-huru wa uchaguzi huamuliwa na Rais? Kweli hili la kuwaambia wananchi walioaminishwa tangu dahali kuwa chaguzi zetu ni huru na za haki na huwa CCM yetu tunashinda (na si kushindishwa) kwa haki na kwa Ilani bora? Why Comrade!??
Yaani watanzania, pamoja na kazi yote iliyofanywa tangu uhuru kuwaaminisha kuwa washindi uchaguzini hupatikana kwa haki baada ya taasisi husika kuchakata wagombea na wananchi kuamua, sasa waamini kuwa Rais ndiye mwamuzi wa iwapo au la uchaguzi uwe huru na wa haki? Kwanini lakini?
Komredi Kinana, amini nakwambia, umemwaga mtama kwenye kuku wengi. Ulipaswa kuzitetea taasisi za kiuchaguzi na uhuru wao ambazo huzalisha chaguzi huru na za haki. Rais, pamoja na kuwa kiongozi wetu kichama, kiserikali na kinchi, si mtu sahihi wa kuamua uhuru na uhaki wa uchaguzi.
Nimetafakari na nikakumbuka mbali!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)