Habari zenu wanaJF.
Naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa namna hesabu za malipo ya mikopo benki zinavyofanyika atujuze hapa.
Kwanza inabidi niseme tu kuwa inasikitisha sana kwamba hadi leo hii, huduma kwa mteja kwa taasisi nyingi sana ni mbovu hadi zinatia hasira. Nasema hivi kwa sababu nimejaribu kutembelea benki mbalimbali ili nipate maelezo ya kutosha kuhusu mikopo na hesabu pamoja fomula zinatozumika kukokotoa malipo hayo kuanzia mwanzo wa mkopo hadi pale deni linapokwisha, lakini kati ya benki zote nilizotembelea (NMB, CRDB, TWIGA na KCB) ni KCB tu ndiyo waliojitahidi kidogo kulinganisha na wengine wote kutoa maelezo ya kuridhisha. Cha kushangaza ni kwamba hata hao waliowekwa kushughulikia wateja kwenye haya masuala hawana elimu kabisa kuhusiana na hesabu za makato.
Sasa basi pamoja na kuwa nimepata mwanga kidogo lakini, nitashukuru sana kama kuna yeyote anayeweza kutoa elimu zaidi. Nafanya hivi ili nitakapoamua kuchukua mkopo benki basi niwe ninajua hasa ni kwa namna gani itaniathiri kiuchumi.
Ili kurahisisha swali langu, chukulia kwa mfano mtu analipwa net salary(kiswahili chake sijui) ya milioni moja (1,000,000/=) na amechukua mkopo wa Tshs 12,000,000/= ambao anatakiwa kuulipa ndani ya miaka mitatu na riba ni 20%. Mchakato hapa utakuwa vipi?
Ni hayo tu....
Natanguliza shukrani zangu wadau.