SWALI: Je, ni bora kuwa Specialist au Generalist kwenye biashara?

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Kabla Sijakwambia Chochote kuhusu Mtu kuwa Specialist au Genelalist kwenye Biashara.

Naomba kwanza Nikuoneshe huu MSEMO Mmoja wa Kizungu.

Unaosema Hivi...

"Mtu Anaye Kimbiza Sungura Wawili Hukosa Wote"

Ni Msemo wenye UKWELI Ndani Yake na ni Sawa na huu Msemo wa Kiswahili, Unaosema Hivi

"Mshika Mbili...Moja Humponyoka"

Kama Utakuwa Umesoma kwa Umakini utagundua kwamba...

Watu wote waliosema Misemo Hiyo yote Miwili walikuwa Sahihi kwa Mitazamo yao.

LAKINI...

Ukienda kwa...

"LARRY PAGE"

Mmilikiwa na Muanzilishi wa Kampuni Maarufu ya...GOOGLE

Yeye Anasema Hivi...

Ili mtu awe Mfanyabiashara Makini na Aweze kupata KAZI Kwenye Kampuni yake Anatakiwa awe na Sifa Moja ya Kipekee ambayo Inaitwa...

"T —Shape Character/Person"

Nimekuacha?..

Ondoa Shaka, Nimekuwekea Maelezo yake Hapa Chini

T—Shaped Person Ina maana ya...

Mtu au Watu ambao wana UJUZI wa Vitu Mbali mbali Mwanzoni halafu Kuna Kitu KIMOJA Ambacho amebobea Nacho Zaidi kuliko vyote.

Mfano...

Unaweza Ukawa Wewe ni Mtaalamu wa Maswala ya Picha...

Yaani ni..."PHOTOGRAPHER"

Lakini vile vile una UJUZI wa Ziada kuhusu...

Creativity, Art, Design, Video Production, Communication Skill, Sales & Marketing N.k..

Kwahiyo wewe Huwezi kufanana na Photographer wa Kawaida ambaye anajua...

Colour and Light Setting Tu!

Mkienda kwa Mr. Google Wewe utakuwa chaguo Lake la kwanza Kwa sababu...

T — Shaped People

Huwa wana Faida nyingi zaidi kwenye Kampuni tofauti na hawa Wengine.

Mfano Mwingine ni Daktari...

Karibia Madaktari wote huwa wanasoma Miaka 5 kama Basic halafu wengine Ndio wanaenda kubobea kwenye Kitu kimoja Kama ni...

Macho, Figo, Meno n.k

Kwanini Asome Kila Kitu Mwanzo na Asiende moja kwa moja kwenye kitu anachota?..

Kwa sababu kuwa Generalist kuna Msaadia yeye kuwa bora wakati atakapo enda kuwa Specialist...

Yaani atakuwa anajua Mfumo mzima wa mwili wa Binadamu Ulivyo kwahiyo Inakuwa rahisi ku Connect DOTS akiwa kama Specialist.

Kwahiyo...

Hata kwenye Biashara nayo iko hivo hivo kama Ndio Unaanza, Anza kwa kuwa...

"GENERALIST"

Ili uweze kujifunza Vitu vingi zaidi Mwanzoni huku wakati huo huo...

Ukijitafuta kwa Kuwa...

"SPECIALIST"

Kwenye Biashara Yako.

Mtu yoyote Aliyefanikiwa Lazima awe "T— Shaped" ili aweze kujua Vitu vingi zaidi

Kwa sababu Biashara SIO Kuuza na Kununua Tu, Kwenye Biashara Lazima ujue Mambo ya...

Tax, Accounts, Laws, Finance, Management, Sales, Marketing N.k..

Kwahiyo ILI Ujue vyote Hivyo Inabidi Uanze Kujifunza Sasahivi huku...

Ukiendelea Kujitafuta Taratibu kwenda kuwa Mtaalamu wa Kitu... KIMOJA

Kwahiyo kwa Ufupi Tu ni Kwamba...

Anza kwa Kuwa..."Generalist"

Yaani...

Jifunze na Soma kila kitu unacho kutana nacho Mbele yako.

Halafu Taratibu...

Endelea Kujitafuta Ili Kuwa..."Specialist"

Yaani...

Mtu ambaye Umebobea kwenye Jambo Moja tu ambalo watu wanakutambua kama ni Mtaalamu!

I Hope Umejifunza Kitu japo kwa Uchache.

By the way...

Tarehe 22 Mwezi Huu Nitaenda Kufanya MASTERCLASS na Wanafunzi wangu wa Consultation.

ILA...

Nilikuwa nafikiria Nichukue na watu wengine kama 10 Hivi Ili Tuungane nao.

Kwahiyo...

Kama utakuwa INTERESTED Unaweza Kuanza Kujianda Mapema kwaajili ya Darasa.

PS: Taarifa Zingine Zaidi Nitazitoa Kadri Muda Utakavykuwa Unasogea.

Uwe na JUMATATU Njema.

Gracias

Seif Mselem
 
Back
Top Bottom