Swali fikirishi usaili wa Sensa ya watu na makazi 2022

kaka-blaza

Member
Nov 7, 2019
84
124
Swali: Je upo tayari kushiriki semina ya sensa ya watu na makazi itakayoanza tarehe 29 July hadi tarehe 15 September?
A: Ndio
B: Hapana

ndugu zangu hivi hili swali lilikuwa linataka nini. semina itafikaje mwezi wa 9 ile hali sensa inafanyika tarehe 23/08/2022?..

sasa hapo ilikuwa tunakataa au tunakubali?
 
IMG-20220719-WA0006.jpg

Nchi ngumu sana hii
 
Swali: Je upo tayari kushiriki semina ya sensa ya watu na makazi itakayoanza tarehe 29 July hadi tarehe 15 September?
A: Ndio
B: Hapana

ndugu zangu hivi hili swali lilikuwa linataka nini. semina itafikaje mwezi wa 9 ile hali sensa inafanyika tarehe 23/08/2022?..

sasa hapo ilikuwa tunakataa au tunakubali?

Kuna wale waingiza data baada ya sensa kuisha so zoezi litaendelea kwa wao...so swali lipo in general
 
Swali: Je upo tayari kushiriki semina ya sensa ya watu na makazi itakayoanza tarehe 29 July hadi tarehe 15 September?
A: Ndio...
Hili swali walikosea wao kuchapa badala ya kuandika mwezi wa nane wao wakaandika mwezi wa tisa. Hawakuliona kosa hili na kiuhakika wale waliokataa na kusema hapana ndio wapo sahihi.

Wengi watakuwa wamejibu hapana kwani semina inatakiwa iishe mapema kabla ya tarehe ya sensa yenyewe ambayo ni tarehe 23.08.2022,

Kama waliwapa zero waliojibu HAPANA na wakawasitishia usaili Ina maana hawakuwachagua waliojibu vema na kuwanyima haki yao ya msingi ya kufanya kazi waliyostahili kuifanya. Viongozi wa juu msipoangalia hawa wataharibu kazi, tafuteni watu weledi. Sensa ni kitu muhimu Sana kwa taifa letu.

Ni Jambo la aibu Sana Sana kwa viongozi wetu hawa kukosa umakini wa vitu vya msingi. Kumbe Basi hata maswali ya usaili ilipaswa yatungwe moja kwa moja na NBS na kuhakikiwa kwa umakini mkubwa.

NB: Nimesikitishwa Sana na namna zoezi zima la kuchagua makarani, wasimamizi, na watu wa tehama. Nilijua kazi yote ingeishia NBS. Kosa kubwa mno walilofanya NBS ni kutochagua wenyewe na kuleta watendaji wa kata ndo wachague. Imewapotezea Sana watu walioomba muda wao, fedha zao za nauli na chakula n.k na hatimaye hawajachaguliwa wengi. Watu kwenye kata walifika Hadi 1000 lakini wanaotakiwa hawazidi 100, unawatesa watu wote Hawa 900 bure kabisa wengine siku nzima wengine siku mbili halafu watendaji kumbe wana watu wao. Hii haipendezi hata kidogo.

Mimi najiuliza kwanini NBS hawakumaliza zoezi zima wao wenyewe ili kuondoa ukiritimba huu?

Mbona walimu huwa wanawapangia kazi bila usaili, Anavyoenda kuripoti ndipo anapeleka vyeti wao walishindwa nini kuchagua moja kwa moja makarani, wasimamizi na watu wa tehama ili Hali wanajua kila mkoa, kila wilaya, kila kata na kila mtaa/Kijiji unahitaji watu wangapi. Kwanini wawasumbue maelfu kwa maelfu ya watu kwenda kwenye usaili hewa, kupoteza muda wao na fedha zao bure?

Kwani waliochaguliwa(hao watakaofanya hiyo kazi) wangewaita kwenye semina wakawaomba kuona vyeti vyao wasingepeleka? Kuliko kuita maelfu ambao wanajua kabisa hawatawachukua wote.

Kazi zenyewe hizi za muda tu lakini watu wanasumbuliwa Kana kwamba ni kazi za kudumu na kazi zenyewe wasipate. Huu usumbufu kwakweli kabisa siku nyingine waangalie usie ukatokea tena. Binadamu wote ni sawa si vema kunyanyasana na kusumbuana.

Hili Mimi naliona kabisa kuwa kwa wale waliosumbuka na hatimaye wakakosa na hizo nafasi hata zoezi zima la sensa wanaweza wasishiriki kwa kinyongo. Lakini kama NBS wangemaliza kazi nzima wao wenyewe hata waliokosa wasingekuwa na kinyongo maana hawajasumbuka.

Wasiwasi wangu ni kwamba Kama Mambo yanakuwa hivi tutegemee pia data zilizopikwa, maana kinachoendelea ni usanii tu weledi ni mdogo Sana.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Wapo sahihi kwenye tarehe
 
Mimi waliniuliza Endapo simu ikiharibika utafanyaje, (hawakusema kustuck)
 
Back
Top Bottom