Sumaye amkaanga JK

Sumaye alimpeleka mtoto wake Maricani kusoma baada ya kuona mafisadi wenzake wote wamewapeleka watoto wao nje kusoma kwa hele za kifisadi.
 
BOT dhaifu Africa kwa sababu ya watoto wa Vigogo. Angalia Kenya watu wanaweza kupokea pesa kwenye paypal pia kuna online payments nyingi sana. Watalii wanapenda kulipia safari kwa credit cards.
 
Hata Idd Azzan mb ccm majuzi eti anakemea watoa rushwa ktk chaguzi za ccm,wakati yeye alikopa bank zote kutoa rushwa kwa wana kinondoni.
 
Kwanza huyu Sumaye amebebwa sana hakustahili ile nafasi ya uwaziri mkuu, waliombeba wametulia yeye anajaribu kusimama kwa miguu yake. Ndani ya moyo wake anayajua haya na ndio maana alienda shule Marekani labda angeweza kujipatia sifa lakini wapi imeshindikana.
Nampa mtihani akiuweza nitamfikiria "Akemee watoto wa vigogo waliopo benki kuu kama kweli amejirudi kuwa mzalendo".

Kiongozi hv bank kuu kumejaa watoto wa vigogo? Tena na hisi hata elimu yao ni kuunga unga hatari sana ndugu yangu kama kwek sumaye ana uwezo ajitoe aje kwa wazalendo ndipo tutakapo jua ana nia ya dhati kabisa na anamaanisha anayo yazungumza
 
Not too late bana,kwani mtu akigundua kuwa alikuwa anapaswa kufanya kitu fulani tangu jana lakini anakifanya leo na ni baada ya kugundua kosa hiyo ni too late!!?
Kuchelewa kupo kwenye uhai tu kwani ndio ambao hauwezi kurudishwa

Mh Sumaye hakukiri kama huku nyuma alifanya makosa,yeye amesemea uozo wa chama chake,anajua wapi pa kupeleka malalamiko yake iwe polisi,kwenye chama chake hata Takuru matamshi kwenye makongamano hayamsafishi bali yanaongeza alama za maswali.Ni vizuri kuachana na siasa, abakie kama mshauri tu.
 
Tumechoka na ngonjera za Sumaye...
Kila siku maneno, mbona hachukui hatua zozote?
Kama kweli anakerwa na hiyo hali basi tumuone akichukua hatua, Vinginevyo ni hana jipya
 
anyway, nafurahia Sumaye anavyowapelekesha CCM akiwa humo ndani yao maana inanipa fursa ya kuujua ukweli unaonuka ndani ya CCM, na wakimgusa tu, kifo cha CCM kitakuja haraka kuliko inavyotarajiwa. Kwa vile magamba wanajua hili, sidhani kama watamgusa badala yake watasema ni upepo tu utapita.

Tanzania ya Neema chini ya CCM haiwezekani..!
 
Kama Sumaye analalama kuwa watu wanaaingiza wake washikaji na watoto wao kwenye siasa atueleze huyo Nagu amefikisha nani hapo alipo na kwa sababu gani, hasitufanye mazoba hizo ni hasira za kushindwa na woman friend wake.
Namshauri kama alivyowahi kusema kuwa kama unataka biashara yako ikunyookee tundika bendera ya CCM, uwanja bado ni uleule wachezaji ni walewale peperusha bendera mwaya. stop crying a wolf
 
JUMAMOSI, OCTOBA 13, 2012 08:58 BENJAMIN MASESE NA ZITHA KANNONYELE, DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu mstaafu, Fedrick Sumaye ameshambulia Serikali ya awamu ya nne, akidai imekiuka misingi ya uongozi iliyoasisiwa na baba wa taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Sumaye alisema Serikali imeshindwa kusimamia usawa, maendeleo ya watu, uzalendo, maadili, mfumo wa kujitegemea, na demokrasia shirikishi vilivyoachwa na Mwalimu Nyerere.

Sumaye aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mdahalo maalumu uliondaliwa na Chuo cha Kumbumbuku ya Mwalimu Nyerere na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.

Sumaye alikuwa mgeni rasmi na mchokaza mada katika mdahalo huo kwamba nini kifanyike katika kumuenzi Mwalimu Nyerere, ikiwa ni sehemu ya kumbu kumbu ya miaka 13 baada ya kifo chake.

Sumaye alisema kuwa kauli za Mwalimu Nyerere kuhusu rushwa zimepuuzwa na kwamba rushwa sasa ndiyo inayotumika kuwapeleka watu Ikulu.

RUSHWA

Akizungumzia rushwa Sumaye alisema rushwa imekuwa janga kubwa Tanzania na Afrika nzima huku jambo ambalo alisema ni hatari katika suala la amani na usalama wa nchi.

"Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mtu yeyote anayeonekana anapenda kwenda Ikulu na hata yuko tayari kununua kura ili kufika Ikulu ni wa kumkwepa kama ukoma.

"Leo hali ikoje? kauli zote za mwalimu zimepuuzwa na rushwa ndiyo inayotumika kuwapeleka watu Ikulu tena vitendo hivi vinafanywa mchana kweupe bila haya.

"Leo Ikulu imefikia hatua ya watu kuitumia katika biashara yao, sasa swali la kujiuliza na kujitafakari wote hapa ikitokea miujiza Mwalimu Nyerere akafufuka ni wangapi watajitokeza kwenda kumlaki?

"Tuseme ukweli kwamba asilimia kubwa ya viongozi wa sasa watakimbilia katika mapango ya wakoloni na wachache ambao hawamfahamu na hawakulelewa na Mwalimu ndiyo watakaomlaki," alisema.

Sumaye alisema kuwa Mwalimu Nyerere alikaa katika uongozi kwa miaka mingi bila kuihusisha familia yake na Ikulu na kwamba hata watoto wake walisoma na kula chakula ambacho Watanzania wengine walikuwa wanakula.

"Isitoshe hakutaka kujenga wala kujilimbikizia mali pia alikuwa mtu wa maono ya mbali na kuchukua hatua na alipinga ubepari.

"Lo tunashuhudia Serikali imeshindwa kukemea mabaya na kuendeleza mazuri ya mwalimu, watoto wa viongozi wanapewa madaraka na elimu yao ni tofauti.

"Tunapokuwa tunafanya maadhimisho ya kifo cha Mwalimu Nyerere kila mmoja ajitafakari anachofanya, anachotamka mbele ya jamii na kukifananisha na kile ambacho mwalimu alikipinga kama vina uhusiano," alisema.

Sumaye ambaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka 10 alisema kiongozi yeyote aliyefanya kazi na Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake leo hii anashikwa na kigugumizi kulingana na mambo yalivyo.

ELIMU

Akizungumzia elimu, Sumaye alisema asilimia kubwa ya vijana wamefikia elimu ya sekondari ambayo haina manufaa kwao kutokana na kutoandaliwa katika misingi ya kujiajiri.

"Hali katika shule nyingi za binafsi ni tofauti na ufaulu wa wanafunzi wa shule za Serikali jambo ambalo ni hatari, sasa tujiulize kwanini unatokea utofauti, jibu ni kwmaba kumeibuka matabaka ya wenye fedha na masikini.

‘Hali hii isipozuiliwa mapema italeta matabaka ingawa hakuna wa kuizuia kutokana na kupuuza misingi tuliyoachiwa, sisi sote ni mashahidi ndani ya jamii yetu wamekuwa hawajali wengine kutokana na umaskini kuongezeka.

"Leo Tanzania iliyoachwa na Mwalimu Nyerere imefikia hatua ya kufuta elimu ya kujitegemea ambapo vijana wengi wamemaliza shule hawana ajira kutokana na Serikali kushindwa kuanzisha viwanda vya kusindika

Katika hatua nyingine Sumaye alisema moja ya ugonjwa uliopo sasa ni wa viongozi kukubali kuwa na udhaifu na kutokiri kukosea kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere.

"Nyerere alikubali kukosolewa na akalazimika kuanzisha kitabu cha tujisahihishe, kitabu kilitumika kurekebisha pale walipokuwa wakikosea.

"Lakini leo hakitumiki na kila kiongozi sasa anatumia siasa kuongeza, nisema wazi tusipiorudi katika misingi tuliyoachiwa hatutafanikiwa.

"Watu wanasema mdomoni kwamba wanamuenzi mwalimu na kulinda misingi bora ya utawala lakini moyoni wanachofikiwa ni kitu kingine.

"Viongozi wa Serikali wa leo wamefikia hatua ya kutumia ushirikina kutafuta madaraka na pia wananchi wanapouliza maswali magumu wao hutoa majibu rahisi, hili ni tatizo katika uongozi.

"Wameshindwa kusimamia ushupavu, usomi, busara, kupenda maendeleo, haki, msimamo na mambo mengine kama hayo ambapo hivi sasa wamejigeuza na kujiita waheshimiwa badala ya ndugu,"alisema.

Akizungumzia uchumi wa nchi alisema anaipongeza Serikali kusimamia ukuaji wa uchumi lakini akaongeza kwamba uchumi huo hauonekani dhahiri katika mabadiliko chanya.

"Katika maisha ya mwalimu alisimamia upande wa wanyonge na aliwatetea maisha yake yote lakini kutokana na mtawanyiko wa mali hivi sasa katika nchi yetu hautupi tena tumaini la amani na utulivu la muda, hivyo kwa faida ya wote ni vema marekebisho yatakafanya bila kuchelewa,"alisema

Sumaye alisema Tanzania itarudi katika hali yake ya kimaadili na utu ikiwa viongozi watarejea misingi ya uongozi iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.

"Watanzania tuwe kama familia moja bila kujali cheo na nafasi ya mtu kula chakula kinachofanana, elimu yenye mazingira na ubora unaolingana, kupewa adhabu inayofanana bila upendeleo na kutoa ajira kwa usawa," alisema.

Naye Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. John Magoti alisema mdahalo alisema lengo la kufanya mdahalo huo ni kupima na kutathmini misingi na maadili ya Mwalimu Nyerere yanavyoenziwa.

 
Sikujua VIONGOZI wengi wa CCM walio MADARAKANI wanayajua fika Maelezo na Maneno ya Mwl. Nyerere... Hadi hilo suala la kutaka kwenda IKULU kwa kuhonga ni wa kuogopa kama UKOMA!!! Lakini sasa MBONA wanaendelea kuhonga ? MKAPA aliyajua hayo bado alifanya visivyotakiwa; Kikwete yeye ndio kabisaa anatupeleka kubaya zaidi ya UKOMA
 
images


Sumaye amkaanga JKna Efracia Massawe
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye, amewalipua viongozi wa sasa wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete kwa hatua yao ya kuruhusu baadhi ya wanafamilia wao kuwania vyeo vya juu vya uongozi.


Akiwasilisha mada kwenye mdahalo wa maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, jana jijini Dar es Salaam, Sumaye alisema hatua ya viongozi wengi kuandaa watoto na wake zao kwa ajili ya kuwa viongozi wa nchi, ni kinyume na katiba ya nchi, na dalili ya ubinafsi.


Katika chaguzi za sasa ndani ya CCM, Rais Kikwete ni mmoja wa viongozi waandamizi ambao familia zao zimegombea na kushinda nafasi za uongozi ndani ya jumuiya za chama hicho. Baafhi ya watu kutoka familia ya Rais Kikwete waliojitosa katika chaguzi hizo ni pamoja na mkewe, na watoto wake wawili.

Kauli hiyo nzito ya Sumaye ni ya pili tangu alipoanguka katika kinyang’anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC Taifa, akishindwa na Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu.
Mwishoni mwa wiki, Sumaye alikaririwa akisema kuwa, kukithiri kwa rushwa ndani ya chama hicho, ndiyo sababu kubwa iliyomwangusha na kueleza hofu yake ya nchi kupata viongozi wabovu.


Aliongeza kuwa ubinafsi umekuwa chanzo kikubwa cha kukithiri kwa rushwa katika sekta mbalimbali kwa kuwa viongozi wengi wa serikali, hawako tayari kupoteza madaraka yao, hivyo hutumia rasilimali za nchi na uwezo wao wa kifedha kuwahonga wapiga kura ili waendelee kukaa madarakani, hata kama wananchi hawawataki. “Rushwa imekithiri sehemu muhimu na mtu yeyote anayetaka kwenda Ikulu kupitia rushwa hafai. Mosi hizo fedha za kuwahonga wananchi alipata wapi? Kama amekopa anategemea Ikulu kuna hela ambazo hataweza kurudisha deni hilo?


“Chaguzi zote zimetawaliwa na rushwa moja kwa moja jambo ambalo hayati Mwalimu Nyerere alilikemea hadi mwisho wa uhai wake, na kama hatutaliangalia tatizo hilo kwa makini, kuna athari kubwa kwa taifa,” alisema. Sumaye alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, kama Mwalimu Nyerere angefufuka leo, kusingekuwa na kiongozi wa kumlaki, badala yake watu wengine wangekuwa wa kwanza kukimbilia porini.


Mbali ya ubinafsi huo, alisema uchumi wa nchi umeshikiliwa na kundi la wachache, hivyo kuzuka kwa hali ya kutojali kundi la watu masikini ambalo ni tatizo kwa taifa, kwa sababu viongozi hao wamewekeza kwa kuwajali wenye nacho ili wanufaike kama wao.


Naye Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. John Magotti, alitumia fursa hiyo kuzungumzia suala la kiwango cha elimu itolewayo nchini hususani katika shule za kata kuwa ni chachu ya kukwamisha ufaulu sanjari na ajira kwa wahitimu. “Kuna haja ya serikali kutafuta ufumbuzi katika sekta ya elimu kabla haujaleta madhara makubwa, kwa sababu elimu bora inaendana na nafasi bora ya ajira, hivyo mwito wangu elimu inayotolewa katika shule za kata isitofautiane sana na ile ya shule za watu binafsi,” alisema Magotti.


Tanzania Daima
 
Ni kwa msaada wa mungu sikuwahi kufikiria hata ingetokea aina hii ya uongozi wa koo na kifamilia yani wanataka kurithishana jamani kwa sasa vijana wasomi wenye uwezo wa uongozi jiungeni vyama vingine mupambane na chama hichi cha ukoo na familia fulani tu wakutane nc kwao mwanangu nishamwambia mie apeleke wapi harakati zake

Siku hazigandi wajue.

Nayanda.
 
inamana leo ndio kajua au ni wivu tu.angeshinda? angesema?

Kikwete ameingia mke, watoto wake na ndugu zake kwenye nafasi nyeti za uongozi wa CCM taifa hadi matawini kipindi hiki cha uchaguzi, namtetea Sumaye kwa hili. Mbona kuna wengi bado hawajajua mchezo wa Kikwete aliucheza safari hii?
 
Kapotea njia huyo. Juzi si alikuwa na press conference mbona hakuyasema hayo na mengine mengi tunayoyajua?

Kwa hakika Sumaye ni mwoga na mnafiki hivyo hafai kabisa kuwa kiongozi wa Tanzania tuitakayo.
 
Tatizo la Sumaye haelezi marekebisho yaweje, na anayoyasema wengi tunayachukulia kama maneno ya mkosaji, si juzi tu alikosa ujumbe wa NEC.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom