SUMA JKT tujifunze toka SAMSUNG kuikomboa Tanzania kiuchumi

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Toka Twitter anaandika @jamzsjason

Tunaposherehekea miaka 60 ya JKT tunajivunia umahili na uadilifu unaoendelea kuwepo katika Jeshi letu la Kujenga Taifa pamoja na ubunifu wao katika SUMA JKT.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari jinsi gani Tanzania inaweza kupata taasisi kama SAMSUNG kampuni moja iliyoweza kulikomboa lililokuwa Taifa masikini la Korea Kusini.

SAMSUNG na SUMA JKT wanafanana sana. Wote ni makampuni binafsi yenye mkono wa Taasisi za Kiserikali.
SUMA JKT ikiwa ni Jeshi la kujenga Taifa JKT Tanzania na SAMSUNG ikimilikiwa kwa 7.92% na Mfuko wa Huduma za Pensheni wa Korea.
Makampuni yaliyo chini ya JKT ni
1.Sumajkt construction co.ltd
2.Sumajkt bottling co.ltd
3.Sumajkt port & service co.ltd
4.Sumajkt guard co.ltd
5.Sumajkt auction mart co.ltd
6.Sumajkt leather products
7.Sumajkt agri-machinery
8.Sumajkt mlale food processing
9.Sumajkt electric co.ltd
10.Sumajkt cartering co.ltd
11.Sumajkt chang'ombe furniture co.ltd
12.Sumajkt garments co.ltd
13.Sumajkt logistics co.ltd
14.Sumajkt insurance brokers co.ltd

Makampuni yaliyo chini ya SAMSUNG
1.samsung venture investment
2.samsung c&t corporation
3.samsung engineering
4.samsung heavy industries
5.samsung life insurance
6.samsung fire and marine industries
7.samsung SDS
8.samsung SDI
9.samsung biologics
10.samsung electro-mechanical
11.samsung bioepis
12.samsung card
13.harman
14.samsung medical center
15.samsung group

SAMSUNG ni alama ya Ushindi kiuchumi kwa watu wa Korea Kusini. Wanaipenda na kuithamini. SUMA JKT tunaipenda na kuikubali watanzania lakini ni wakati sasa iende hatua moja mbele.
1. SUMA JKT ibaki kusimamiwa na JKT

2. (Branding) Tuondoe neno JKT ibaki SUMA

3. Iweke % fulani za umiliki kwa umma hata 10% wananchi wananunue Shares DSE jina liwe SUMA PLC

4. SUMA LOGO iwe kibiashara na sio Kijeshi.

5. Iwe Sera / Vision ya kitaifa kuipeleka SUMA mbele kitechnolojia, miundombinu na Fursa zaidi za Kazi kuwezesha kukua mtaji wake. Leo tunasema DP World ina mtaji ni kwa sababu serikali yao imeamua kuipa support kama alama ya Taifa. National Brand.
Tuweke taasisi kama SIDO, VETA na Shule za Ufundi kama sehemu ya SUMA PLC.

Simu ya Kwanza toka Tanzania, Gari la Kisasa toka Tanzania, Mapinduzi ya Kiubunifu na Exports zinatakiwa zitoke SUMA PLC. Tutengeneze Toothpick zetu wenyewe (inawezekana).
Hata lile jengo refu zaidi duniani limejengwa na SAMSUNG ENGINEERING. Sisi tuwaze SUMA Engineering (Inawezekana)
MELI KUBWA Duniani zinatengenezwa na SAMSUNG heavy industries. Sisi Tuwaze SUMA Heavy Industries (Inawezekana)
Vifaru vya Kijeshi na vifaa vya Kijeshi vinatengenezwa na Samsung AeroSpace Industries. Sisi tuwaze SUMA AEROSPACE Industry (Inawezekana)

Narudia tena inawezekana View attachment 2687008View attachment 2687007View attachment 2687012View attachment 2687009View attachment 2687010View attachment 2687011
20230713_203201.jpg
 
Ili kitu kama hiki kiwezekane, lazima......
1. Kuwe na sera clear, tangible vision na utashi wa viongozi wake...
2. Udhubutu, branding & marketing ya kutosha na innovation sana.
3. 100% full governmental and local customer supports.
4. Wapunguze import zisizo na msingi. (Kama vile, electronic devices, agricultural machinery, domestic products like sifuria, kikombe, toothpick, etc. Magari, dawa za binadamu, dawa za mifugo).
5. Wapate kiongozi (CEO) mwenye kujitambua.

Na vingine vingi ambavyo makampuni smart kama SAMSUNG wanafanya.

Pia, kiongozi asiwe na ugonjwa maarufu Tanzania wa UCHAWA......SUMA itafanya vizuri sana kuanzia local market mpaka International......
 
Tatizo la watanzania wanaongea weeeeh, mpaka basi.

Nilienda sabaaaba na kuwatembelea SUMA JKT.

Jama wanafanya mambo makubwa, wamejenga ikulu ya Dodoma, wamejenga majengo mapya ya Mzumbe kuanzia idea ya majengo, ramani, ujenzi halisi, mpaka umeme, kila kitu.

Jamaa wapo vizuri, na wanaeza ku-handle hata bajeti ya mabilioni ya pesa...nadhani hata matrilioni ya pesa.

Kama hawatafanyiwa figisu na kuendelea kufanya kazi vizuri, ni rahisi kuaminiwa na watanzania, ndani na nje ya nchi, hata nchi za jirani wanaweza kutoa huduma kwa weledi mkubwa.

Nimejivunia sanaa kuwa mranzania na naamini siku nikiwa tajiri, nitawaajiri wanijengee maghorofa yangu, au naamini nitafurahia kufanya nao kazi.

Iwe ni ujenzi, au shughuli zingine zozote.

Naipenda Tanzania, nimefurshishwa na Kazi nzuri za SUMA JKT.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Toka Twitter anaandika @jamzsjason

Tunaposherehekea miaka 60 ya JKT tunajivunia umahili na uadilifu unaoendelea kuwepo katika Jeshi letu la Kujenga Taifa pamoja na ubunifu wao katika SUMA JKT.

2. (Branding) Tuondoe neno JKT ibaki SUMA

3. Iweke % fulani za umiliki kwa umma hata 10% wananchi wananunue Shares DSE jina liwe SUMA PLC
TACH=full]2687010[/ATTACH]View attachment 2687011View attachment 2687013
Mkuu ujue Samsung inalindwa na serikali yao Korea.Hapa sisi tunawapa maeneo kama nchi ya Rwanda, loliondo kwa waarabu wachukue Simba, tembo, giraffe, wanyama wote sisi tupo kimya.

Pia tunawapa bandari zote mito, maziwa, bahari Tanganyika.

Anauza nchi Rais na CCM.

Mikataba ya kitumwa tunaishangilia.
 
Tatizo tumepenyeza siasa kila sehemu. Siasa zinafubaza ubunifu na vipaji, watu vyeo wanapandishwa kwa uchawa, kujipendekeza na kujuana
 
Mkuu ujue Samsung inalindwa na serikali yao Korea.Hapa sisi tunawapa maeneo kama nchi ya Rwanda, loliondo kwa waarabu wachukue Simba, tembo, giraffe, wanyama wote sisi tupo kimya.

Pia tunawapa bandari zote mito, maziwa, bahari Tanganyika.

Anauza nchi Rais na CCM.

Mikataba ya kitumwa tunaishangilia.
Kwa kweli viongozi wetu pamoja na kuwaombea kila siku makanisani lakini akili zao haziwasaidii chochote sijui ni rushwa zinawafanya wawe wapumbavu.

Tanzania yetu mgeni anathaminiwa kuliko mwenyeji, misamaha ya kodi, archi za bure na mikataba ya kipumbavu ndio wanapewa wageni. Ugumu mwingi sana kwa watanzania sijui shida zao huwa ni nini. Mfano TCRA wale ni wazee wa kunyonga yaani ni kuminya wazawa kila iitwapo leo leseni zao ni maelfu ya dola.

Mambo ya nchi wakati fulani ukitakari unakereka sana
 
Mkuu nipe solution. Naona kama tumeuza, tunauza nchi na rasilimali zake zote.
 
Back
Top Bottom