Sukari ni madawa ya kulevya yaliyohalalishwa, jihadhari nayo kama unataka kuwa na afya bora

Uko sahihi, lakini uko kwenye extreme end. Sukali ni muhimu sana kwa mwili wa binaadamu tatizo ni sukali zinazozalishwa viwandani
 
Hizi zote ni harakati zako zakutafuta pesa hakuna kingine.Mambo ya kula kila mtu ale anachoweza kwasababu dunia ya sasa watu wanaongea mambo mengi sana ambayo hayasaidii chochote.
 
Matunda NO
Nyama NO
Interesting...
Sukari NO
Chumvi NO
Mafuta NO
Wanga NO
Pombe NO

Sasa tule nini wadau?
Lakini ya kufaidi nini usipofurahia vitamu duniani? Tule ila mwili upate mazoezi....
Imagine kungekua na statements kama marehemu alipofariki alikuwa na kila kitu kizima ini moyo pafu hvyo mbinguni atapokelewa na shangwe.....
Hebu tufurahie maisha we will all die...
 
Mago
Ukichagua sana vyakula unakuwa unaishi kwa hofu, na hii ndo mbaya zaidi....maana kuna magonjwa kibao yanayosababishwa na kuwa na hofu.
Ugonjwa wa moyo wa siku hizi unazishwa na matatizo ya kimaisha mfano mawazo ya kukosa fedha/mahitaji muhimu,kushinikizwa kufanya mambo kazini n.k
Mtu unaishi kwa hofu..hofu ya kutekwa hofu ya kufa maskini,hofu ya kutomudu gharama za afya,chakula,elimu..lazima tu moyo wako hautakaa sawa siku zijazo..
 
Dr.Ndodi aliwashika watu na ugali wa dona mwaka huu TFDA nao wametoa tangazo la madhara ya ugali wa dona kwa hiyo mimi wote siwasikikizi kabisaa maana mmevamia hadi kwenye matunda na miwa?
 
Mama wa Kisabato naona ndio anatrend hizi siku ngapi na masomo yake ya afya huko Dodoma. Ila hata Dkt Ndodi alitulisha sana matango poli na kuwakandia wenye vitambi ila nasikia nae siku hizi ni tukunyema kitambi hicho. Wewe kula bhana hata mavegan wanaumwa kansa ila hawajui wameipataje ingawa wameacha kula vyakula nyama na vyakula wanavohisi vina chemical mbaya, wanasema dunia ni ya ajabu utachagua kula hiki sababu una nafasi ya kuchagua kuna watu wanaishi sehemu ambazo hawana option ya vyakula so ishi unavoweza aiseee
nimemsikia kwa mbali jana mitaa ya nkuhungu halafu kama anatumia lafudhi ya watu fulani hivi ili kuwaaminisha watu wengi.
 
sijawahi ona mtu amekunywa chai aka 'randuka' hizi tafiti uchwara hizi zitakuja kutu tumbiza mtoni hizi
 
Dr.Ndodi aliwashika watu na ugali wa dona mwaka huu TFDA nao wametoa tangazo la madhara ya ugali wa dona kwa hiyo mimi wote siwasikikizi kabisaa maana mmevamia hadi kwenye matunda na miwa?
Mimi navyofahamu kuna muda mwili unakupa taarifa ya kuhitaji aina fulani ya chakula tatizo ni pale unapokula kupita kiasi na kuacha mazoezi au kufanya kazi itayopelekea utumikaji wa nishati na virutubisho ulivyopata.
Mfano mwili hutoa taarifa ya kuhitaji maji ila mtu atashindwa kunywa maji kwa sababu mbali mbali pengine hayapo,yapo machafu au mpaka anunue,kuna muda unahitaji ule matunda tena kwa taarifa ya mwili inakupa pengine wazo ule Papai na sio Embe kabla ata ujaona tunda lenyewe..ule nyama ya kuku na sio mbuzi..ila sasa kumeibuka hali ya kuwa "induced" mfano unaona Tangazo la "Nyama Choma Festival" au matangazo ya Pizza na Juice kubwa za kampuni fulani kwa bei nafuu,akili yako itaunda hamu bandia na inapelekea ulaji uliopitiliza kama hautakuwa makini.
 
hawa huwaga ni wapiga ramli tu kama wapiga ramli wengine

Kuna mmoja anashauri watu wasinywe maji mengi ni vibaya na yanasababisha damu kuwa nyepesi

Hakuna kitu kisicho na madhara iwapo kitatumiwa kwa viwango vikubwa kuliko kawaida.
hahahaa nilimskia yule, eti maji yanaosha madini mwilini hivyo haitakiwi kunywa mengi
 
KWA NINI SUKARI NI MADAWA YA KULEVYA YALIYOHALALISHWA.
Hivyo unapotumia sukari, ubongo unazalisha dopamine, ambayo inakufanya ujisikie vizuri na upate utamu wa sukari. Lakini baada ya hapo unasukumwa kutumia tena sukari ili upate utamu zaidi na kujisikia vizuri zaidi.
Kwa hiyo ukiwa na hamu ya kurudia kutumia kitu ulichokitumia, hicho kitu kinaingia kwenye kundi la madawa ya kulevya?
 
Ndani ya majani ngombe anapata kila kirutubisho anachohitaji, kwa sababu mwili wake unazalisha kemikali zinazoweza kuvunja majani hayo.
Lakini sisi binadamu hatuna kemikali hizo, ndiyo maana ukila mboga za majani kwa wingi, choo yako inakuwa kijani, sehemu kubwa ya mboga zinatoka kama zilivyo, mwili hauzivunji.
Lakini sasa ukachagua kula nyamba ya ng'ombe pekee, ng'ombe ambaye amekula nyasi pekee, ukala pamoja na mafuta yake, unapata virutubisho vyote ambavyo ng'ombe amevipata kwenye majani. Na hapo utakuwa umekula kwa afya kuliko kula sukari kwa wingi.
wewe unashauri wale nyama ya ng'ombe kwa wingi, wengine wametuambia nyama nyekundu hazifai kabisa tule samaki na kuku, hamuoni kuwa mnapiga ramli mchana kweupee!
 
Elimu zengine ni za kupuuza tu

Eti vyakula vimegawika kwenye mfungu manne...kweli.!?

Ng'ombe anakula nyasi tu na bado ana nguvu kuliko wewe tena mnene na magonjwa hapati hovyohovyo kama wewe na Mimi

Kweli wazungu wameanzia mbali kutuloga
Makundi ya vyakula ni muhimu...ila namna ya ulaji sijali.

Kipindi cha hali ngumu watoto wanashida na maembe tuu mwezi mzima ...unaona afya zinavyozidi zorota
 
Nikiona nyuzi kama hizi huwa naishia kusoma tu nikimaliza natabasamu kidogo halafu maamuzi yanabaki kwangu mwenyewe.
 
kila nikimfikiria de ndodi.....haya mambo naona kama ubatili mtupu.

alokuwa anakataza yeye ndo kadumbukia....

kipindi anaanza pale star tv....alikuwA na mwili simply kama mtoa mada.
lkn baadae kidogo kitambi kikamshinda.

sijui anawqambiaje wale alowaaminisha kitambi ni ugonjwa
 
Kula sukari kutakuua haraka kuliko kutokula sukari.
Ulaji wetu wa sukari umekuwa ni mazoea tu, lakini ukiuzoesha mwili vyakula vingine maisha yanaendelea kama kawaida.
Mwili wako una uwezo mkubwa wa kupata nguvu kutoka kwenye mafuta na kwa uhakika kuliko kutoka kwenye sukari.
Vipi kuhusu mayai mkuu?
 
hahahaa nilimskia yule, eti maji yanaosha madini mwilini hivyo haitakiwi kunywa mengi
Mkuu hii ni kweli
Hujui mkojo na jasho hutoka na chumvi za mwili?
Kumbuka pia maji kupita kiasi mwilini hu dilute chumvi sana na kuleta shida ktk osmoregulation
 
Back
Top Bottom