Sugu ameachwa mbali na Dkt. Tulia katika kila kitu, ni vema akubali ushauri wa kugombea Ubunge Makete au Ubungo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,026
Hakuna namna Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini anaweza kumshinda Mbunge wa sasa ambaye pia ni Spika wa Bunge la JMT na Rais wa Mabunge yote Duniani.

Kama Taifa hatuwezi kukubali kupoteza nafasi ya kuwa na Rais wa Mabunge ya Dunia.

Hivyo nashauri Msanii wa kizazi kipya akubali ushauri aliopewa kutoka juu kama tetesi zinavyosema kwamba akajaribu Makete Njombe au Ubungo DSM na kama kura hazitatosha atatunukiwa uDC kwa Upendo wa mama.

Sugu Moto Chini Usiwe mbishi Wenzako Joshua, Lijualikali na Mtatiro maisha wameyarahisisha jaribu kuiga mfano.
 
Acha uchawa, sasa kama hawezi kumshinda shida iko wapi ya kumkataza kugombea na Tulia, maanake wananchi wataamua, tulia kama anauzika atashinda mapema, kama sugu ndiye chaguo la wananchi, shida ipo wapi hapo? Kwa hiyo wewe mtoa maada unataka tulia apite bila kupingwa kisa ni rais wa mabunge duniani? Yeye kuwa rais wa mabunge duniani mimi kama mwananchi wa iyunga inanisaidia nini?

Tuache democracy ifanye kazi yake!! Msituletee yale ya magufuli eti mtu anapita bila kupingwa yaani mambo ya hovyo kabisa, tunataka ushindani kwenye sanduku la kura, wewe kama tulia wako ana ushawishi na anamshinda sugu kwa kila kitu mwache basi sugu wakashindane kwenye sanduku la kura tujue mbabe ni nani!! Usituletee bla bla hapa!! Hao waliopita bila kupingwa wametusaidia nini mpaka sasa? Badala yake limekuwa bunge la serikali badala ya kuwa bunge la wananchi!

Acha uchawa!
 
Hakuna namna Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini anaweza kumshinda Mbunge wa sasa ambaye pia ni Spika wa Bunge la JMT na Rais wa Mabunge yote Duniani.

Kama Taifa hatuwezi kukubali kupoteza nafasi ya kuwa na Rais wa Mabunge ya Dunia.

Hivyo nashauri Msanii wa kizazi kipya akubali ushauri aliopewa kutoka juu kama tetesi zinavyosema kwamba akajaribu Makete Njombe au Ubungo DSM na kama kura hazitatosha atatunukiwa uDC kwa Upendo wa mama.

Sugu Moto Chini Usiwe mbishi Wenzako Joshua, Lijualikali na Mtatiro maisha wameyarahisisha jaribu kuiga mfano.
Tulia aende Busokelo au Rungwe,pale Mbeya mjini ni pagumu sana kwake labda wapindue meza kama 2020!
 
Back
Top Bottom