Sudan Kusini kujiunga na EAC Julai

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
SUDAN Kusini, nchi iliyozaliwa hivi karibuni baada ya kujitenga kutoka iliyokuwa Sudan, inatarajiwa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Julai mwaka huu.

Tujadili, Faida na Hasara zake.

Natanguliza shukrani.
 
Waache waje tusaidie kujenga Taifa lao kwani ni ndugu zetu, Sudan ya Kaskazini hawana msaada wowote kwao. Wanahitaji uzoefu wetu
 
Itakuwa December 2011. Wamewaomba wenzao wa Kaskazini kuongeza muda ili kuweka sawa mambo flani flani kama mgawanyo wa rasilimali, jinsi ya kudeal na uraia kwa watu waliopo kusini/kaskazini etc

Pia kuna issue ya stability huko Kusini maana kuna makundi flani bado yanapigana huko.
 
Waache waje tusaidie kujenga Taifa lao kwani ni ndugu zetu, Sudan ya Kaskazini hawana msaada wowote kwao. Wanahitaji uzoefu wetu
Mkuu.
Wa Kaskazini wakitaka kujiunga EAC tutawakataa? wao si ndugu zetu?
Nyerere, Nkurumah,Gaddaffi anataka Afrika yote iungane.
 
Mkuu.
Wa Kaskazini wakitaka kujiunga EAC tutawakataa? wao si ndugu zetu?
Nyerere, Nkurumah,Gaddaffi anataka Afrika yote iungane.

Wa Kusini wamelazimika kukimbia, hata wale wa Darfur pia wakipata upenyo watakimbia fasta. Hao ndugu zako wa Kaskazini ni moto wa kuotea mbali, hawajui kuheshimu wala kuthamini maisha ya wengine. Usifikirie kabisa kuwaleta EAC.
 
They are most welcome. Ni wenzetu, tuliishi nao enzi za mwanamapinduzi Nyerere na kina Garang walisomea hapa, na wengi miongoni mwa viongozi wa kule wa sasa waliishi Dar, Kampala au Nairobi. Umoja ni nguvu Utengano ni udhaifu. Natamani na DRC pia wangejiunga nasi ili ku-enhance peace and stability huko.
God Bless Africa.
 
Ni vizuri, ili watuuzie na mafuta. Si unajua 80% ya mafuta sudan yanatoka kusini japo kwa sasa yanauzwa China
 
Tunawakaribisha hata wale wa kaskazini wakitaka hatutawatenga ilimradi wafuate conditions zinazotakiwa kabla ya kujiunga. Nina hakika wa kaskazini wakiungana na EAC WATABADILIKA na kutakuwa na uwezekano mkubwa wa amani kurejea. Hatuwezi kuwatenga kwa sababu ya vurugu zao. Maandiko yanasema "aliye mzima haitaji tabibu bali aliye mgonjwa" hivyo sudan kaskazini nao wanahitaji tabibu.
 
Mkuu.
Wa Kaskazini wakitaka kujiunga EAC tutawakataa? wao si ndugu zetu?
Nyerere, Nkurumah,Gaddaffi anataka Afrika yote iungane.

Gadafi hatufai,si vema kumnukuu kwa jambo jema, kawashambulia na kuwaua raia wa libya kwa kutumia ndege za kivita, "kutawala si lazima" gadafi hafai, hafai, nasema hafai.
 
wakenya ni wajanja sana baada ya sudan kusini kujitenga wamekuwa wana iconvise ijiunge e.a.c ili wanufaike kiuchumi wao kwani bidhaa zao zote watauza kule tena zitakuwa zinapita bila sababu nchi haina hata kiwanda cha penseli pia wakenya wengi wataenda kulishika soko la ajira maana pia kule wasomi ni wachache kwa kuanzia wanajenga bandari mpya lamu special kwajiri ya sudan kusini pia barabara yao wameanza kuipanua na kuifanyia marekebisho from nairobi nakuru eldoret mpaka mpaka sudan.tujiulize wote nchi nyingine tutafaidika vipi na sudan kusin?
 
Si umesema hawana hata pencil?? Sasa tuwauzie na sisi tufaidike. Vilevile kilimo kwanza cha JK kitatuwezesha kuwauzia chakula ambacho kwa sasa bei yake ipo juu na inazidi kupanda!! Tuache kulalamika, kama EAC hatuwezi basi tutoke. Mbona hata huku SACD sisi kufaidika kwetu ni kuhuduria mikutano na kupeleka akina Sofia Simba kwenye bunge!!
 
Wa Kusini wamelazimika kukimbia, hata wale wa Darfur pia wakipata upenyo watakimbia fasta. Hao ndugu zako wa Kaskazini ni moto wa kuotea mbali, hawajui kuheshimu wala kuthamini maisha ya wengine. Usifikirie kabisa kuwaleta EAC.
Dhambi ya ubaguzi...vipi hawa wa kaskazini wanakuwa ndugu zangu mimi na si ndugu zako pia?
Mimi nimezoea Waafrika wote ni ndugu.
Binadamu wote ni ndugu.
 
Sio kila kitu kinaitaji source, mambo mingine ni mawazo binafsi ya watu! Mkuu thread yako nimeipenda, nadhan hawa wakaribishwe tu, bt niwakorofi sana watu, itabidi tujipange jinsi ya kudeal nao. Mh. John Garang ktk maisha yake aliishi km mtanzania na hata harakati zake mipango mingi, strategies yake nyingi zilipangwa Bongo, zaidi alisoma University of Dar es salaam, ndie Baba wa taifa hili jipya la sudan kusin, tuwapokee hawa ndugu pia tuwe makini nao mpaka watakapo settle!
 
Sio kila kitu abt EAC tusingizie ujanja wa wakenya tutakuwa tunawapa sifa bure zisizo na msingi, mambo mingine ni mawazo binafsi ya watu na mtazamo wa nchi juu ya jinsi gani itashirik ktk siasa za nje, mambo ya kuzingatia hapa ni kwamba HILI TAIFA NDIO KWANZA LIMEPATIKANA then wamekua ktk mapigano na Sudan kaskazin kwa takriban miaka 50 na zaidi so kuanza kwa kujitenda, kukata mawasiliano na kaskazini ni njia nzuri ya kujijenga pia kujitegemea! Mkuu kifup thread yako nimeipenda, nadhan hawa wakaribishwe tu wajiunge tena pasipo vikwazo vyovyote ili mradi wanavigezo vya utaifa, kwangu Sudan kusini ni kama mtoto anaejifunza kutembea hivyo anapaswa kushikwa mkono na mataifa yaliyo simama pamoja na Tanzania. bt napenda toa angalizo kwan kiasilia hawa watu niwakorofi sana, itabidi tujipange jinsi ya kudeal nao. Mh. John Garang ktk maisha yake aliishi km mtanzania na hata harakati zake mipango mingi, strategies yake nyingi zilipangwa Bongo, zaidi alisoma University of Dar es salaam, ndie Baba wa taifa hili jipya la sudan kusin, tuwapokee hawa ndugu pia tuwe makini nao mpaka watakapo settle!
 
Sioni tatizo la wakenya, waache wafaidike.
Acheni tubakie na usanii wetu, Cheki Mombasa Road inavyopanuliwa tokea pande za Embakasy mpaka Jomo Kenyatta Int. Airport hiyoooo hadi Kipengela kuelekea Kajiado.
Tumebaki na majungu na kukatisha tamaa viongozi wanaotaka kuleta mabadiliko kimaendeleo.
Upuuuuuuz wetu.
Kichaka cha wezi CCM kimeua nchi.

Na subirini Kenya ndiyo itakuwa inchi iliyo katikati ya EAC watataka hadi makao makuu yawe Kenya.
 
Kila kitu kulalama tu. Ikiwa huna cha kuuza acha walionacho wauze
 
Mwinyi alishasema, Nchi kichwa cha mwendawazimu hii. Tumeua refining plant pale kigamboni, sasa tungekuwa tunapanga madeal ya kupata pafuta toka Sudani na Uganda na kurefine hapahapa na mengine kuuza kusini.
 
Hili jambo si lakuchukulia mzaa na kuona kama la kawaida....kwa upepo huu tunaoenda nao kuna hatari ya kuwa watumwa wa nchi nyingine......
 
Back
Top Bottom