Sudan Kusini imefikia ndoto yake?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
120620162405_south_sudan_uhuru_1_624x351_bbc_nocredit.jpg

120620162405_south_sudan_uhuru_1_624x351_bbc_nocredit.jpg
Raia wa Sudan Kusini wanatarajia kusherekea mwaka mmoja wa uhuru wa nchi hiyo. Ilikuwa mbwembwe na furaha 9/7/2011 siku ambayo taifa mpya kabisa duniani ilipozaliwa.











Sudan Kusini inaadhimisha mwaka mmoja wa uhuru wake mwezi Julai baada ya taifa hilo kujiondoa kutoka Sudan hapo Julai Tisa mwaka wa 2011.

Baada ya vita vya miaka mingi raia wa Kusini walijawa na matumaini, kwamba uhuru wa eneo lao utatoa nafasi ya kumalizika kwa matatizo ya nchi yao.

Wakati wa uhuru wake, Sudan Kusini ilitajwa kama moja wa mataifa masikini zaidi Barani Afrika. Nchi hii inaongoza na idadi ya vifo vya wanawake waja wazito na watoto. Aidha idadi kubwa ya wanawake hawajui kosoma na wala kuandika.


Mwaka mmoja baadaye nini kimebadilika?


Mwaka mmoja wa uhuru,Sudan Kusini imejipata katika mzozo na jirani wake Sudan hali iliyotishia kuzuka upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.


Kuna hoja kadhaa zinajitokeza wakati Sudan Kusini ikiadhimisha mwaka mmoja wa uhuru;

Je matarajio ya raia yameafikiwa au matumaini yaliyokuwepo siku ya uhuru yamedidimia?

Sudan Kusini inaweza kujinasua kutoka historia yake iliyokumbwa na ghasia?

Nini kitahakikishia mustakabali wa Sudan Kusini?
Ndio mjadala wa mwezi huu unaongazia Afrika ambapo BBC itakuwa mjini Juba ,Ijumaa Juni 29.

BBC Swahili - Kwa Kina - Sudan Kusini imefikia ndoto yake?


 
Back
Top Bottom