Suala la tanesco kutaka ushauri toka kwa wananchi:-

kamkoda

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
396
71
Nina mashaka kidogo na propaganda za shirika letu la umeme kutaka maoni kwa wananchi kwamba sisi tunataka shirika liweje. Kimsingi matatizo ya shirika hili ni ya kimfumo na kiutekelezaji ambapo inahitaji upembuzi yakinifu kwa maana kwamba ili mtu atoe ushauri elekezi stahiki...ni sahihi kwanza aingie ndani ya mfumo wenyewe uliopo austadi ndipo ashauri njia bora zaidi...Sijaelewa bado wao wana maana gani ama wanataka maoni ya kisiasa katika mambo ya kiufundi?...kuna makampuni makubwa sana ambayo yanaweza kuwapa ushauri wa kitaalamu kwa kutafuta suluhisho za kiufundi na kimfumo na ikawa ni suluhu ya moja kwa moja...Tanesco mkumbuke ushauri unalipiwa na si dezo dezo...ama ndio mnataka baadae mseme kuwa yalikuwa maoni ya wananchi mambo yatakapo kwenda kombo?...wekeni masanduku ya maoni kwa mambo ya huduma kwa mteja na myafanyie kazi. Leo nimeona kigamboni kuna nguzo zimefichwa sasa hata hilo mnataka maoni? Jisafisheni!!!...Mnalipwa mishahara na posho nzuri fanyeni kazi zenu muwe wabunifu nasi twafanya zetu!...sipati picha kila shirika la umma litakapotaka maoni kwa wananchi wakati si wana hisa!!!
 
Hawa wanataka kucheza mchezo wa kuigiza , wanaelewa sana! kuwa Consultant wengi wlishatoa ushauri,
 
Siyo mbaya nawe ukawapa ushauri. Kuwa consultant siyo paka uwe na vyeti, inaweza kushauri kitu na kama kikifanyika, tunaenda mbali.

Mfano mie nashauri wale wote waliohusika kulihujum wanyongwe, na wakinyonga hata wawili basi umeme utarudi kwenye nidham yake.
 
Back
Top Bottom