Wakuu naandika huku nina stress. Huwa ni mzito wa kuongelea mambo yangu ya mapenzi ila hapa JF naona ni sehemu sahihi ya kuomba ushauri kwasababu kila mtu yupo huru kwa feki ID.
Kiufupi mimi ni kijana mdogo wa miaka 37, mkristo na mwanachama wa CCM. Baada ya kumpata msichana tuliyependana nikaona anafaa kwa ndoa. Mkoa niliopo kikazi ni mkoa wa mbali kutoka kwetu. Nilipofikia uamuzi huu nikaona niwapigie wazazi simu na kuwajulisha kwanza nia yangu hii. Baada ya maswali kadhaa wazazi wakaona iko poa tunaweza anza mchakato wa kuelekea ndoa. Ila kwa upande wa mama ndo akaja na jambo linalonifanya niombe ushauri.
Mimi kwetu wasabato wazuri kabisa ila mimi binafsi tangu nikiwa na miaka 19 nilianza kwenda tofauti na usabato. Imefikia wakati ni kama tu sina dini. Siendi kanisa lolote kwa miaka mingi. Ikitokea nimeenda ni labda msiba, harusi au ibada nyingine maalum. Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitafuta sana kuhusu suala la imani kwasababu kwenye SDA siwezi kabisa. Siku za karibuni nimegundua moyo wangu upo kwenye misa ya kwanza ya Roman Catholic. Yaani najiona nikiwa imara kiroho na familia yangu tarajiwa ndani ya RC.
Huyu mchumba wangu ni KKKT ila mama yangu kasema hataki ndoa ya dhehebu lingine zaidi ya SDA (Sabato). Na hata nikilazimisha yeye hatakaa aifurahie. Kimsingi inaonekana baraka zake itakuwa ngumu kuzipata nikifunga ndoa kwenye dhehebu lingine. Hadi sasa sijafikia muafaka na mama.
Nishaurini wakuu.