Strategies for Tanzania's Economic Development

Koba na Bin Maryam,
Tuwe wakweli mkuu wangu let's face the truth na sio kusingizia Azimio la Arusha kwa kigezo cha mbinu alizotumia Mwalimu, bado tunao ng'ombe wetu wawili kinachotakiwa ni kuweka Azimio litakalo hakikisha ng'ombe hao wapo kwa faida ya wananachi wote na sio fungu la watu wachache.

Mkuu wangu give me a break, Mkapa kuwa kiongozi wa kusifiwa kweli?...

Mkanadara:

Mpaka hapa sina amabacho nigeongezea kwenye maelezo uliyotoa kwa hoja inayoedelea. Nimekuna kichwa nikajiuliza ni mimi sijui maana ya hili azimio la arusha au tunapishana wapi na wengine.

Nimemuelewa Mtanzania, nikisoma post za Kichuguu nazielewa... Zinanipa moyo kuwa kama kimsingi hawa wanaona kama ninavyona may be bado ninalijua Azimio la Arusha ni nini!

Uzuri wa JF tofauti na hizi yingine nilizozipitia kwa kipindihiki cha "mahangaiko ya Mapolisi" ni kuwa michango ni mingi na wakati mwingine ina vina kwelikweli. Ninafurahia JF kwa hilo.

Nafikiri nijipe muda kuangalia na kujifunza kwa undani wachangiaji wengine, nione mitizamo yao, niangalie kwa makini kabisa wanafikiri Azimio la Arusha ni nini. Bahati mbaya kabisa mimi sio mwansiasa kabisa. Na sikumbuki kufindishwa maana ya Azimio la Arusha mahali popote shuleni. Kama walifundisha basi sikuwa msikivu. Labda niliona ni kitu kisichonihusu..na kukiondolea mbali!!

Lakini hivi karibuni imebidi na imetokea nikaamua kufuatia kwa kina na mapana. Nikafikiri nimelielewa. ndio maana nikaona mtizamo inayofanana na ya baadhi ya post hapa, Nikaiona ni ok, Nikajisemea, kama ninawaelewa maoni ya badhi ya wenzangu ..nafikiri niko njiani..lakini nikaona pia kuwa kwa kutoelewa maoni mengine...nijibidiishe kujifunza Azimio la Arusha. Najipa muda!!!

Moyoni ninajua kabisa Kuna jambo ndani ya hili Azimio la Arusha. Na ninafikiri litaibuka wazi hadharani!!!
Sitegemei liwe photocopy ya lile cha 1967.... lakini kwa kuwa huu ni mfumo wa maisha ulio na structure, value na character it can come in any shape and form kutoa majibu muhimu ya ustawi wa maisha.

Na inawezekana maneno haya Azimio la Arusha yanapotosha ..kwani the tool and its system inaweza kuweko kwa ubatizo tofauti tu!! Lakini ikihudumia jamii kwa ufanisi mkubwa. Ni kama neno UMEME lisivyo husiana na KITU CHENYEWE. Na kulibadili neno umeme kwa maneno mengi kwenye nyakati tofauti na hali tofauti isivyo adhiri KITU CHENYEWE! Tutafute kitu chenyewe!
 
Koba,
sasa tunaenda mbele with free market Economy AKA capitalism...low taxes + less regulations + small government = innovations,freedom and prosperity
...

Sielewi haya ulozungumza yanahusiana vipi na hoja hii ya Azimio la Arusha. Zipo nchi za kibepari zenye serikali kubwa (tukianza na Tanzania yenyewe), tax kubwa (Canada), na regulation kibao kwa sababu hawahitaji wawekeshaji toka nje...Tanzania ya leo regulation kibao ndani ya nchi lakini sio kwa wageni...Hii yote ni katika kuhakikisha ng'ombe wote wanaliwa..i

Swala mkuu wangu tuna ngombe wawili, tufanye nini ikiwa leo hii mpango ni kula wote tunaomba msaada kesho. Kupiga madongo Azimio la Arusha hali huna Azimio kabisa ni sawa na Maskini anayelala msikitini akisubiri sala ya Asubuhi...Hayupo hapo kusubiri sala isipokuwa target yake kubwa ni kuomba msaada kwa waumini watakao jitokeza.

Sasa unapozungumzia Capitalism hali huna Azimio la kile unachotaka kujenga na utafanya nini kabla/baada ya hata kukipata ni uchuro mtupu...tutaitana wachawi hadi Kiyama...Ubepari hautafutwi hivyo mkuu, wenzetu wote walianza na Maazimio kama yetu kabla hawajafika hapa walipo. Ujenzi wa nyumba hii Capitalism haukuanza kwa kujenga paa, na tunayoyaona leo na kuyafurahia ktk Ubepari ni matunda ya Maaziomio mazito na kazi ngumu waliyoipitia hawa jamaa zetu...Kumbuka walianza na kodi za vichwa na kushika makoloni zaidi (vita) kuchangia kodi zao kukuza uchumi wa nchi zao...

Leo hii hawa watu wapo zaidi ya millioni 250 na mauzo ya mwaka kwa trillioni ya dollar unataka kulinganisha asilimia ya makusanyo ya kodi zake na Tanzania ati kwa kutumia Capitalism...Mkuu siku zote utajipima koti kwa umbo lako na sio kuiga uwezo wa tembo ktk kushusha kipudu...Utapasuka msamba!

Mkuu wangu hata sisi wengine hapa tulikuwa na mashamba yetu na hayakuchukuliwa hata moja ila yamekuja chukuliwa wakati wa Mkapa walidai upanuzi wa mji na barabara. Hizo habari za wananchi kuchukuliwa mashamba yao nimezisikia hivi karibuni kuliko wakati wowote ule na nakuhakikishia kuwa Azimio la Arusha liliweka msisitizo zaidi ktk kilimo. Kila nyumba (familia) wakati huo walikuwa na shamba somewhere, na hata wafanya kazi serikalini na mashirka ya Umma walilazimika kuwa na mashamba yao binafsi.


Mashamba yaliyochukuliwa na serikali yalikuwa mashamba ya walowezi tena bidhaa za mauzo (cash crops)..Kwa kutazam picha ya mafanikio kwa uchache tu naweza kwambia kuwa pamoja na kidogo walichoweza pata ktk kilimo hicho kila mzazi wetu aliweza jenga nyumba, hata kiwe kibanda. Leo hii nambie mnafanya kazi Benki tena Ofisa lakini huwezi kununua hata kiwanja Kimara juu..sii swala la kukosekana viwanja, hawana uwezo, Lowassa na wenzake wana ma hekalu bila kuzalisha kitu wala kutoka jasho!

Kwa hiyo hizi shutama zako hazina sura kabisa mkuu wangu, labda huko ulikotoka wewe.
 
Koba na Bin Maryam,

Naomba liweke Azimio la Arusha hapa kisha tujadili maanake unachojaribu kujenga hapa ni jinsi tulivyojenga Azimio hilo badala ya kutazama Azimio lenyewe..

Mthalan, Ukiwa na Azimio la kujenga Nyumba kwa familia yako, haina maana utatazama Azimio hilo kulingana na nyumba ya Mjamaa mzee kibule aliyeezeka nyumba yake kwa udongo. Laa Azimio ni zile fikra za ujenzi wa nyumba na kwa ajili gani sasa unaweza jenga nyumba leo hii kwa azma hiyo hiyo na ikawa ktk hali ya kileo na kwa ajili ya falimia yako..

Pili, Msisitizo kwa wana familia nzima kushiriki ktk ujenzi wa nyumba hiyo haina maana ni lazima kila mmoja abebe tofali kama ilivyosemwa na Michuzi kule kwenye uchumi wa Kirusi...COWMATICS - Laa hasha, kushirki kwa wananchi ktk azma hiyo kunaweza kuwa ktk hali nyingi na tofauti maadam wananchi wote wenye uwezo wa kufanya kazi wanawezeshwa ili kujenga kile mlichokusudia.

Kama alivyoelezea mwandishi kule kwa Michuzi, tatizo la Tanzania tuna ng'ombe wawili tunakula wote kisha tunaomba msaada.... Azimio ni kuhakikisha ng'ombe hao wanaboresha maisha ya wananchi, mikakati itakayo tumika ni sera za kila chama lakini tukiwa na malengo endelevu.

Mwisho mkuu wangu, swala hapa ni kuondoa - Confict of interest, Azimio la Zanzibar halikuja na hoja yoyote mpya zaidi ya kuhakikisha ngo'mbe wote tunaopata wanaliwa...

Nimeshangazwa na hivi vifijo vya ujio wa Bush kuwa tumepata mikopo hali Wadanganyika wanafahamu kuwa Tanzania tumekuwa tukipata mikopo ya Mellenium Challenge toka utawala wa Mkapa, Bush alipounda Account hiyo. Tumepokea mabillioni enzi ya Mkapa na tena kapewa sifa kubwa kuwa ni kiongozi pekee ktk Africa na nchi masikini aliyepigana na Corruption,.. hiyo ni 2003 -2004! sasa leo hii tunashangilia haya bila kufahamu kuwa Bush kampa mgonjwa wa Kijugu (drug addict), fedha za kwenda lewa zaidi.

Tuwe wakweli mkuu wangu let's face the truth na sio kusingizia Azimio la Arusha kwa kigezo cha mbinu alizotumia Mwalimu, bado tunao ng'ombe wetu wawili kinachotakiwa ni kuweka Azimio litakalo hakikisha ng'ombe hao wapo kwa faida ya wananachi wote na sio fungu la watu wachache.

Mkuu wangu give me a break, Mkapa kuwa kiongozi wa kusifiwa kweli?...

Mkandara:

Nadhani mada ni mikakati ya maendeleo. Toka tumepata uhuru mikakati ilikuwepo na mingi ilikuwa inapangwa na viongozi na sisi wananchi tulilamishwa kufuata. Na moja ya hayo ni Azimio la Arusha.

Mtu mmoja anakaa mezani na kuandika jinsi nchi itakavyokuwa bila mjadala na bila kuangalia matatizo yatakayotokea iwapo kile anachoandika kitashindwa.

Kuhusu mfano wako wa ng'ombe hauniingii akilini. Je ukila ng'ombe wote na kupata nguvu ya kwenda kuiba ng'ombe wengine kumi kutakuwa na matatizo gani?
 
Bongolander:

Azimio la Arusha ni kwa masochists, watu wanaopata raha kwa kupewa maumivu.

Hiko proved kuwa competition inaongeza innovation. Azimio la Arusha lina-discourage ushindani kiasi cha kuleta uzezeta kwa vijana wa kitanzania. Utingo analipwa sawa na daktari.

Wanaotaka Azimio la Arusha safari hii wajiandae na mapambano ya ideology na ngumi.

Bin Maryam,

Ukisoma Azimio, limitation ziko kwenye viongozi ambao walikuwa na upper hand kwa madaraka. There is no where in Azimio ambapo lilizuia ushindani katika jamii zaidi ya Viongozi.

Ndio ni kusadikika kujenga jamii iliyo sawa. Lakini mandhari ya Tanzania wakati tunatangaza Azimio hata leo hii, kuna haja ya kutoa nafasi sawa ili kujenga Taifa imara. Ziwe jitihada binafsi kuwa na nyongeza katika uzalishaji mali.

Mchaga na Mhaya wao walilima mpaka ziada na kuuza kwa majirani. Mgogo na Mzaramo wao walilima kwa kuhemea, kilimo cha kula leo, kesha ajua Mola!

So Azimio was not prohibitive to competition, it was restrictive to the leaders from exploiting the mass. In turn, these leaders decided to use articles meant to them to suppress everyone and this is where Nyerere failed short by allowing viongozi to mis-intepret the Azimio and suppress Juhudi na Maarifa kwa wananchi na kuwa washindani!
 
Tanzania hili itoe huduma za shule tu inabidi kuomba au kukopa madeni yasiolipwa. Na ukiwaongezea kodi watu ili walipe gharama zao, wengi wako tayari kurudi kwenye maisha yao ya ujima kuliko kulipa gharama zenyewe.

Azimio la Arusha halina uzuri wake (period). Ukienda kwa watu masikini na kuwapa ahadi nzuri za maisha bora, wapo tayari kukubali mawazo yao. Na kukubaliana kwao kutatokana na wao kufikiri kuwa wanaweza kuruka umasikini wao bila kufanya juhudi kubwa.

Hivyo basi si azimio au sera za ujamaa zilikuwa ni mbovu, bali ni watu na tabia zao (tamaduni) kama ulivyosema hapo juu, kukimbilia ujima badala ya kukabili hali halisi na kuchangia gharama.

Nakumbuka jinsi Serikali ilipoleta mambo ya wananchi kuchangia elimu na afya, kila mtu hata wale wenye uwezo walilalamika kuwa hawawezi kulipia na kukimbilia ujima.

Tunahitaji mfumo wa kulazimisha watu wawe wanajenga jitihada na ikiwezekana basi extreme measures zitumike mfano kuacha wadorore na kuteketea!
 
Mkandara,Azimio la Arusha was a sad and failure chapter for our country,sasa halipo na believe me halitarudi tena labda insane people waamue kulirudisha lakini ujue it'll be blood kuja kuchukua shamba na nyumba yangu kama mlivyofanya 1967,na sijui kwanini mnataka kurudisha stupid policy za 1967 ambazo ukweli ndio zimetuongezea njaa tuu,sasa tunaenda mbele with free market Economy AKA capitalism...low taxes + less regulations + small government = innovations,freedom and prosperity,upo hapo mkuu sasa tuache hadithi za kudhulumiana mashamba na nyumba za 1967 hapa!

Koba,

Lets say we stop asking for Azimio, what economic policies and strategies do you think will make Tanzania improve economically and financially? Do the FME policies you are advocating working for us? if they do how? if they are not how and what are the alternatives?

What are the social policies that are currently pushing and unifying Wananchi to be more productive and innovative if we keep Azimio on back burner?

Let us for a minute stop criticising Azimio as failure and cause of complete collapse of Uzalishaji mali and hear from you opponents of Azimio your Social Economical programs and mechanism that can revamp Uchumi and start fighting Umasikini.
 
Mkandara:

Nadhani mada ni mikakati ya maendeleo. Toka tumepata uhuru mikakati ilikuwepo na mingi ilikuwa inapangwa na viongozi na sisi wananchi tulilamishwa kufuata. Na moja ya hayo ni Azimio la Arusha.

Mtu mmoja anakaa mezani na kuandika jinsi nchi itakavyokuwa bila mjadala na bila kuangalia matatizo yatakayotokea iwapo kile anachoandika kitashindwa.

Kuhusu mfano wako wa ng'ombe hauniingii akilini. Je ukila ng'ombe wote na kupata nguvu ya kwenda kuiba ng'ombe wengine kumi kutakuwa na matatizo gani?

Bin Maryam,

Okay you are right on this one. What do you propose? what is your plan? i think it is time that we hear from you solutions and plans rather than constant criticism on Azimio and Nyerere failures!
 
introducing a policy like China where by no foreign company can own a business in China, companies must form a joint venture with a local company if they want to do business there, the can own no more than 50% of any shares in a company. Kama hawataki basi yaache madini na maliasili zetu zibaki huko ardhini. We have something they need and now its about time Tanzanians to use that as a bargaining chip. (no more excuses of sijui oooh kulikuwa na ukame ....in order to get us in these shady business deals)
 
Jaribuni kufanya bishara TZ ndio mtagundua ninachoongea kuhusu hizo regulations & taxes ambazo ni product ya siasa zetu.

Nakuhakikishia bila dirty tricks & corruptions utafunga biashara the next day, na kumbe kitu gani msichoelewa kuhusu small government huku nyie ndio wapiga kelele wakubwa wa baraza la Jk la mawaziri 60 wengi wao hawana akili na VXs zaidi ya 10000 za serikali...wewe tupatie low taxes + less stupid regulations then utaona jinsi watu watakavyofanya kazi kwa bidii.

Na wewe Mkandara hizo nchi zinazochukua Tax kubwa at least hiyo Tax inaonekana inaenda wapi,Germany wanachukua 40% lakini Elimu bure mpaka University, health care is almost free na infrastructure ziko tight, wabongo wanachukua wanaenda kuongeza VX za serikali sasa hapo wapi na wapi.
 
From our meagre resources we have, for sure we do not have much choice of which strategies to implement.

I would quit misallocating resources on basic tourism.

My strategy, to start with is to invest in processing (usindikaji) industry, especially of agricultural produce. Along with that, there should be in place policy of protectionism of these infant industries againt the competitive advantages of multinationals.

Mkuu sana Invincible,
Kabla ya kusoma mchango wako, nilikuwa najiandaa kuandika mkakati ambao mie ningeupendekeza. Lakini baada ya kusoma wako imekuwa kama umesoma wazo langu kuu siku zote.

NAKUUNGA MKONO KWA 100%
 
Mkandara:

Kuhusu mfano wako wa ng'ombe hauniingii akilini. Je ukila ng'ombe wote na kupata nguvu ya kwenda kuiba ng'ombe wengine kumi kutakuwa na matatizo gani?

Bin Maryam;

Mfano ulikuwa unasiamia kuonyesha two aspects za development. Kuwa; Unahitaji kitu cha kwanza cha kuanzia "starter" kama hatua ya kwanza na hatua ya pili ni “jasho”, jitihada, maarifa na good manegement kufanya the stater kuwa expected product.

Kuwa na mental set up inayo kuelekeza kwa makusudi ku extinguish starter.... na kuwala Ngombe wawili... Kwa kuwa Utawaiba wengine ni tatizo la kiutu. Pili wizi huo si chelei kuuita ni kukiukwa kwa moral values.

Hatuwezi kutafuta maendeleo kwa udi na uvumba yaani hata ikibidi kuvunja maadili na haki za kibinaadamu.

Set up ya azimio la arusha ilikuwa imetake care all those measures. Yaani maadii ya utu na hatimaye ya uongozi katika kujenga uchumi. Usingekaa na kufikiri kula mavuno yote ya msimu huu simply ulikuwa na uwezo wa Kuiba mbegu za mahindi kwa jirani. Au tuseme kwa kuwa unauwezo wa kuiba ng’ombe wengine.

Mitizamo kama hiyo ikiachiwa ndio inatupelekea hapa tulipo. Kila kiongozi anaona ni rahisi na sawa tu kuiba ili kukuza mtaji wake. Miiko ya maadili na usawa katika utu amabayo ni nguzo kuu ya azimio la Arusha vilihakikisha hilo halitokei katika harakati za kujenga maendeleo ya jamii. Na leo jamii inadai maadili hayo kwa kasi ya ajabu. Hata bunge lililokuwa limelala sasa limepata pa kuibukia.

You know what?

"Mind set ya maadili na utu" vilivyokuwa vinajengwa kwenye azimio la arusha kwa kumfunza mtu uvumilivu na subira ya kutokula ”Ngombe” wawili wa mwisho, pamoja na maumivu na kuhitaji kujitolea kwa dhati ili kuyaweza..lakini ndio msingi wa kumtofautisha binadamu na mnyama. Na imegundulika kuwa are the same “social forces” zinazodaiwa na ugonjwa wa ukimwi ili kupunguza maambukizi na kurefusha maisha ya mgonjwa.

Ukimwi kama natural social force inamdai mwanadamu utu, ubinadamu, uwezo wa kujinyima, kuvumilia, subira etc ili kunusuru taifa kuteketea. Cha ajabu? Hizo ndizo nguvu ndani ya azimio la Arusha ambazo zinakimbiwa na wengi. But tutakimbiaje ukimwi/Magonjwa yanayodai traits za azimio la Arusha kama social remedy? Ni kupitia uchumi na mtindo wa maisha uliosimamia maadili ya utu na uliotandaa kwa kila familia utakaoweza kuzuia sehemu ya maambukizo mapya. Nani haoni hilo? Na hapa kwetu njia iliyotandaa kwenye kila familia ambayo unaweza kujegea uchumi wa aina hiyo ni “KILIMO” kama ilivyoainishwa kwnye Azimio la Arusha.


Hatuwezi kuua utu na maadali yake ili kujenga uchumi maana tukifika angaza kabla ya kupewa dawa za kurefusha maisha wanatudai tujifunze kutokuiba mali au “watu”, tuwe na utu tusiambukize wenzetu, tudumishe maadili ya kifamlia, maadili ya kazi, uongozi na maadii katika kujenga uchumi. Kwa hiyo leo dawa zinatudai utu ili zifanye kazi yake. Sasa itakuwaje Uchumi usiojali, usawa na utu kwanza? Wenye nacho siwatawaambukiza wasio kuwa nacho na kutekeketeza Taifa?

Kama una "jicho" sahihi ona Angaza wanacho advocate. Ni basic traits au componets mihumu ndani ya azimio la Arusha.
 
..Maoni ya Jenerali Ulimwengu kuhusu yaliyojiri wakati wa Azimio la Arusha na siasa za Ujamaa.

Tumemwaga maji machafu pamwe na mtoto?

Jenerali Ulimwengu Februari 20, 2008

NIMESEMA awali kwamba, pamoja na sifa zote nilizozitaja (na nyingine nyingi) Mwalimu Julius Nyerere hakuwa mwana-demokrasia. Nasema hivyo nikijua kwamba hili linaweza kuhitaji maelezo, nami sina tatizo na hilo.

Kwanza kabisa ni muhimu nieleze ni kwa nini ninahusisha moja kwa moja sudi ya nchi na mtu mmoja, kiongozi mmoja wakati tunajua kwamba nchi hujengwa na watu wengi, mamilioni, na mustakabala wake huundwa na kila aina ya mikondo ya nishati zinazokutana katika mchakato ambao mara nyingi haufuati msitari ulionyooka.

Nimekwisha kuzungumzia kile nilichokiita zama za Bwana Mkubwa na chama-tawala tulizokuwa nazo baada ya Uhuru, na hizi zama zilizikumba nchi zote za Afrika, bila kutofautisha. Leo hii tunaweza kusema kwamba hali imebadilika sana, hasa kutokana na kufunguliwa milango ya siasa inayoruhusu, angalau kidogo, raia kujiunga katika vyama vya siasa wanavyovipenda au kuanzisha asasi za kijamii zinazokidhi matarajio yao.

Lakini, hata hivi leo, nafasi ya kiongozi mkuu bado ni kubwa mno barani Afrika kwa sababu asasi zetu za utawala na uongozi bado ni changa, mifumo yetu ndiyo kwanza tunaijenga na itachukua muda kidogo kabla hatujawekeza matumaini yetu kwenye mifumo, asasi na taratibu zaidi kuliko kutegemea fikra na busara za kiongozi mkuu.

Huko tulikotoka hali ilikuwa ni ngumu zaidi. Hata pale tulipomchagua kiongozi wetu (mara nyingi kwa sababu yeye alikuwa miongoni mwa wachache waliodiriki kutuambia kwamba tunaweza kuung’oa ukoloni) bado mtu huyo mmoja alikuwa na nguvu na ushawishi kuliko asasi alizoziongoza. Mara nyingi rais wa nchi ya Kiafrika alikuwa na nguvu na ushawishi mkubwa zaidi kuliko katiba ya nchi, sembuse taratibu nyingine zilizowekwa kwa misingi tuliyofundishwa na wakoloni wakati wakiondoka.

Kwa jinsi hii, viongozi wakuu wa Afrika ambao tunawakumbuka kwa ushujaa wao na uwezo wao wa kuona mbali (Nkrumah, Toure, Nasser, Nyerere, Kaunda) wote hawakuwa wana-demokrasia, kimsingi kwa sababu nyakati hazikuwapa fursa ya kuwa wana-demokrasia.

Kilichohitajika wakati ule kilikuwa ni maendeleo ya haraka ambayo yangetuondoa katika hali mbaya ya umasikini, maradhi na ujinga; hatukuhitaji mabishano na ukinzani wa kisiasa ambao ungetukawiza katika jitihada za kupata maendeleo.

Huo ndio ulikuwa mtazamo wa zama hizo, na mtazamo huo ndio uliozaa urais-ufalme, au kile kinachoitwa ‘imperial presidency’.

Tukiangalia kidogo tu, hata leo, tutagundua dalili nyingi zinazoonyesha ‘ufalme’ huu ndani ya urais, pamoja na kwamba tunatamba kwamba tumeimarisha demokrasia, tumejenga asasi, na nchi zetu ni huru zaidi kuliko zilivyokuwa miongo minne iliyopita.

Tunaweza kusema leo kwamba ilikuwa haiepukiki kuwa na kiongozi wa aina ya Julius Nyerere, ambaye yeye mwenyewe aliwahi kusema kwamba kwa katiba ya nchi angeweza kabisa kuwa dikteta (wapo wanaosema kwamba hivyo ndivyo alivyokuwa). Kwa vyo vyote vile Nyerere alikuwa ndiyo Tanzania, na Tanzania ilikuwa ni Nyerere, si tu wakati akiwa madarakani bali hadi alipoaga dunia…. na labda hadi leo hii.

Katika mazingira kama haya, hata sera nzuri kama zile zilizotangazwa katika Azimio la Arusha na baada yake, pamoja na programu kadhaa za utekelezaji wa sera hizo zilitangazwa na kutekelezwa katika mazingira ambamo fikra za mtu mmoja zilikuwa na uzito mkubwa kuliko ambavyo ingekuwa katika mfumo wa kidemokrasi. Yeye ndiye aliyefikiri; yeye ndiye aliyetunga sera; yeye ndiye aliyeamua vipi zitekelezwe; yeye ndiye aliyeamua nani azitekeleze.

Hii ilikuwa na maana kwamba iwapo jambo alilitia maanani jambo hilo lilishughulikiwa kwa ari kubwa na kila aliyekuwa chini yake; iwapo jambo hakulitia maanani, hata lingekuwa ni la muhimu sana, jambo hilo halikupewa uzito; iwapo alimwamini mtendaji, mtendaji huyo alishamiri; iwapo hakumwamini, mtendaji huyo hakushamiri.

Kama alivyosema Nyerere mwenyewe, madaraka makubwa mno yaliwekwa mikononi mwa Rais, hali ambayo bado tunayo hivi leo, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa watendaji hadi ngazi ya wilaya. Baraza la mawaziri likawa (na hadi leo) ni baraza la ushauri kwa Rais. Hakuna kinachofanyika bila yeye.

Azimio la Arusha lenyewe lilikuwa kwa kiwango kikubwa ni azimio la Nyerere, ingawaje lilipitishwa na Halmashauri Kuu ya TANU, na kwa kuungwa mkono na maelfu ya Watanzania, likawa azimio la Watanzania wote. Ukweli ni kwamba hakukuwa na mjadala uliowahusisha wananchi (au hata wana-TANU) katika utungaji wa azimio lenyewe wala katika mbinu za utekelezaji wake.

Mwaka 1968, tutakumbuka, walichomoza wabunge kadhaa waliotaka kufurukuta na kuihoji TANU ndani ya Bunge la chama kimoja. Alichofanya Nyerere ni ‘kuwashitaki’ wabunge hao (Kaneno, Bakampenja, Choga, Masha, Anangisye, Mwakitwange) ndani ya vikao vya chama. Wakanyang’anywa uwanachama wa TANU, na hivyo wakapoteza ubunge.

Huo ukawa ndio mwisho wa kutaka kuhoji cho chote ndani au nje ya TANU. Wengi wa wabunge hao machachari wa wakati huo wamekwisha kufariki (lakini walikuwa wamekwisha kufa kisiasa muda mrefu kabla ya kuaga dunia), ukimwacha Masha, ambaye sasa ni mbunge wa Afrika Mashariki baada ya miaka mingi ya kuishi uhamishoni-laini katika Umoja wa Mataifa.

Hakika ilianza kusadikika kwamba ukipata laana ya Kambarage ujue umemalizika kisiasa, imani ambayo imezidi kujengeka katika miaka ya karibuni.

Utamaduni ulioanzishwa wakati wa Nyerere umeendelea ndani ya chama-tawala kiasi kwamba majadiliano ni nadra sana, na mara nyingi mijadala huzuka ili kumshughulikia mtu fulani, na wala si kusaili hoja wala falsafa. Athari mojawapo ya utamaduni huo ni kwamba hivi sasa, Nyerere akiwa hayupo, hakuna kiongozi hata mmoja, hata wale waliokuwa safu ya mbele kabisa katika kuhubiri Ujamaa leo hii huwezi kuwatambua.

Hali hii ilianza kujitokeza hata wakati Mwalimu akiwa madarakani. Kadri umri ulivyoongezeka na nguvu za mwili kupungua ndivyo kasi ya kusimamia sera na utekelezaji wake ilivyoendelea kupungua, kiasi kwamba chama na sera zake vilianza kuonyesha uzee kadri nywele za Mwalimu zilizvyozidi kuwa nyeupe.

Katika hali ya kutokuwapo na mjadala, sera zilizolenga kumkomboa Mtanzania zikaishia kumletea matatizo ambayo yaliupa Ujamaa jina baya. Serikali ikajiingiza katika biashara isiyokuwa yake – kuuza nyama na chumvi; vyama vya ushirika vikavunjwa; serikali za mitaa zikafutwa, na kadhalika.

Leo hii ni vigumu kujua CCM imesimama wapi. Ni dhahiri kwamba sera za Ujamaa zimetupwa, hata vipengele ambavyo vingeweza kuwa na manufaa leo. Katika mkanganyiko uliotokana na utekelezaji mbovu wa sera za awali, viongozi wa CCM wameamua kumwaga maji machafu pamoja na mtoto, lakini kimya kimya.

Hawathubutu kusema kwa sauti kubwa kwamba falsafa yao ni Ujamaa, na wala hawathubutu kusema wazi kwamba wameachana na siasa hiyo. Chama hakina dira wala mwelekeo, na kila kukicha kinafanya kile kinachoonekana kufaa kwa siku hiyo.

Athari nyingine ya hali hiyo ni kwamba ukosefu wa falsafa-ongozi umekivua chama-tawala ile taswira ya kuwa mtetezi wa wanyonge. Uongozi na utetezi wa wanyonge unahitaji falsafa inayowaongoza viongozi wenyewe kwanza, falsafa inayopingana na ugandamizaji wa kila aina, unyonyaji wa kiuchumi unaomdhulumu mtu wa chini (ndani ya nchi) na udhalimu unaofanywa na mataifa makubwa na mitaji yao(nje ya nchi). Utetezi wa wanyonge hauna budi kuandamana na msimamo dhidi ya ubeberu na ukoloni-mamboleo.

Hii ina maana ya kutegemea nguvu ya wananchi walio wengi wanaojiunga na chama, na michango yao, hata kama ni kidogo. Badala yake, tunachokishuhudia ni chama-tawala kugeuka chama cha matajiri wachache ambao ndio wanakibeba kifedha, na vivyo hivyo serikali ya chama hicho kuwa tegemezi kwa misaada ya mataifa ya nje kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
 
I believe in Education nothing else,
Maana strategies must be configured in hierarchical model with full of protocals.
kama huna wasomi hizo protocal hawatazielewa wala kuzifuata na hatima yake the failure of whole system.
Mkamap, education bila uzalendo wa hao wasomi hauna maana yoyote.... academicians na wengineo mbalimbali tulionao ndani ya Taifa letu wangetosha kabisa kulisukuma Taifa letu a 2 step ahead. Tunachokosa kwa wasomi wetu ni uzalendo.
 
Game Theory,

Naomba maoni yako kuhusu nguvu na tofauti kati y Cash economy na Credit economy.
 
Hivi tukibadilisha mfumo wa malipo ya mishahara Tanzania mathalani kuwa lipa watu mara mbili kwa mwezi badala ya mara mmoja kunaweza kutusaidia kuongeza ufanisi na kupunguza rushwa?
 
Rev. Kishoka,
haya matatizo ya Marekani kama yangekuwa Bongo tunaweza kutoka kweli?....
Duh, sijui Koba atasema nini kuhusiana na Ubepari maanake uliubebea bango bila kufahamu kwamba Ubepari nao una nyufa mbaya sana ambazo nchi kama Tanzania ikija shikwa na matatizo kama hayo ndio kitakuwa kifo cha nyani!...

Bin Mayram,
Mkuu hivi kweli unafikiria kula ng'ombe wako ili upate nguvu ya kwenda kuiba ng'ombe wa mtu mwingine... mtu mwenyewe unayemkusudia kumwibia nani?... Mmasai na pinde zake!
 
Hivi tukibadilisha mfumo wa malipo ya mishahara Tanzania mathalani kuwa lipa watu mara mbili kwa mwezi badala ya mara mmoja kunaweza kutusaidia kuongeza ufanisi na kupunguza rushwa?

Rev., tukifanikisha hilo katika sekta binafsi basi hata mfumo wa malipo kwa saa nao utawezekana. Isitoshe, takwimu zinaonesha kuwa sekta binafsi tanzania ndiyo mwajiri mkubwa kuliko zote (sorry no ref.)
 
well, Steve unajua umeileta hii thread nilishaisahau

anyway nitarudi kuchangia baada ya muda
 
Mkamap, education bila uzalendo wa hao wasomi hauna maana yoyote.... academicians na wengineo mbalimbali tulionao ndani ya Taifa letu wangetosha kabisa kulisukuma Taifa letu a 2 step ahead. Tunachokosa kwa wasomi wetu ni uzalendo.

Wasomi wetu wana uzalendo mkubwa sana! Kama wasingekuwa Wazalendo, wasingeshinda ndani ya JF wakijadili mustakabali wa taifa letu!

Tatizo kubwa ni wanasiasa wetu ambao wengi wao, nachelea kusema kwamba, si wasomi! Siasa zetu zimejaa watu wababaishaji huku wasomi wengi wakijiengua kutoka kwenye siasa na kufanya kazi zao zingine za kitalaamu zaidi, ndani na nje ya nchi!

Siasa zimeachiwa watu ambao wanafanya kazi kwa kujipendekeza kwa wakubwa, baadhi yao ni washirikina wakubwa, na hivyo kuwatisha watu wengine ambao wana njia za kujikimu na kuendesha familia zao pasipo mambo yanayofanana na hayo!

Hebu niambie, uzalendo gani unahitajika kumhudumia mgonjwa pale Muhimbili huku ukiwa huna gloves, wala vitendea kazi vingine, wakati misafara ya viongozi wa nchi inaandamana na kuchoma mafuta ya serikali kila siku bila sababu za msingi?

Ni nani atakuwa mzalendo wa kujitoa kufundisha wanafunzi 400 ndani ya madarasa mawili, halafu mshahara wake unacheleweshwa kwa miezi zaidi ya 7?

Ni askari gani ambaye anaweza kuwa mzalendo kiasi cha kutosha kulinda usalama wa raia wakati mshahara wake ni mdogo, na anaishi kwenye nyumba ya mabati kuanzia chini mpala juu!!?
 
Back
Top Bottom