Steven Kanumba Ndani ya Radio Mbao!

Jazzie

Member
Jan 30, 2008
73
35
KOMBOLELA SHOW JUMAMOSI HII January 30, 2011 @ 01:00pm - 02:00pm EST, 9:00pm -10:00pm East African Time

Kama wewe ni mpenzi wa sinema, na hasa sinema za Kitanzania, jina la Steven Kanumba “The Great” si geni. Kanumba amethibitisha kwamba ni muigizaji mahiri, jambo ambalo ushahidi wake ni tuzo mbalimbali ambazo ameshinda, ikiwemo Muigizaji Bora (2006) na Msanii Bora (2007).

Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Steven Kanumba kufahamu mambo mengi yanayomhusu binafsi, lakini vilevile mambo yanayohusu sanaa ya uigizaji wa filamu nchini Tanzania.

Jiunge nasi kwa kupitia hapa: Radio Mbao ili usikose uhondo!
 
Back
Top Bottom