Steve 'Nyerere' Aingia rasmi kwenye siasa... Awa kamanda wa vijana wa CCM-Bwawani

Juzi juzi alikuwa akisema eti hawatakuja kupata Rais bora km Jeikey
hizi ndizo IQ za masupaster wetu,hatareeee
 

Nimeshtushwa sana na matumizi ya fedha za akiba maalumu (escrow account) iliyokuwa benki kuu (BoT). Nikiwa mwenyekiti wa kamati ya PAC nina haya ya kusema; Mwaka 2006 Rais Jakaya Kikwete aliagiza kwamba, ili kumaliza kabisa suala la mkataba wa kuuziana Umeme wa IPTL, mitambo ya kampuni hiyo ichukuliwe na Serikali. Mwaka 2006, 2007 na 2008 Kamati ya BUNGE ya Nishati na madini imekuwa ikitoa maagizo hayo hayo kuhusu suala la IPTL. Mwaka 2009, Aprili 30 Kamati ya Bunge ya POAC ilipeleka mapendekezo bungeni kwamba IPTL ichukuliwe na serikali na fedha zilizopo katika escrow account zitumike pia kubadili mtambo ule kutoka mafuta mazito kwenda kutumia Gesi Asilia. Pendekezo hilo lilipitishwa na Bunge na POAC ikatoa maelekezo maalumu kwa Gavana wa Benki Kuu kuwa fedha zilizopo escrow account zisitumike kwa namna yeyote ile bila mitambo ya IPTL kuwa ya umma na kubadilishwa ili itumie Gesi Asilia.
Chanzo cha escrow account?
Baada ya mkataba wa IPTL kuingiwa, iligundulika kuwa kuna udanganyifu mkubwa ulifanyika katika kiwango cha mtaji wa kampuni hiyo na hivyo kufanya malipo wanayolipa tanesco kwa IPTL kuwa makubwa mno. Wakati katika kukokotoa gharama za uwekezaji (capacity charges) mtaji uliowekezwa katika IPTL ulisemwa ni dola milioni 36, ukweli ni kwamba IPTL waliweka dola 50 tu. Hivyo capacity charge ya dola milioni 3 kwa mwezi haikupaswa kulipwa yote kwani kampuni iliendeshwa kwa mkopo kuliko mtaji wa wawekezaji ( debt financed and not equity financed). Hivyo, mahakama ya kimataifa ya ICSID ikaamua kuwa, fedha zote za capacity charges ziwekwe Benki Kuu mpaka gharama halisi ziamuliwe na mahakama ndio wahusika wagawane (tanesco na IPTL). Akiba hiyo, nimeambiwa, ilifika dola 250m kabla ya kuchukuliwa na kugawanywa kwa wanahisa na wanunuzi wa IPTL. Hivyo kabla ya mgawo huu ilipaswa pesa ambazo tanesco walikuwa wanalipa kama ziada ya capacity charges kwa IPTL zirejeshwe kwanza na zinazobakia ndio zilipwe kwa wadai (creditors) na wanahisa. Kwa hali ilivyo sasa mnunuzi wa IPTL kapewa mitambo na fedha za kuinunua, ikiwemo fedha za tanesco ambazo zilipaswa kurejeshwa (Richmond cha mtoto kwa kweli).
Maswali ya kujibiwa ni haya;
Je, ziada ya fedha za malipo ya capacity charges zimerudi tanesco?
Je, mwekezaji Mpya kapewa mkataba Mpya wa kuuza Umeme (PPA) kwa utaratibu gani wa zabuni?
Je, agizo la Rais na BUNGE kwamba Mitambo iwe ya umma limetupiliwa mbali kwa vigezo gani?
Wizara ya Nishati na Madini na Benki Kuu wametoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu masuala haya? Wizara itoe taarifa, CAG akague
Kwa namna yeyote ile CAG anapaswa kukagua mchakato huu na kuweka majibu kwa umma kupitia kamati ya PAC. Hii ndio njia bora zaidi ya kuondoa wingu katika suala la IPTL ambalo toka limeanza miaka ya tisini limegubikwa na mazongezonge ya rushwa na uvundo wa kifisadi. Uwazi utatoa ukweli na kuwezesha uwajibikaji wa fedha za umma. Wakati mchakato wa ukaguzi unafanyika ni vema Wizara ya Nishati na madini itoe tamko rasmi.
Zingatia:
Kwa mujibu wa mkataba kati ya TANESCO na IPTL capacity charge inapaswa kukokotolewa kwa kuzingatia mtaji wa asilimia 30 na mkopo wa asilimia 22.31. Mtaji wa IPTL ulikuwa $50 tu, tofauti na $36 milioni zilizotajwa kwenye mkataba na kuamuliwa na mahakama. Badala ya TANESCO kulipa ‘capacity charge' ya dola 50,000 kila siku Umeme uzalishwe au la, udanganyifu wa mtaji ulipelekea TANESCO kuwa inalipa dola 100,000 kila siku tangu mwaka 2002. Kuanzia mwaka 2007 fedha hizo zilianza kuwekwa kwenye akaunti maalum (escrow account) BoT.

SOURCE: Zitto kabwe
 
Katiba mpya iruhusu watu wenye elimu ya degree na kuendelea na ambao ni wanachama hai wa chama cha siasa kuwa miaka isiyopungua mitatu ndio wawe wagombea wa nyadhifa za kisiasa. Na idadi ya wabunge isizidi wabunge 120.. Vinginevyo tutaishia kuruhusu watu ambao ni mazuzu kisa majina yao yanatajwa kulia siku kwenye vyombo vya Habari ndio wawe wabunge.
 
Kachoka kuzika kila siku analia timing 2015

hapo nimempenda bra nani anataka kyzika kilasiku loh
 
ccm ni kazi tu, hapo hapo kijana akaanza kuunguruma...
steve+nyerere1.jpg


mgeni rasmi akizindua shina lililopewa jina la steve nyerere....paul makonda at work
6.jpg


bongo movie huwa hawabaki nyuma, linapokuja tukio la ccm au la kitaifa wakamsindikiza kijana wao.
1.jpg


ndani ya mavazi matukufu ya ccm....ni raha sana na unajiamini.
7.jpg


silaa za ajadi hutumika katika kuwasimika makamanda wa ccm...
9.jpg


4.jpg

huyusijamaa wa vipochi bungeni ama nikumbusheni kidogo
 
hawa bongo muvi ni miongoni mwa wanafiki kila uchao wansemaka serikali inawatupa kwa kutowasaidia kulinda kazi zao lakini haohao wanajiunga na ccm ambayo ndio inamiliki serikali inayo waburuza kwali nimeamini njaa mbaya sana.

Acha ufala unataka wakamuunge nani sema basi mama yako watamfata tu ili urizike naona povu
 
Acha ufala unataka wakamuunge nani sema basi mama yako watamfata tu ili urizike naona povu
JF Sio mahali pakutukana matusi bali pakujenga hoja za msingi kwa Taifa lakini wewe kwa sababu umeahidiwa buku 7 kwa kila tusi basi endelea. Unajifanya hujui kuwa wanasinii wengi hapa Tanzania wanailalamikia serikali ya ccm kuhusu kuto kufaidika na kazi zao za sanaa? pole ndugu.
 
Umesahau kusema kwa miaka miwili mfululizo na huu ni wa tatu anaenda


Sent from my iPad using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom