Stergomena Tax: Serikali ipo hatua za Mwisho kutoa hadhi maalum kwa Diaspora

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,850
12,086
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 36 leo Mei 30, 2023.

Upatikanaji wa Dawa kwa Wazee
Akijibu swali Bungeni kuhusu namna ambavyo Serikali inajipanga kutatua changamoto ya ukosefu wa dawa kwa wazee kwenye vito vya afya, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel amesema dawa ambazo hazikuwa zinatolewa kwenye vituo vya Afya na Zahanati sasa zitatolewa huko, pia wahudumu watajengewa uwezo ili kutoa dawa sahihi kwa wazee kulingana na magonjwa yao.

Aidha, Dtk. Mollel amesema wazee wapo kwenye sehemu ya mpango wa Bima ya Afya kwa wote, hivyo watakuwa miongoni mwa wanaufaika wa mpango huo baada ya kukamilika.

Diaspora kupewa hadhi Maalum
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Stergomena Lawrence Tax amesema Wizara ipo kwenye hatua za mwisho kuwapatia hadhi maalum Diaspora yenye asili ya Tanzania na Diaspora wenye uraia wa Nchi nyingine.

Hadhi maalum inayoandaliwa imezingatia mapendekezo yote yaliyotolewa na Diaspora. Nia ya Serikali ni kuhakikisha Diaspora hawa wanapata fursa na huduma mbalimbali nchini. Hadi mwisho wa mwaka huu wa fedha, hadhi hii maalum itakuwa imetolewa.
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 36 leo Mei 30, 2023.

Akijibu swali Bungeni kuhusu namna ambavyo Serikali inajipanga kutatua changamoto ya ukosefu wa dawa kwa wazee kwenye vito vya afya, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel amesema dawa ambazo hazikuwa zinatolewa kwenye vituo vya Afya na Zahanati sasa zitatolewa huko, pia wahudumu watajengewa uwezo ili kutoa dawa sahihi kwa wazee kulingana na magonjwa yao.

Aidha, Dtk. Mollel amesema wazee wapo kwenye sehemu ya mpango wa Bima ya Afya kwa wote, hivyo watakuwa miongoni mwa wanaufaika wa mpango huo baada ya kukamilika.

Mpuuzi tu huyo. siasa tu
 
Back
Top Bottom